SoC01 Elimu bure iondolewe tupunguze tatizo la ajira

Stories of Change - 2021 Competition

DustBin

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2021
Posts
609
Reaction score
604
Janga la ukosefu wa ajira linaloikumba nchi yetu limepelekea kushuka thamani kwa elimu na kudharauliwa wenye elimu. Watu wamefikia kusema huku mtaani kwamba hakuna haja ya kusomesha watoto kama wakimaliza tunaendelea kukaa nao nyumbani na hawaajiriwi. Lakini kwa upande wa waajiri katika sekta binafsi nao wamezidi kiburi kwa wafanyakazi wao kwa kuona kuwa hawana namna nyingine kwani serikali haitoi ajira ya kuweza kutosha wahitimu wa vyuo. Nimesikitishwa kusikia kwenye shule moja ya binafsi ndugu zetu wahitimu wa vyuo vikuu wanalipwa chini ya laki moja ikiwa ni mshahara wao kwa mwezi. Na hawana chaguo isipokua kuendelea kutumika kama nguvu kazi rahisi (cheap labor).

Sasa kijana ambae wazazi wake walijinyima kwa kumhudumia masomo yake tangu anaanza darasa la kwanza, anamaliza chuo kikuu anapata kazi kwenye sekta binafsi mshahara wake wa kwanza ni chini ya laki moja. Unafikiria ni nini kitakachotokea hapo? Kumbe ndio maana matukio ya kujinyonga, na kujiua kwa sumu yameongezeka, hii inaweza ikawa ni sababu moja wapo. Hali hii ni huko kwenye sekta ya elimu, sijajua huko kwenye sekta zingine hali ipoje.

Nilishangaa sana mwaka jana kusikia kwenye jimbo fulani idadi ya waliochukua fomu ya kuwania ubunge imefika mia moja. Hao ndio vijana wahitimu wa vyuo vikuu baada ya kuona maisha ya mtaani yamezidi kubana wakaona huenda huko kwenye ubunge labda wataweza kupata unafuu. Na hivyo hivyo hali ilikua kwenye ngazi ya udiwani, hasa wakifikiria wabunge hawana kodi kwenye malipo yao ya mshahara basi hamasa inakua kubwa sana.

Wengi wametoa maoni yao kutatua janga hili au kupunguza hii hali. Mimi muono wangu umeakisi kwenye hili la elimu bila malipo (EBM). Ninavyoona ni kana kwamba suala la elimu bila malipo liliwekwa kisiasa lakini kwa namna hali ya utekelezaji unavyoendelea hivi sasa inaonesha kabisa serikali imeelemewa na mzigo huo mzito. Na kwa upande mwingine huku kuna tatizo kubwa la uhaba wa ajira. Na ndio maana serikali inajaribu kubuni namna nyingine ya kuhakikisha inapata fedha angalau ikaweza kujikwamua mpaka tukaletewa tozo za miamala.

Kwa utafiti nilioufanya kwa kutumia sampo ya eneo ninaloishi hapa mjini familia nyingi zinajiweza kugharamia malipo ya shule kama ada itarejeshwa wanao uwezo wa kuwalipia watoto wao na wakasoma bila matatizo yeyote. Ijapokuwa zipo familia chache zinahitaji msaada. Nalisema hili kwa sababu nimeona kwenye baadhi ya shule kunakuwa na sherehe kadhaa katika mwaka ambazo zinahitaji gharama ili uweze kushiriki, kama vile mahafali na wanafunzi wanachangia kwa asilimia kubwa. Safari za kitaaluma zinazofanywa na shule pia wanafunzi huchangia ili waweze kwenda, na wanachangia fedha safari zinafanyika. Hiki ni kiashiria tosha kwamba familia zina uwezo wa kulipa ile ada (karo) ya Ths. 20,000/- kwa mwaka kama itarejeshwa.

Twakwimu za awali wakati zoezi la EBM linaanza mwaka 2016 zilionesha serikali inatoa bilioni 18.8 kila mwezi kwenda mashuleni. Nilikua nawaza endapo nusu ya wanafunzi wangeachwa wajilipie wenyewe alafu nusu tuchukulie ndio idadi ya familia masikini ina maana serikali ingepeleka bilioni 9.4 mashuleni hiyo nusu nyingine inayobaki ingeweza kuingiza kwenye ajira mpya na kulipa mishahara ya walimu/wafanyakazi wengine zaidi ya elfu kumi na tatu wenye kima cha mshahara chini ya shilingi laki saba kwa mwezi.

