Electrical eel samaki anayetoa umeme

Electrical eel samaki anayetoa umeme

Huyo samaki aligundulika miaka mingi tu anatoa kiasi fulani kuendana na umri wake, wataalam waliwakusanya wengi kwenye bwawa maalum kwa makusudi ya kuwatumia kama chanzo cha kuzalisha nishati ya umeme.

Lakini ilikuja kugundulika wanatoa shoti mara moja tu ukiwagusa na ukiwagusa tena hawatoi shoti yoyote sababu wanajua wewe ni msumbufu tu so walivyowaweka kwenye hilo bwawa walitoa shoti mara moja tu na walipoendelea kuwashtua hawakutoa shoti tena hivyo mradi ukafa. Hii Habari ya 2003

Anaitwa electric eel fish
animals-electriceel-slide3-web.jpg
 
wazungu wamefanya project nyingi za kutaka kuwatumia kuzalisha umeme haijawezekana mpaka leo, sio muda wote hao electric fish huwa wanatoa shoti, hiyo ni kama defense mechanism wanapoona hatari.
Ni sawa na paka kutoa makucha yake anapoona hali ya usalama si shwari au pale anapowinda, akipatikana mtu wa kuwafanya wawe katika defense mode yao kila saa inawezekana kabisa kupata umeme kutoka kwa hao samaki
 
nilijua hili nikiwa form 1 mwaka 1978
Mtofautishe voltage na current ni kweli eel electrical fish yupo

Sent using Jamii Forums mobile app
Wapo samaki zaidi ya aina tano wanaotoa umeme range ya 10 to 600 voltage wanaitwa strongly electric fish na weak electric fish Nafikiri huyu eel ambaye ndio kati ya waliopo kwenye strong electric fish amegundulika miaka hiyo ya 90
 
Nimepata Mengine Kuhusu Huyo Samaki Kuna Mtu Kajamba Kwenye Basi Nimechefukwa Unanuka Zaidi Ya Kunuka Subirini Nawaletea
 
Achilia mbali huyu samaki, JF tuna jamaa mtemacheche/umeme anaitwa mshana jr, yeye ni balaa Zaidi kwani anatuma umeme kwa barua pepe pia.
 
swali la kujiuliza umeme wa huyu samaki unatokea wapi yaani source ya umeme wake
GOD IS GREAT

then mleta uzi ukiandika tulia kidogo maana kuna typing errors kadhaa hapo

Do Something 2day That Your Future Will Thank You 4
 
Mmeamkaje? Kweli Mungu Anaumba.From Natgeo Tv Wanetoa Documentary Ya Samaki Umewe Yani Electric Eel.Ukimgusa Anakupiga Shoti Ufe Kabisa Unazikwa.
nachukia sana aina hii ya upotoshaji. Huyo samaki hana uwezo wa kuzalisha umeme wa kuua mtu.

In the electric eel, some 5,000 to 6,000 stacked electroplaques can make a shock up to 860 volts and 1 ampere of current (860 watts) for two milliseconds. Such a shock is extremely unlikely to be deadly for an adult human, due to the very short duration of the discharge. Atrial fibrillation requires that roughly 700 mA be delivered across the heart muscle for 30 ms or more, far longer than the eel can produce.
 
Huyu samaki kweli yupo, lakini hana current ya kuweza kuua, kwa wale wataalam wa electronics tunaelewa kuwa kinachoua ni current na sio voltage.

Jamii Forums mobile app
 
ELECTRIC EEL

Huyu ni samaki mwenye umeme yani mwili wake unatengeneza umeme wenye nguvu ya volt 600.
Wanapatikana bara la Amerca kusini

Kisayansi wanaitwa "Electrophorus electricus" hawa samaki wala nyama yaani carnivores wanaurefu wa futi 5-8

Miili yao imeundwa na organs zipatazo 6000 ambazo ndani yake zina cell ziitwazo "electrocytes" special kwa ajili ya kugenerate umeme ambao hutumika kukamatia prey na kujikinga na predators

Wanaishi kwenye mabwawa na maji katika mito ya amerca kusini chakula chao kikuu ni samaki na ndege
hawaoni vizuri hvyo muda wa chakula hutoa kama volt kumi kuijua direction ya prey pale atakapopigwa shoti

Wanaua sana mamba na samaki wengine kwasababu mamba anapokamata hupigwa shoti mfululizo ambapo husababisha kifo hata binadamu pia walishauliwa na hawa samaki kwa kuendelea kumshika wakati wa shoti ambapo hupoozesha mapigo ya moyo

Uzao wao ni wa tofauti sana na samaki wengine wakati wa kutaga mayai jike hutaga kufikia mayai 17,000 na hutotoa watoto wapatao 1200 na muda wote kiota kinakua kimezungukwa na ulinzi ambao ni mate ya dume

Wanaishi miaka 10-15

VIDEO (download kwa chini ya maelezo)

Huyo ndo electrical eel ni samaki ambae hana noma usimpomgusa, sasa mamba hasa hawa alligator hawajui kwamba huyu ni umeme unaotembea mamba akajua msosi umejileta

umeona kilichompata? (Download video)

amekula shoti za kutosha mpka kafa hapo hapo ndani ya sekunde 30 hapo ndio eel katoa volt 600

Umeme tu wakaida wa volt 220 wa (tanesco) unaua sasa jiulize huu wa samaki ambao ni 600-650 volt inakuaje??
.
Lakini sehemu za brazili wanamla ila wanamuua na kumuacha baada ya masaa nane..

Follw us on instagram Thewildlife_tz
5fb89ff714b93eacbaec4499a786847e.jpeg
 

Attachments

  • thewildlife_tz-20190426-0002.mp4
    7.3 MB
Back
Top Bottom