mwana ally
JF-Expert Member
- Jan 30, 2014
- 363
- 119
Je nisipokata yai vipande viwili kama ulivyosema ktk step one itakuwaje. Na nikiangalia step 4 baada ya kupakaza unga ..kuna kuweka mayai... halafu tena step 6 kuna kuchovya ktk mayai tena. Msaada tafadhali Fakhrina.....swali halijaisha....
Asante dada. Hapo kwenye kukata vipande viwili vya mayai..je nikiweka zimaa? na vipi kuhusu bread scrumbs zinawekwa wapi na wakatu gani
Shukraaan Fakhrina. ngoja nijaribu feed back itakuja.
Mahitaji
1)Mayai yaliochemshwa (kata pande 2 kila yai)
2)Viazi
3)Mayai mabichi
4)Garam massala
5)Pilipili manga
6)Pilipili ya kuwasha
7)Limao au ndimu
8)Bread crumbs au unga wa ngano
9)Chumvi kiasi
10)Mafuta ya kupikia
Namna ya kutaarisha
1)Chemsha viazi hadi kuwiva then bonda bonda hadi iwe laini
2)Add chumvi,garam masala,pilipili na ndimu...changanya vizuri
3)Then tengeza duara kwa hivo viazi then weka kipande cha yai kati...weka pembeni
4)Pakaa unga hizo round za viazi na mayai....
5)Weka mafuta katika karai jikoni yapate moto
6)Vunja mayai then yachanganye vizuri....then chukua hizo round tia kwenye mayai hakikisha mayai yanaenea vizuri
7)Dumbukiza katika karai na kaanga hadi ziwe brown
8)Egg chops tayari kwa kuliwa
Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
Vp kama nitakosa hiyo garam massala pishi halitapendeza?
Hahaa kumbe hata wewe..mi huwa nakasirika sipiki tena naona like hiki kitu ni kigum
sikiwezi tena..hii imenifanya nisijue kupika mapishi mengi kwa kweli
hahaaaa, tupo wengi mama, mie kachori walaaaa cna hamu tena kitu kilichonitenda, cthubutu tena
Uwiiii!! Umenikumbusha mbali best,wakati najifunza kachori zilivyokuwa zinatawanyika.
Shida yangu mie napenda mno kucheka,ukisikia kicheko na niko mwenyewe jikoni ujue mambo yameshaharibika,nitacheka mpaka nitoe machozi ila kesho niajaribu tena!!!
Kutokata tamaa ndio siri kubwa
Nambie tatizo lako plz
yaani zinatawanyika tu na kunywa mafuta, nilichoka mwili na roho, hata cjui nlikosea wapi
Umetengeza uji ule wa kuchomea mlaini sana next fanya mzito kiasi then add yai hii inasaidia sizivurugike