Katika kuliendea jambo hili la kuiondoa EBM, serikali haina budi kuwa na takwimu za familia zenye umasikini wa kupindukia ambao kwa hakika hawawezi kabisa kukidhi gharama za shule. Taarifa hizo zinaweza kupatikana Tasaf au hata kwenye ofisi za halmashauri zetu.

Kufanya maamuzi haya ya kuondoa EBM ili kuongeza ajira mpya kuna faida na tija kama ifuatavyo;-

  1. Tukumbuke kuwa fedha za EBM ni fedha ambazo zikipelekwa shuleni hazirudi, tofauti na mishahara ya wafanyakazi ambayo zikishawekwa kwenye akaunti zao baada ya muda zinarudi tena serikalini kwa njia ya kodi, tozo na ankara mbalimbali ambazo wafanyakazi hulazimika kulipa kwa hali yeyote ile.
  2. Wingi wa ajira utaongeza uwezo wa familia nyingi kuweza kuhudumia wanafamilia wakiwemo na hao wanafunzi wanaosoma kwenye shule za serikali. Hivyo vijana hawa watakaoajiriwa itawasaidia kuwalipia ada ndugu zao.
  3. Kupunguza mzigo kwa serikali kwa gharama zisizo na ulazima. Kuna watu wanalipiwa gharama za elimu na serikali lakini wala hawakuhitaji huo msaada hivyo kulipiwa na serikali ni kama vile serikali inaingia gharama isiyo ya lazima.
  4. Kupunguza manung’uniko ya baadhi ya wakuu wa shule na walimu wakuu wenye shule zenye idadi ndogo ya wanafunzi. Namna fedha zinavyogaiwa mashuleni kigezo kikubwa kinachozingatiwa ni idadi ya wanafunzi, hivyo kufanya shule yenye wanafunzi wengi kupata mgao mkubwa ukilinganisha na shule zenye wanafunzi wachache. Wakati kuna baadhi ya gharama ni sawa kwa shule zote bila kujali una idadi kubwa au ndogo ya wanafunzi. Na hili ndilo lilipelekea kuwepo kwa wanafunzi hewa.
Hivyo ninaishauri serikali kuangalia kwa mara nyingine mpango wa elimu bila malipo, na ikiwezekana waufute na mfumo wa kila mwanafunzi kupa ada mwenyewe urejeshwe ili fedha hizi zitumike kutengeneza ajira mpya. Hata hivyo endapo ada na michango ya shule itarejeshwa kama awali, serikali iweke viwango maalumu vya michango. Shule zote ziwe na michango sawa kama ilivyo kwa shule za kidato cha tano na sita.

DustBin
 
Upvote 5
Hapana mkuu wasiiondoe waboreshe tù, na mitaala ibadilishwe iendane na mazingira yetu, tukisoma kwenye mazingira yetu tutaweza kujua opportunities na challenges zinazopatikana kwenye mazingira yetu hivyo kujiajiri ,you have my vote mkuu
 
EBM ina changamoto sana na imekua ni mzigo kwa serikali.., tusione aibu kuitoa. Naona kiuitoa ndio wazo zuri maana kwa sasa haiboresheki...!! Ishu ni kwamba inakula pesa nyingi mno..!!
 
Kwani mpaka serikali inasema elimu bure walikua hawajui kama wanaweza kumudu huo mzigo? au umetumwa na serikali?
 
Huo ni mpango, ni kawaida mpango usiwe kama ulivyodhani. Hivyo kuubadilisha au kuuondoa haiwi dhambi
waanze kwa kuondoa tozo kwanza maana hata huo mpango haujawa kama walivyodhani.
 
Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
Umeniwahi.. Nilikua nataka nikupe mfano huo.., kwa hiyo kuondoa EBM ni sawa tu kama inaleta hasara na kusababisha matatizo mengine makubwa. By the way mimi sio msemaji wa serikali na wala serikali haijanitu. Lakini raia nina haki ya kutoa ushauri kwenye serikali yetu
 
Kwa utafiti nilioufanya kwa kutumia sampo ya eneo ninaloishi hapa mjini familia nyingi zinajiweza kugharamia malipo ya shule kama ada itarejeshwa wanao uwezo wa kuwalipia watoto wao na wakasoma bila matatizo yeyote.

