Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Niliwahi kuwa na tatizo hili kwa kipindi kirefu sana, lkn baada ya kuhangaika sana kutafuta tiba yake nikaja kuambiwa tiba yake ni mazoezi tu kwa sana, na kweli naweza kusema 100% yalinisaidia kuchelewa kufika kileleni.
Ila nikiacha mazoezi kwa muda nikikutana na unyago hali inarudi kuwa ya mwanzo,kwa hiyo nimekuwa mtu wa mazoezi karibu muda mwingi kulinda uwezo wangu, na kuna muda nikiwa sawa sawa hasa kimazoezi mchuchu anaweza kudhani namkomoa maana wageni huwa hawaji nabadili mitindo tu. Mkuu mimi yalinisaidia mazoezi na ndiyo nguzo yangu kuu mpaka sasa kuchelewa kufika kileleni,vinginevyo bint alikuwa ananikimbia maana alishaanza kusema hawezi kuivumilia hali hiyo.
Lakini sasa hivi mimi ndio kidume maana mchuchu wangu keshafikia kusema; "kuna muda nasikia hamu na wewe lkn huwa najiuliza kukupa unyago maana ukikaa hapo juu hubanduki", mkuu, sijala pili pili mtama wala iliki wala kitunguu swaumu wala nyanya chungu,ni mazoezi tu.
Na ilinichukua kama wiki 3 au mwezi hivi wa mazoezi kupata matokeo hayo,ila nilikuwa nafanya mazoezi sio masihara.
Sasa sijui kwako wewe,maana binaadam tumeumbwa tofauti tofauti,lkn kwangu ndio tiba yangu mpaka nnavyoandika ujumbe huu.
Mkunga,Punguza papara, fanya maandalizi ya kutosha, kula balanced diet hususan natural foods, acha sigara/pombe. Ukiweza kunywa asali na mdalasini itakusaidia ndugu yangu. Hili ni tatizo la kisaikolojia zaidi...
Mazoezi yangu ni ya namna gani?
Mkuu ni haya haya wanayofanya wengine,ila bahati nipo ughaibuni gym kila kona na vifaa vyote vya mazoezi vipo kama unavyojua,nilichofanya nilitafuta gym ya mbali na makazi yangu (ingawa ya karibu na makazi ipo) kutoka kwangu kuifata gym ilikuwa kama km.10 au 11 hivi, nilikuwa natumia baiskeli kwenda kwenye hiyo gym.
Nikifika gym nilikuwa nakimbia kwenye running machine km. 10 au 12 kwa nusu saa,nikimaliza napumua kdg (kumbuka nilianza taratibu mpaka kuja kufikia hatua hiyo) halafu naenda kwenye bench press,napiga mizunguko 5,kila mzunguko nanyanyua mara 10. na nilianza na kilo 40 ss hivi 80. na kwenye hii bench press na mazoezi mengine kuna siku nilikuwa nafanya zaidi kama mwili upo sawa sawa (sijachoka na kazi).
Nikimaliza nakwenda kwenye mashine ya msuli wa kutengeneza paja,nayo round zake inakuwa kama ya bench press, nikimaliza napiga 21 mazoezi ya kutengeneza nguvu za mikono, mazoezi haya yana sehemu tatu tofauti jumla ya yote mazoezi ya mkono unapiga kama 105 hivi.
Nikimaliza napiga ya kutengeneza mabega,hii nayo round zake kama bench press, baada ya hapo nafanya mazoezi ya misuli ya tumbo (mara nyingi hili ndio huwa zoezi la mwisho),kama pumzi bado nnayo ya kutosha huwa napiga push-up 150 kama nimechoka napiga kulingana na uwezo wa mwili baada ya hapo nafanya stretching napumua kdg,naenda kujimwagia maji nachukua baiskeli kurudi nyumbani.
Lakini naamini kukimbia ndio kulinisaidia(na bado inanisaidia) sana kuweza kuumudu unyago ingawa mengine yalichangia,na kwa wiki nilikuwa naenda gym mara 4 ikiwa pungufu mara 3 mpaka kufikia hali hiyo.
Zaidi ya kuumudu unyago,nimekuwa mwepesi sio kawaida na body yangu kwa sasa nashukuru sio mwili yenze yenze (kizembe zembe).
Jambo la kupendeza zaidi ni mm ni mtu wa martial arts kwa kama miaka 7 iliopita kwa hiyo mazoezi haya yananifanya kuwa mwepesi zaidi nikiwa dojo,ingawa sensei wetu (mwalimu wa martial arts) ni mtu mzima kwa hiyo anatufanyisha mazoezi sio kivile,lkn ya kwangu binafsi yamenifanya niongeze kitu fulani.
Haya ndio mazoezi yangu mkuu ulieuliza na ndio dawa ambayo naiamini kwa 100% imenifanya niumudu unyago,kwanini naamini hivyo? nikiacha kbs kufanya mazoezi perfomance inakuwa mbovu,lkn nikiwa sawa sawa bint anajiuliza kunipa unyago.
Sasa sijui kwa mdau alietaka msaada na wengine maana kama nilivyosema mwanzo,binaadam tumeumbwa tofauti.