EFM yatangaza kumchukulia hatua Hando, yadai maoni yake kuhusu Serikali kukopa si msimamo wa taasisi

EFM yatangaza kumchukulia hatua Hando, yadai maoni yake kuhusu Serikali kukopa si msimamo wa taasisi

Majizo hakuwa na jinsi kwanza EFM wanapata sponsorship kubwa toka wizara ya afya kuhamasisha chanjo ya covid kupitia tamasha lao la mziki mnene. Its a lucrative sponsorship toka kwa serkalini. Serikali ndio mtoa matangazo anayelipa pesa nyingi kwenye media wote hawa hata kina millard ayo, cloudsfm wanategemea mdau mkubwa toka serikalini.

Hando ameongea ukweli na kipindi chao cha asubuhi huwa kina mizaha na kejeli nyingi hata ukimsikiliza kijana wa serikali chumvi kitenge naye huwa anamizaha minhi kufurahisha wasikilizaji. Wangekuwa wenye akili wangeliacha kama lilivyo likajulikana ni mizaha ile ya joto la asubuhi. Kilichomponza hando ni wanazengo kukata ile clip na kuisambaza kwa manufaa yao binafsi.
 
Mm Niko nasimama na majizo ,tetea media yako watu wanakudanganya tu ukishaletewa zegwe na watawala hkn mtu atakuja kukulishia lulu wako

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Anyooshwe huyo Hando na bwana Majizo umefanya vizuri.

Hawa Wapinzani wa Maendeleo sio wa kuchekea ,fukuza..

Eti Nchi imekopa Sana ,taahira Kama Hando anajua nini kuhusu Uchumi?

Kwa hiyo Hawa wanaotuweka grade hizi hapa Ni wajinga Ila Hando ndio mwenye akili?

Fukuza huyo atakuharibia bure 👇

Et wanasema hicho kilichotokea kwa Hando ni matokeo ya ushetani wa Jiwe? Kwamba Samia anaendeleza udikteta wa Jiwe?
 
Kiukweli nimeshangaa sana ni nini kimemtuma Majizzo kuomba msamaha kwenye public? Kuna jambo lolote baya kutoka kwa Hando? Maana yeye alisema binafsi hafurahishwi na serikali kukopokopa kama raia wa nchi ana haki ya kuishauri serikali na kutoa dukuduku lake kama katiba inavyosema.

Kwani Hando kuna sehemu kadanganya? Si kweli tunakopa? Kama hakuna ubaya kukopa kwanini Majizzo anaomba msamaha? Kama taifa tuna safari ndefu sana.

View attachment 2464611
Daaah nchi cjui lini itaacha unafiki!!!
 
kipindi chao cha asubuhi huwa kina mizaha na kejeli nyingi hata ukimsikiliza kijana wa serikali chumvi kitenge naye huwa anamizaha minhi kufurahisha wasikilizaji
Kipindi kina wasikilizaji wengi hasa kwenye daladala mkuu, ongezea hapo
 
Hayo maoni angeyaweka kwenye page yake ya IG au FB wala Sio tatizo.

Ishu ni kutumia ofisi ya mtu kutoa misimamo yako binafsi... Inaleta sintofahamu kujua ni msimmo wa kampuni au msimamo wa mtu binafsi. Kuliondoa hilo ndio wenyewe wametoa ufafanuzi.

Hayo ya kuchukuliana hatau kiofisi watajuana wenyewe kulingana na sheria na miongozo ya Sehemu za kazi. Nadhani kila mahali Kuna taratibu zake.
Mbona Hando amesema yeye hapendi serikali inavyokopa kopa, yani "yeye" sio "wao" au E fm.
 
Jamaa inaonekana kapiga kwenye mshono.

Na kwanini Bi Tozo na wapambe wake wakiambiwa kukopa wanakuwa wakali sana.

Hiyo inaonyesha kuna shida kubwa sana hazina ndio maana wako too sensitive watu wakiongelea deni la taifa. .
 
Majizo amfukuze kazi Hando, EFM ni kituo kizuri sana Cha Radio, tatizo Hando anaingia akiwa amelewa chakari halafu anaruhusiwa kuingia hewani, aweke vipimo vya kilevi mlangoni.

Na akianza kuweka kipimo hicho, akipita Hando, kitapiga alarm ambayo itafika mpaka Morogoro, na kipimo kinaweza kupiga shoti hapohapo na kuharibika
Hando kaongea vizuri saanaa.. sanaa.
Acheni utoto nyie CCM..
 
Of course au kwenye site Wapinzani nk maana Ile tv anakofanyia kazi haijasajiliwa Kama chombo Cha mlengo fulani au Kama ana akili angemualika mtu back kwenye kipindi ndio afikishe hayo maoni yake.
Hebu andika kwa lugha nyoofu.Sijaelewa maana ya ulichokiandika kwa kuchanganya maneno ya lugha mbili pasipo umuhimu wowote.
 
