KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Mkuu 'Monk" tusiweke huu mjadala uwe kama ni wa mabishano. Tueleze tu tunachokijua kwa uzoefu/elimu inavyotuonyesha kuhusu ugonjwa wenyewe.Umejibu vema sana na nnashukuru kwa mchango wako mkuu.
Kwanza kabisa, naomba nikutaarifu kwamba nilishaugua huu ugonjwa na nikapona, nnavyokwambia hofu inawamaliza watu na kufanya hali iwe mbaya zaidi nnaelewa nnachokisema.
Tokea mwaka huu uanze, umetumia usafiri wa public? Tafiti zilizosababisha tukaambiwa tutadondoka kama kuku na maiti zitazagaa si ni hizo hjzo projection za kisayansi? Na kimsingi kwa tunavyoishi na tafiti za kitaalam zinavyoelekeza, iliktakiwa tupukutike, tumeendelea kujazana bila kuzingatia tahadhari kama tulivyoambiwa na wataalam kwamba uongonjwa unaenea kwa hewa. Niambie kitu gani kimezuia tusipukutike kwa kasi kama tafiti zinavyoelekeza pale njia zilizopendekezwa zinapokiukwa.
Maana ya chanjo ni nini mkuu? Achilia mbali ya Covid-19, neno vaccination linamaanisha nini kwako kama mtafiti?
Hakuna mahali nimetaja kujifukiza...ili uelewe swali langu, naomba nieleze Covid-19 ni ugonjwa wa aina gani, dalili zake ni zipi na unaambukizwa kwa njia gani? Naomba urejee tafiti za kitaalam lakini pia utumie akili yako vizuri kwa sababu ntakurudisha kwenye maswali ya kawaida na hali halisi, uwe tayari kuhusianisha nadharia za utafiti na ntakayoyauliza baada ya maswali yako.
Nimeuliza hayo maswali sio kwamba nabeza hizo tahadhari au kutokuthamini kinga, swali ni kwamba, tunauelewa huu ugonjwa vizuri na tunatumia njia sahihi kupambana nao? Hapo ndio msingi wa maswali yote haya. Wengi sasa hivi dalili tulizoambiwa ndio za Covid 19 hatuzioni tena, watu hawakohoi, hawana mafua, ni homa, viungo kuuma, mahuti na kukutwa na mauti. Bado tunaambukizana kwa hewa?
Ngoja nikujibu tena hatua kwa hatua uliyoyaeleza hapa, kama ninavyoyajua mimi:
1. Mimi kadri nijuavyo, sijawahi ugua huu ugonjwa, lakini inawezekana pia nikawa nimeugua huu ugonjwa bila ya kujua kuwa ndio uliokuwa unanisumbua kipindi fulani, kwa sababu sikwenda kupima, lakini nilichukua tahadhari zote za kuzuia watu waliokuwa karibu nami nisiwaambukize.
Kwa vile sikwenda hospitali, na wala sikupimwa vipimo vyoyote, siwezi kukana/kukubali kwa hakika kwamba nilishaugua au sijawahi ugua ugonjwa huo.
Kumbuka, sio watu wote wanaoambukizwa huo ugonjwa wanapata dalili na ukali sawa juu ya ugonjwa wenyewe.
Kwa kumalizia hili- kuugua kwako huo ugonjwa, haikupi ufahamu ya ugonjwa huo kamilifu. Unachoweza wewe kueleza ni jinsi ulivyojisikia dalili zake, ambazo zinaweza kuwa ni tofauti na za mtu mwingine.
2. Matumizi ya "usafiri wa Public"- TAFITI ZI PI- mlizoambabiwa kwam mtado kuku?ndoka kama? Unaweza kuweka matokeo yoyote ya utafiti yaliyochapishwa kuonyesha kuwa tafiti hizo zilionyesha "watu wakidondoka kama kuku"? Hapa niseme wazi sielewi una maana gani.
"Projections", ni tofauti kabisa na matokeo ya utafiti, kwa hiyo unachanganya mambo tofauti kabisa hapa.
Hata hivyo inanibidi nikueleze kwamba COVID-19 ni ugonjwa mpya. Ni ugonjwa ambao haujawahi kutokea na ukashambulia watu na tafiti juu yake zikafanyika.
Hizo 'projections' unazozungumzia hapa zina/zilitokana na uzoefu wa magonjwa mengine ya milipuko kama ilivyoonyesha COVID-19 ilipokuwa inaanza.
Hakuna sayansi yoyote iliyokuwa imefanyika juu ya COVID-19 yenyewe, kwa sababu haikuwahi kutokea. Hayo yote ya kuvaa barakoa, matumizi ya sanitizer, maji tiririka,n.k.; yote hayo ni njia za kawaida zilizofanyiwa utafiti juu ya matumizi yake kwenye magonjwa ya milipuko kama Ebola na mengineyo.
Kwa hiyo, COVID-19, ilikuwa haifahamiki, na hadi leo hii bado tafiti zinaendelea kujua mengi juu yake. Fahamu pia kwamba, Corona iliyoanzia Wuhan, sasa hivi siyo tishio kubwa kama hii ya Delta iliyoibukia India, ambayo ni kali zaidi. Pamoja na hayo yote, nimekueleza huko juu, hali ilivyokuwa mbaya Ulaya na Marekani, ambako watu maelfu kwa maelfu walikuwa wakiathirika. Hapa kwetu, nimekueleza, hatujui kinga yetu ilitokana na kitu gani kiasi kwamba katika wimbi lile la kwanza sisi tuliponea chupuchupu, na ndio nikatoa shukrani kwa Muumba kwa kutuepusha na janga lile. Utafiti unatakiwa kufanyika, tujue, sisi tuliepuka vipi ile hali iliyotokea Ulaya na Marekani? Corona wetu hapa alikuwa ni dhaifu kuliko yule wa sehemu zile? Au Joto letu hapa ndiyo ilikuwa kinga yetu? HATUJUI, mpaka tufanye utafiti.
Ngoja niliachie hili hapa, maana nalo litakuwa gazeti refu. Lakini kama bado huoni ninachoeleza, basi huenda sijielezi vizuri kwako.
3. Unauliza, maana ya chanjo ni nini? Ni kukinga dhidi ya maambukizi na mashambulizi ya viini vinavyosababisha ugonjwa. Unaniuliza swali hili kama kejeli, au unataka ubishi juu yake?
Sasa kwa vile chanjo ya COVID-19 haizuii moja kwa moja maambukizi, ndiyo tuseme kwamba chanjo haifanyi kazi ipaswayo kufanya, hata kama wanaoambukizwa hawapati madhara makubwa kama wale ambao hawana chanjo kabisa? Hapa unatafuta ubishi, na sina muda huo.
4. Kama sasa hivi huzioni dalili za covid-19, kama ulivyoelezwa hapo mwanzo, fahamu kwamba COVID-19 ni ugonjwa mpya. Kuna mambo mengi ambayo bado hayafahamiki, kwa sababu tafiti juu yake bado zinaendelea. Pia ni muhimu utambue kwamba, COVID-19, kama inavyojulikana kuhusu magonjwa yanayosababishwa na Virusi, ana uwezo wa kujibadilisha mara kwa mara kutokana na mazingira tofauti tofauti ya maeneo anapojitokeza.
Inatosha.