EFM yatangaza kumchukulia hatua Hando, yadai maoni yake kuhusu Serikali kukopa si msimamo wa taasisi

Majizo hakuwa na jinsi kwanza EFM wanapata sponsorship kubwa toka wizara ya afya kuhamasisha chanjo ya covid kupitia tamasha lao la mziki mnene. Its a lucrative sponsorship toka kwa serkalini. Serikali ndio mtoa matangazo anayelipa pesa nyingi kwenye media wote hawa hata kina millard ayo, cloudsfm wanategemea mdau mkubwa toka serikalini.

Hando ameongea ukweli na kipindi chao cha asubuhi huwa kina mizaha na kejeli nyingi hata ukimsikiliza kijana wa serikali chumvi kitenge naye huwa anamizaha minhi kufurahisha wasikilizaji. Wangekuwa wenye akili wangeliacha kama lilivyo likajulikana ni mizaha ile ya joto la asubuhi. Kilichomponza hando ni wanazengo kukata ile clip na kuisambaza kwa manufaa yao binafsi.
 
Mm Niko nasimama na majizo ,tetea media yako watu wanakudanganya tu ukishaletewa zegwe na watawala hkn mtu atakuja kukulishia lulu wako

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Et wanasema hicho kilichotokea kwa Hando ni matokeo ya ushetani wa Jiwe? Kwamba Samia anaendeleza udikteta wa Jiwe?
 
Daaah nchi cjui lini itaacha unafiki!!!
 
kipindi chao cha asubuhi huwa kina mizaha na kejeli nyingi hata ukimsikiliza kijana wa serikali chumvi kitenge naye huwa anamizaha minhi kufurahisha wasikilizaji
Kipindi kina wasikilizaji wengi hasa kwenye daladala mkuu, ongezea hapo
 
Mbona Hando amesema yeye hapendi serikali inavyokopa kopa, yani "yeye" sio "wao" au E fm.
 
Jamaa inaonekana kapiga kwenye mshono.

Na kwanini Bi Tozo na wapambe wake wakiambiwa kukopa wanakuwa wakali sana.

Hiyo inaonyesha kuna shida kubwa sana hazina ndio maana wako too sensitive watu wakiongelea deni la taifa. .
 
Hando kaongea vizuri saanaa.. sanaa.
Acheni utoto nyie CCM..
 
Of course au kwenye site Wapinzani nk maana Ile tv anakofanyia kazi haijasajiliwa Kama chombo Cha mlengo fulani au Kama ana akili angemualika mtu back kwenye kipindi ndio afikishe hayo maoni yake.
Hebu andika kwa lugha nyoofu.Sijaelewa maana ya ulichokiandika kwa kuchanganya maneno ya lugha mbili pasipo umuhimu wowote.
 
Yaani mimi na akili zangu timamu, niamini takwimu zenu zisizo na uhalisia wa hali halisi ya maisha mtaani! Am sorry for that.

Mimi niko upande wa Gerald Hando na pia Job Ndugai! Acheni tabia yenu ya kukopa kopa hovyo! Wenzenu wanakopa kwa malengo, nyinyi mnakopa ili mlipie madeni mengine! Akili gani hii!!

Wananchi wanalipa kodi! Bado mnatoza matozo ya kila aina!! Hela zote hizi mnafanyia nini? Mbona nyinyi wanasiasa mnazidi tu kutajirika, na wananchi wanazidi kuwa maskini?

Kwa nini tusiamini asilimia kubwa ya hizo hela mnazitumia kwa manufaa yenu! Na ndiyo maana mnapigia chapuo kukopa kopa hovyo?
 
Kahofia asije letewa Takukuru, NEMC, Ewura, Tanesco, Dawasco, Latra, Immigration, TRA na Polisi Kwa uchunguzi zaidi...
 
Yaani hapa ndio wamewafanya na ambao hawajui sasa wajue kuwa serikali inakopa sana.
 
Mh Rais asiruhusu huu upumbavu....maneno hayaui....
Chawa wana mambo ya kifala sana....
 
Mkuu haujanielewa tunakopa tusichoweza kurejesha tunasubiri kusainishwa mikataba ya ajabu na kusamehewa madeni, hicho ndicho cha pekee tunachokitegemea pamoja na kusamehewa madeni Ila deni linazidi kupaa kulilipa hatuwezi tunazidi kukopa tu, Cc: Job Ndugai nchi itapigwa mnada
 
Endelea kuamini hivyo hivyo,mtu akikumbatia upumbavu unamsadiaje? Probably mna level Moja ya akili Sasa Ni kuwaacha hivyo hivyo na hizo kauli zenu za Asilimia kubwa 😆😆
 
Job Ndugai, Kaka upo wapi?
Kuna kura zinakusubiri. Wee bisha tu, Treni likiondoka usije kusema....ati Ulisema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…