Electrical eel samaki anayetoa umeme

Electrical eel samaki anayetoa umeme

Hatuwezi kuwafuga kwenye dimbwi tukawawekea nyimbo ya rayvany ya tetema wakawa wanatoa umeme tuunganishe kwenye grid
 
ELECTRIC EEL

Huyu ni samaki mwenye umeme yani mwili wake unatengeneza umeme wenye nguvu ya volt 600.
Wanapatikana bara la Amerca kusini

Kisayansi wanaitwa "Electrophorus electricus" hawa samaki wala nyama yaani carnivores wanaurefu wa futi 5-8

Miili yao imeundwa na organs zipatazo 6000 ambazo ndani yake zina cell ziitwazo "electrocytes" special kwa ajili ya kugenerate umeme ambao hutumika kukamatia prey na kujikinga na predators

Wanaishi kwenye mabwawa na maji katika mito ya amerca kusini chakula chao kikuu ni samaki na ndege
hawaoni vizuri hvyo muda wa chakula hutoa kama volt kumi kuijua direction ya prey pale atakapopigwa shoti

Wanaua sana mamba na samaki wengine kwasababu mamba anapokamata hupigwa shoti mfululizo ambapo husababisha kifo hata binadamu pia walishauliwa na hawa samaki kwa kuendelea kumshika wakati wa shoti ambapo hupoozesha mapigo ya moyo

Uzao wao ni wa tofauti sana na samaki wengine wakati wa kutaga mayai jike hutaga kufikia mayai 17,000 na hutotoa watoto wapatao 1200 na muda wote kiota kinakua kimezungukwa na ulinzi ambao ni mate ya dume

Wanaishi miaka 10-15

VIDEO (download kwa chini ya maelezo)

Huyo ndo electrical eel ni samaki ambae hana noma usimpomgusa, sasa mamba hasa hawa alligator hawajui kwamba huyu ni umeme unaotembea mamba akajua msosi umejileta

umeona kilichompata? (Download video)

amekula shoti za kutosha mpka kafa hapo hapo ndani ya sekunde 30 hapo ndio eel katoa volt 600

Umeme tu wakaida wa volt 220 wa (tanesco) unaua sasa jiulize huu wa samaki ambao ni 600-650 volt inakuaje??
.
Lakini sehemu za brazili wanamla ila wanamuua na kumuacha baada ya masaa nane..

Follw us on instagram Thewildlife_tzView attachment 1081515

Kigoma pia wanapatikana lake tanganyika
 
Mkunga aina ya poraquê (Electrophorus electricus) anaweza zalisha volts 650 za umeme. Samaki huyu hutumia umeme kujikinga dhidi ya maadui zake. Anaweza kukua hadi kufikia urefu wa mita 1.8. Anaishi kwenye maji baridi na anapenda mazingira ya tope. Wale wanaoishi kwenye maji chumvi maarufu kama Ibrahimu huzalisha volts220 tu

Makazi ya samaki huyu ni kwenye tope, pigo moja la samaki mkunga linatosha kumfanya mtu akose nguvu na azame majini, akipiga mara tatu ana uwezo wa kumuua mwanadamu

Inasemekana kuwa wale tunawaita chunusi, ni huyu samaki anapompiga shoti mwanadamu na kufanya mtu azame majini na kufa. Na kwa kuwa samaki hawa huishi kwenye tobe, watu wengi wanataja chunusi huwa ni maeneo ya tope ambayo ndio makazi ya mkunga

Samaki huyu ni kiumbe aliyevunja rekodi ya kuzalisha umeme mwingi

Samaki huyu amevunja rekodi ya kuzalisha umeme mwingi kati ya viumbe wote
 
Back
Top Bottom