EFM na WASAFI Wanadhalilisha Tasnia ya Habari nchini

Wale ni watu wa Burudani, mambo laini laini,michezo.Ukitaka mambo serious angalia TBC na Azam TV.
 
Masanja
Kitenge
Sijui nawaonaje
Kitenge huwa ana makelele,mimi magazeti naangalia TBC au Clouds media. Hawa wasafi na Efm wamelenga majority wale wa mtaani ,mjini waliochoka na maisha wao wanataka Burudani, vichekesho katika kila kitu.Na ndiyo walio wengi.
 
wivu wa nini, acha upoyoyo na wewe. Hivi Mtu km Kitenge au Masanja ule ni utangazaji au ukichaa. Kitenge anapiga kelele bila sababu km kichaa. Uzuri mi huwa napitaga tu siwezi kusikiliza ule upuuzi. shida yao ni elimu hakuna kitu kichwani. Mtu km Kitenge navyoona hata ungempeleka shule hawezi kuelewa, kile kichwa panzi
 
Bongo ukilenga ki profesheno,hailipi .Wasikilizaji wengi wenyewe hawana profesheno. Maisha yamewapiga wengi ...Vichekesho walau vinawafariji. Siku inapita.
Ina maana Vyombo vya habari haviwezi kuliinua hili kundi ..litaendelea kuwa wajinga! Hii ni Hatari sana Kwa mustakabali wa Taifa!
Ndio maana Wana Siasa,Wenye Dini wanawachezea wanavyotaka!
 
Ina maana Vyombo vya habari haviwezi kuliinua hili kundi ..litaendelea kuwa wajinga! Hii ni Hatari sana Kwa mustakabali wa Taifa!
Ndio maana Wana Siasa,Wenye Dini wanawachezea wanavyotaka!
Bahati mbaya, huo ndo uhalisia. Si unaona wananunua mafuta ya upako,sijui maji kitoka mto "Jordan" wakiamini maisha yao yatabadilika na wawe matajiri.
 
Mi kila niki tune E Fm nakuta matangazo ya biashara, hivi huwa wana vipindi?
 
Kitenge huwa ana makelele,mimi magazeti naangalia TBC au Clouds media. Hawa wasafi na Efm wamelenga majority wale wa mtaani ,mjini waliochoka na maisha wao wanataka Burudani, vichekesho katika kila kitu.Na ndiyo walio wengi.
So unprofessional.
 
Maana yake wajinga ni wengi ktk Taifa letu! Na Ndio wateja wao!
Basi kama ni hivyo "wajinga" watakuwa dunia nzima Kwa nyakati Kwa sababu mambo ya burudani yanafuatiliwa zaidi kuliko kitu kingine, hata channel za YouTube zenye subs wengi ni za burudani

Hata nchi iliyoendelea kama USA kuna watangazaji wengi Tu maarufu na hawana taaluma ya uandishi WA habari
Mfano mzuri ni mtangazaji Ryan Seacrest ambaye aliwahi tangaza America Top 40, huyu aliacha chuo akiwa na 19 na kujikita na utangazaji na alianza kutangaza akiwa high school.

Kwangu Mimi hizo redio naziona ni wabunifu Kwa kuwaelewa walengwa wao na nini wanachohitaji wasikilaji wanaowalenga
 
Masanja
Kitenge
Sijui nawaonaje
kitenge mbona fresh tu? Kitenge ni mtangazaji mkubwa, sema alijichanganya kwenda kwenye viredio vidogo vya mitaani ambavyo hata masafa yake yanaishia dar tu. Bora angeenda clouds angebaki kuwa mkubwa kama alivyokuwa redio one. Kama vipi aanzishe redio yake. Kwa masanja bado ni kinda sana kwenye utangazaji wa redio, bado hana expossure kwenye vipindi vya redio/tv kama mtangazaji wa kipindi. Masanja anaingia kwenye utangazaji wa redio kutokana na umaarufu wake wa komedi. Atulize kichwa kwenye fani hiyo japo ana mambo mengi ukiwemo uchungaji kanisani, ukada wa chama na ukomedi wake
 
Mimi niwe mkweli nilishaachaga kufatilia redio za bongo naona wahandishi wengi wa habari uwezo wao na reasoning capacity ni ndogo sana.
Leo hii nimeona tangazo la efm la masanja Yani ni aibu na ujinga mtu masanja anaweka u comedy huku hachekeshi hata kidogo, yule mkaka mwingine amevaa gauni la kike Sasa anafundisha Nini watoto wakiume wawe wanavaa kama wanawake hasa kipindi hichi Cha mumomonyoko wa maadili.
Tasnia inayotakiwa iwe na watu smart ni ya habari ila Tanzania Hadi mashoga Kila lokole, mwijaku eti ni waandishi wahabari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…