Ni Bora mawazo mbadala yakatoka kwa watu wenye credibility na ufahamu kuhusu Uchumi na sio kila mburula anajitokeza kuongea madwala ya Uchumi as if Kuna kitu anajua.

Hando anajua nini kuhusu Uchumi? Hando angekuwa huko Chadema na atumie Hilo jukwaa sawa.

Kati ya Hando na taasisi za Kimataifa zinazoleta takwimu Kama hizi tumuamini Nani? Wewe utamuamini huyo Hando?


Yaani mimi na akili zangu timamu, niamini takwimu zenu zisizo na uhalisia wa hali halisi ya maisha mtaani! Am sorry for that.

Mimi niko upande wa Gerald Hando na pia Job Ndugai! Acheni tabia yenu ya kukopa kopa hovyo! Wenzenu wanakopa kwa malengo, nyinyi mnakopa ili mlipie madeni mengine! Akili gani hii!!

Wananchi wanalipa kodi! Bado mnatoza matozo ya kila aina!! Hela zote hizi mnafanyia nini? Mbona nyinyi wanasiasa mnazidi tu kutajirika, na wananchi wanazidi kuwa maskini?

Kwa nini tusiamini asilimia kubwa ya hizo hela mnazitumia kwa manufaa yenu! Na ndiyo maana mnapigia chapuo kukopa kopa hovyo?
 
Kahofia asije letewa Takukuru, NEMC, Ewura, Tanesco, Dawasco, Latra, Immigration, TRA na Polisi Kwa uchunguzi zaidi...
 
Yaani hapa ndio wamewafanya na ambao hawajui sasa wajue kuwa serikali inakopa sana.
 
Uongozi wa E-FM umetangaza kumchukulia hatua Gerald Hando kutokana na kauli yake aliyoitoa kupitia E-FM kuwa hapendi Serikali inavyokopakopa hovyo na kusababisha ugumu wa maisha.

Hili suala la Mikopo ya Serikali ni jana tu hapa tulijadili sana kwamba Bunge liitake Serikali ije na maelezo ya mikopo iliyochukua kama ina baraka za Bunge au laa ili wananchi wote pamoja tuwe na picha ya pamoja kuhusu mikopo.

Kwani kuna malalamiko makubwa yaliyo sasa ni kwamba mikopo mingi imechukuliwa nje ya Bajeti iliyopitishwa na Bunge kwa mujibu wa Sheria.

Gerald Hando leo amechukuliwa hatua kwa kuhoji kuhusu Mikopo, Ndugai aliondoka kwenye kiti ya Spika kwa sababu ya kuhoji mikopo, Luhaga Mpina alikatwa jina kugombea NEC kwa sababu alihoji mikopo bungeni.

View attachment 2464630
Mh Rais asiruhusu huu upumbavu....maneno hayaui....
Chawa wana mambo ya kifala sana....
 
Acha ujinga wewe kima,lini ukisikia Serikali ya awamu ya 6 inaomba kusamehewa Deni?

Swala la China kusamehe Ni uamzi wao na wamesamehe Nchi nyingi tuu..

Na in fact Mwendazake alipobanwa na Uviko ndio alikuwa anaimba Wazungu wamesamehe madeni Mara aseme wasimamishe ulipaji madeni na Mara ampigie Rais wa China kuomba msaada nk Tena bila aibu waliturushia hizo clip..

Serikali inakopa na inalipa vile vile
Mkuu haujanielewa tunakopa tusichoweza kurejesha tunasubiri kusainishwa mikataba ya ajabu na kusamehewa madeni, hicho ndicho cha pekee tunachokitegemea pamoja na kusamehewa madeni Ila deni linazidi kupaa kulilipa hatuwezi tunazidi kukopa tu, Cc: Job Ndugai nchi itapigwa mnada
 
Yaani mimi na akili zangu timamu, niamini takwimu zenu zisizo na uhalisia wa hali halisi ya maisha mtaani! Am sorry for that.

Mimi niko upande wa Gerald Hando na pia Job Ndugai! Acheni tabia yenu ya kukopa kopa hovyo! Wenzenu wanakopa kwa malengo, nyinyi mnakopa ili mlipie madeni mengine! Akili gani hii!!

Wananchi wanalipa kodi! Bado mnatoza matozo ya kila aina!! Hela zote hizi mnafanyia nini? Mbona nyinyi wanasiasa mnazidi tu kutajirika, na wananchi wanazidi kuwa maskini?

Kwa nini tusiamini asilimia kubwa ya hizo hela mnazitumia kwa manufaa yenu! Na ndiyo maana mnapigia chapuo kukopa kopa hovyo?
Endelea kuamini hivyo hivyo,mtu akikumbatia upumbavu unamsadiaje? Probably mna level Moja ya akili Sasa Ni kuwaacha hivyo hivyo na hizo kauli zenu za Asilimia kubwa 😆😆
 
Job Ndugai, Kaka upo wapi?
Kuna kura zinakusubiri. Wee bisha tu, Treni likiondoka usije kusema....ati Ulisema
 
Back
Top Bottom