DustBin

kutokana na utafiti wako hilo jambo linaweza kutekelezeka mjini tu maana ndo sehemu unayoona watu wana uwezo wa kulipa hio ada. naona utafiti wako umewasahu kabisa watu wa vijijini.

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
kutokana na utafiti wako hilo jambo linaweza kutekelezeka mjini tu maana ndo sehemu unayoona watu wana uwezo wa kulipa hio ada. naona utafiti wako umewasahu kabisa watu wa vijijini.

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
Ni kweli...., Na ndio maana sikuoendekeza iondolewe moja kwa moja bali takwimu zichukuliwe kwani kuna familia bado ni hohehahe hivyo zinahitaji msaada..!
 
unahisi wakiangalia takwimu watu gani wanaweza kupata msamaha wa ada na kina nani watalazimika kulipa?

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Tasaf wanazijua kaya maskini..., waanzie kwao ili kuepuka discrepancies
 
Au shule za sekondari ziondolewe kwenye mpango. Serikali ihudumieshule za msingi tu. Sekondari tuendelee na kulipa ada kama kawaida
 
Janga la ukosefu wa ajira linaloikumba nchi yetu limepelekea kushuka thamani kwa elimu na kudharauliwa wenye elimu. Watu wamefikia kusema huku mtaani kwamba hakuna haja ya kusomesha watoto kama wakimaliza tunaendelea kukaa nao nyumbani na hawaajiriwi. Lakini kwa upande wa waajiri katika sekta binafsi nao wamezidi kiburi kwa wafanyakazi wao kwa kuona kuwa hawana namna nyingine kwani serikali haitoi ajira ya kuweza kutosha wahitimu wa vyuo. Nimesikitishwa kusikia kwenye shule moja ya binafsi ndugu zetu wahitimu wa vyuo vikuu wanalipwa chini ya laki moja ikiwa ni mshahara wao kwa mwezi. Na hawana chaguo isipokua kuendelea kutumika kama nguvu kazi rahisi (cheap labor).

Sasa kijana ambae wazazi wake walijinyima kwa kumhudumia masomo yake tangu anaanza darasa la kwanza, anamaliza chuo kikuu anapata kazi kwenye sekta binafsi mshahara wake wa kwanza ni chini ya laki moja. Unafikiria ni nini kitakachotokea hapo? Kumbe ndio maana matukio ya kujinyonga, na kujiua kwa sumu yameongezeka, hii inaweza ikawa ni sababu moja wapo. Hali hii ni huko kwenye sekta ya elimu, sijajua huko kwenye sekta zingine hali ipoje.

Nilishangaa sana mwaka jana kusikia kwenye jimbo fulani idadi ya waliochukua fomu ya kuwania ubunge imefika mia moja. Hao ndio vijana wahitimu wa vyuo vikuu baada ya kuona maisha ya mtaani yamezidi kubana wakaona huenda huko kwenye ubunge labda wataweza kupata unafuu. Na hivyo hivyo hali ilikua kwenye ngazi ya udiwani, hasa wakifikiria wabunge hawana kodi kwenye malipo yao ya mshahara basi hamasa inakua kubwa sana.

Wengi wametoa maoni yao kutatua janga hili au kupunguza hii hali. Mimi muono wangu umeakisi kwenye hili la elimu bila malipo (EBM). Ninavyoona ni kana kwamba suala la elimu bila malipo liliwekwa kisiasa lakini kwa namna hali ya utekelezaji unavyoendelea hivi sasa inaonesha kabisa serikali imeelemewa na mzigo huo mzito. Na kwa upande mwingine huku kuna tatizo kubwa la uhaba wa ajira. Na ndio maana serikali inajaribu kubuni namna nyingine ya kuhakikisha inapata fedha angalau ikaweza kujikwamua mpaka tukaletewa tozo za miamala.

