Elimu bure bado ipo?

Elimu bure bado ipo?

JF Member

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2014
Posts
7,914
Reaction score
10,793
Nimepita huku kijiweni Baba mmoja hapa Dar anadai kutozwa Elfu4 kwa wiki kwa ajili ya chakula, 500 kwa ajili ya maji, 500 kwa ajili ya mlinzi, na alilipa 1,000 kwa ajili ya kitasa cha mlango (Kiliharibika wakatakiwa kuchangia). JUMLA 6,000.

Baba huyu anadai anakaa na watoto 3 na kila mtoto analipia 5,000 kwa wiki (4,000 chakula, 500 Maji, 500 Mlinzi).

Hivyo kufanya malipo kuwa 150,000 kwa kila mtoto kwa mwaka (wiki 30 za masomo mara 5,000). Ukizidisha kwa watoto watatu atalipa jumla ya 450,000. Je, elimu Bure bado ipo, Amehoji Huyu Baba?

Nilimuuliza wote ni watoto wake? Akasema mmoja wa kwakwe wengine ni wa ndugu zake.
 
Serikali mpaka leo bado inasema elimu ni bure, lakini ukipita huko mashuleni utakutana na utitiri wa michango, walimu lazima watafute pa kutokea.
 
Mwigulu tunamfahamu kuwa ulikwisha jitoa katika jukwaa hili lakini tuna hakika haipiti siku bila kuchungulia, tafadhali jibu hoja hii inakuhusu moja kwa moja!
 
Sina hakika unataka kusema nini. Ila nikuwe sawa labda utaweka wazi lengo halisi,

1. Katika maigizo ya awamu iliyopita na hata sasa haikuwepo ELIMU BORA YA BURE na ushahidi ni matokeo ya kidato cha nne ya mwaka huu.

2. Pamoja na maigizo ya elimu bure, ktk awamu ya tano hakukuwa na chakula mashuleni hivyo suala la chakula limeanzishwa awamu hii.

3. Kama ulikuwa hauijui awamu ya tano imeacha madeni makubwa mashuleni ya walinzi ambao hawakulipwa hadi sasa. Mzingo huo sasa imezilalia Manispaa/ halmashauri ambazo sasa zimetoa kibali cha michango ya walinzi.

3. Ama kuhusu kulipia kitasa ni sheria ya kawaida iliyopo hadi leo kwamba mwanafunzi akiharibu au kupoteza kifaa cha shule mzazi atawajibika kulipa.

4. Kwa maana hiyo hadi sasa hakuna kilichobadilika maana hii elimu bure bado ina mapungufu mengi Sana yakiwemo madarasa kujengwa bila kuwa na madawati ikiwafanya wanafunzi wengi kukaa sakafuni.
 
Nimepita huku kijiweni Baba mmoja hapa Dar anadai kutozwa Elfu4 kwa wiki kwa ajili ya chakula, 500 kwa ajili ya maji, 500 kwa ajili ya mlinzi, na alilipa 1,000 kwa ajili ya kitasa cha mlango (Kiliharibika wakatakiwa kuchangia). JUMLA 6,000...
Unamlalamikia nani, wakati unapata raha na mkeo hatimaye mkazaa ulitegemea nani aje kumlisha mtoto wako? Mbona unakuwa zuzu hivyo? Eti Bure huoni hata haya mwanaume na pumbu zako, mnakera! Ndio maana mnaliwa kwasababu mnapenda vya bure.
 
Ungekuwa wewe ungeambiwa Elimu Bure usinge zaaa?

Watu mkiwa na viuwezo kidogo tu mnaanza kuwaona wenzenu hawana haki kwenye jamii wala hawana haki kuhoji.

Kama huna jibu subir upewe na wewe.
 
Sina hakika unataka kusema nini. Ila nikuwe sawa labda utaweka wazi lengo halisi,

1. Katika maigizo ya awamu iliyopita na hata sasa haikuwepo ELIMU BORA YA BURE na ushahidi ni matokeo ya kidato cha nne ya mwaka huu.

2. Pamoja na maigizo ya elimu bure, ktk awamu ya tano hakukuwa na chakula mashuleni hivyo suala la chakula limeanzishwa awamu hii.

3. Kama ulikuwa hauijui awamu ya tano imeacha madeni makubwa mashuleni ya walinzi ambao hawakulipwa hadi sasa. Mzingo huo sasa imezilalia Manispaa/ halmashauri ambazo sasa zimetoa kibali cha michango ya walinzi.

3. Ama kuhusu kulipia kitasa ni sheria ya kawaida iliyopo hadi leo kwamba mwanafunzi akiharibu au kupoteza kifaa cha shule mzazi atawajibika kulipa.

4. Kwa maana hiyo hadi sasa hakuna kilichobadilika maana hii elimu bure bado ina mapungufu mengi Sana yakiwemo madarasa kujengwa bila kuwa na madawati ikiwafanya wanafunzi wengi kukaa sakafuni.
Unataka kusema Elimu bure haijawahi kuwepo?

Kitu gani kimekufanya umukumbuke mwamba kwenye huu uzi?
 
Unamlalamikia nani, wakati unapata raha na mkeo hatimaye mkazaa ulitegemea nani aje kumlisha mtoto wako? Mbona unakuwa zuzu hivyo? Eti Bure huoni hata haya mwanaume na pumbu zako, mnakera! Ndio maana mnaliwa kwasababu mnapenda vya bure.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Unataka kusema Elimu bure haijawahi kuwepo?

Kitu gani kimekufanya umukumbuke mwamba kwenye huu uzi?
Ilikuwepo awamu ya Nyerere tu, haya mengine ni maigizo.

Mwamba a.k.a Jiwe nimemkumbuka kea kuwa ndiye aliyetulisha matobgopori kuwa kwa sasa kuna elimu bure huku yakiwa ni majanga kama nilivyokupa mfano wa matekeo ya elimu bure wa zero na div four nyingi Sana, lakini pia walinzi wamedhulumika Sana na bado ni changamoto.
 
Umechanganya madawa hapa. Embu tulia kwanza uandike upya nielewe.
 
Elimu bure au elimu bila malipo? Walimu ili kuhalalisha michango wanasema wazazi wamekubaliana na wanakusanya mamilion ya pesa Kifupi mashuleni kwa sasa kunabishara kupitia wanfunzi

Sent from my ANE-LX2 using JamiiForums mobile app
 
iyo 150,000 kwa mwaka ni sawa na bure tu watu wanalipia milion 4 kwa mwaka Na hawalalamiki hapo umeshasaidiwa vya kutosha sasa na wewe lipia tu iyo kidogo. Ila next time ukumbuke kama huna uwezo wa kulipia 150,000 kwa mwaka vaa kondomu ili usije kusumbua watu.
 
Michango kama hiyo huwa inajadiliwa na kupitishwa kwenye vikao vya wazazi. Na wazazi wenye kujielewa wameshashituka kuwa elimu bila malipo inawaingiaza watoto wao shimoni.

Na michango hiyo huwa inapaswa kukusanya na kusimamiwa na wazazi wenyewe kwenye kamati zao wanazoziunda.

Ila sasa, kwa kuwa wazazi wengi wapo busy kupambana mitaani huwa wanawaachia waalimu kwa kuwa wapo karibu zaidi na mazingira ya shule.

Na wazazi wengi wanaolalamikia michango hiyo ni wale ambao huwa hawana tabia ya kuhudhuria vikao hivyo.
 
Back
Top Bottom