El Salvador yakamata tani 6.6 za cocaine, meli iliyobeba unga ina bendera ya Tanzania!

El Salvador yakamata tani 6.6 za cocaine, meli iliyobeba unga ina bendera ya Tanzania!

Ipo sheria inazihusu meli kusajiriwa Nchi yeyote hata kama wamiliki sio Watanzania miaka ya nyuma meli za Korea Kaskazini nyingi zilikua na usajiri wa Tanzania na wanaweka bendera yetu mpaka walipoambiwa wasifanye hivyo na Serikali ya Tanzania...
Meli nyingi za kubeba mafuta za Maduro alizipa usajiri wa Russia hata hiyo moja ambayo wameingia kwenye mgogoro na USA ni ya Venezuela ila usajiri na bendera ya Russia.
Inawezekana, lakini majuzi mkurugenzi wa kuzuia madawa ya kulevya alikua analalamika kuwa maisha yake yapo hatarini. Jaribu kuwaza kwa unyeti wa nafasi yake lakini anatumiwa meseji za vitisho, TCRA wapo wapi kufatilia hizo namba na kujua wahusika?
 
Rekodi Yavunjwa, Wakamatwa wakisafirisha kokeni yenye thamani ya dola milioni 165

View: https://m.youtube.com/watch?v=1ve3bYAP9q8
Tani sita nukta sita za kokeni zenye thamani ya dola milioni 165 zilikamatwa na Jeshi la Wanamaji la Kitaifa la El Salvador kwenye meli iliyoko kilomita 703.7 kusini-magharibi mwa Bocana El Cordoncillo, katika lango la Jaltepeque, kulingana na Rais Nayib Bukele.

Ubalozi wa Marekani huko El Salvador ulielezea operesheni hiyo kama pigo kwa uhalifu wa kimataifa unaochangia usalama wa pande zote mbili.

Meli hiyo yenye bendera ya Tanzania yenye urefu wa mita 54, ilikuwa imebeba dawa hizo za kulevya katika vifurushi 330 vilivyofichwa kwenye vizimba vya ballast vya kubalansi meli, na kuwalazimisha wapiga mbizi wa Jeshi la Wanamaji kuzama chini ili kutoa dawa hizo.
1771966309337.jpeg

Seis punto seis toneladas de cocaína valoradas en 165 millones de dólares fueron decomisadas por la Marina Nacional de El Salvador en un buque ubicado a 703.7 kilómetros al suroeste de la Bocana El Cordoncillo, en el estero de Jaltepeque, según informó el presidente Nayib Bukele.

La embarcación con bandera de Tanzania-África, de 54 metros de largo, trasladaba el narcótico en 330 bultos ocultos en tanques de lastre, lo que obligó a buzos de la Marina a sumergirse para extraer la droga.

La Embajada de Estados Unidos en El Salvador calificó el operativo como un golpe al crimen transnacional que contribuye a la seguridad hemisférica.
 
Si mnasema si ishu kuchukua bendera ya nchi nyingine na kuichomeka kwenye meli yako ili tu uzugie mambo yapite. Labda hiyo meli si ya tanzania wameamua tu kuweka bendera wasishitukiwe
Mpaka wamefikia hapo wamepita sehemu kadhaa..2.wakipita kama wana benders yenu na docs lazima zinaonyesha mizigo frm benders hapa nabaki kimya mjukuu wa mwandamboo
 
Wakuu,

Bendera ya Tanzania kuwa kwenye meli hii inamaanisha nini na ina athari gani kidiplomasia? Na hiyo mizigo hapo chini imefungwa kwa bendera yetu pia?🤔

====

View attachment 3548239

Rais Gustavo Petro ametangaza kuwa nchi ya Colombia imekamata takriban tani 7.25 za cocaine katika operesheni kubwa ya kimataifa, inayotajwa kuwa inaweza kuwa kashfa kubwa zaidi ya ukamataji wa dawa za kulevya kwa siku moja katika historia ya biashara hiyo.

Source: NTD News
Inaweza huo mzigo kuwa na connection na Bongo lakini pia inaweza kuwa hauhusiani kwa maana ya mzigo ila kampuni ya meli imekuwa registered Bongo(Ensign) hence the TZ flag.
 
Inawezekana, lakini majuzi mkurugenzi wa kuzuia madawa ya kulevya alikua analalamika kuwa maisha yake yapo hatarini. Jaribu kuwaza kwa unyeti wa nafasi yake lakini anatumiwa meseji za vitisho, TCRA wapo wapi kufatilia hizo namba na kujua wahusika?
Inategemea vitisho katoa nani, TZ kuna watu untouchable.
 
Tanzania imekuwa inahusishwa na meli za ma-deal ya kihalifu kuanzia madawa ya kulevya, meli za mafuta ya magendo yaliyowekwa vikwazo n.k

 
Habari zote hizi kuhusu nchi yetu zinachosha sana kusoma nyakati hizi.

Kitu pekee kinachotia matumaini kwenye taarifa kama hii ni kwamba hizi zote ni dalili za kulikomboa taifa hili.

Hatuwezi kwenda chini zaidi kama taifa, zaidi ya hapa tulipofikia sasa hivi.
 
Kama taifa ni lini tulikua na meli kubwa kiasi hicho ukichana na Ziwa victoria na Tanganyika?
Wewe hujui biashara ya meli inayofanywa na Jamhuri ya watu wa Zanzibar kwa niaba ya waTanzania wote?

Huna hata akili ndogo ya kukuongoza kujuwa kuwa hiyo meli yenye bendera ya Tanzania siyo ya kwanza kuhusishwa kwenye maswala ya kihalifu?
 
Wewe hujui biashara ya meli inayofanywa na Jamhuri ya watu wa Zanzibar kwa niaba ya waTanzania wote?

Huna hata akili ndogo ya kukuongoza kujuwa kuwa hiyo meli yenye bendera ya Tanzania siyo ya kwanza kuhusishwa kwenye maswala ya kihalifu?
We ndo Mpumbavu hakuna hata mtanzania mmoja aliyekamatwa in connection na dawa hizo bendera ni Geresha tuu mbona rahisi sana kuelewa? Na hakuna mtanzania aliyehusishwa
 
We ndo Mpumbavu hakuna hata mtanzania mmoja aliyekamatwa in connection na dawa hizo bendera ni Geresha tuu mbona rahisi sana kuelewa?
Bendera kwenye meli hutumiwa kwa sababu zipi, hujui? "Flag of convenience". Zanzibar inafanya biashara ya kuweka bendera yetu kwenye meli hizo, hilo nalo hujui?

Unajulikana siku zote kuwa huna akili, kwa hiyo siwezi kukusaidia chochote kilaza kama wewe.
 
Back
Top Bottom