Kwa utafiti nilioufanya kwa kutumia sampo ya eneo ninaloishi hapa mjini familia nyingi zinajiweza kugharamia malipo ya shule kama ada itarejeshwa wanao uwezo wa kuwalipia watoto wao na wakasoma bila matatizo yeyote. Ijapokuwa zipo familia chache zinahitaji msaada. Nalisema hili kwa sababu nimeona kwenye baadhi ya shule kunakuwa na sherehe kadhaa katika mwaka ambazo zinahitaji gharama ili uweze kushiriki, kama vile mahafali na wanafunzi wanachangia kwa asilimia kubwa. Safari za kitaaluma zinazofanywa na shule pia wanafunzi huchangia ili waweze kwenda, na wanachangia fedha safari zinafanyika. Hiki ni kiashiria tosha kwamba familia zina uwezo wa kulipa ile ada (karo) ya Ths. 20,000/- kwa mwaka kama itarejeshwa.

Twakwimu za awali wakati zoezi la EBM linaanza mwaka 2016 zilionesha serikali inatoa bilioni 18.8 kila mwezi kwenda mashuleni. Nilikua nawaza endapo nusu ya wanafunzi wangeachwa wajilipie wenyewe alafu nusu tuchukulie ndio idadi ya familia masikini ina maana serikali ingepeleka bilioni 9.4 mashuleni hiyo nusu nyingine inayobaki ingeweza kuingiza kwenye ajira mpya na kulipa mishahara ya walimu/wafanyakazi wengine zaidi ya elfu kumi na tatu wenye kima cha mshahara chini ya shilingi laki saba kwa mwezi.

Katika kuliendea jambo hili la kuiondoa EBM, serikali haina budi kuwa na takwimu za familia zenye umasikini wa kupindukia ambao kwa hakika hawawezi kabisa kukidhi gharama za shule. Taarifa hizo zinaweza kupatikana Tasaf au hata kwenye ofisi za halmashauri zetu.

Kufanya maamuzi haya ya kuondoa EBM ili kuongeza ajira mpya kuna faida na tija kama ifuatavyo;-

  1. Tukumbuke kuwa fedha za EBM ni fedha ambazo zikipelekwa shuleni hazirudi, tofauti na mishahara ya wafanyakazi ambayo zikishawekwa kwenye akaunti zao baada ya muda zinarudi tena serikalini kwa njia ya kodi, tozo na ankara mbalimbali ambazo wafanyakazi hulazimika kulipa kwa hali yeyote ile.
  2. Wingi wa ajira utaongeza uwezo wa familia nyingi kuweza kuhudumia wanafamilia wakiwemo na hao wanafunzi wanaosoma kwenye shule za serikali. Hivyo vijana hawa watakaoajiriwa itawasaidia kuwalipia ada ndugu zao.
  3. Kupunguza mzigo kwa serikali kwa gharama zisizo na ulazima. Kuna watu wanalipiwa gharama za elimu na serikali lakini wala hawakuhitaji huo msaada hivyo kulipiwa na serikali ni kama vile serikali inaingia gharama isiyo ya lazima.
  4. Kupunguza manung’uniko ya baadhi ya wakuu wa shule na walimu wakuu wenye shule zenye idadi ndogo ya wanafunzi. Namna fedha zinavyogaiwa mashuleni kigezo kikubwa kinachozingatiwa ni idadi ya wanafunzi, hivyo kufanya shule yenye wanafunzi wengi kupata mgao mkubwa ukilinganisha na shule zenye wanafunzi wachache. Wakati kuna baadhi ya gharama ni sawa kwa shule zote bila kujali una idadi kubwa au ndogo ya wanafunzi. Na hili ndilo lilipelekea kuwepo kwa wanafunzi hewa.
Hivyo ninaishauri serikali kuangalia kwa mara nyingine mpango wa elimu bila malipo, na ikiwezekana waufute na mfumo wa kila mwanafunzi kupa ada mwenyewe urejeshwe ili fedha hizi zitumike kutengeneza ajira mpya. Hata hivyo endapo ada na michango ya shule itarejeshwa kama awali, serikali iweke viwango maalumu vya michango. Shule zote ziwe na michango sawa kama ilivyo kwa shule za kidato cha tano na sita.

DustBin
DustBin nashauri uweke mada yako kwenye Dustbin kwani haina mchango chanya kwa msomaji na Taifa kwa ujumla.Licha ya kuelimishwa inaonekana bado haujaelimika !.Inasikitisha sana!.Ebu nikusaidie kidogo.

Lengo kuu la elimu ni kumuwezesha mnufaika wa elimu husika kufanya maamuzi sahihi ya kiujumla na maamuzi sahihi kwenye maeneo ambayo mnufaika amepata elimu husika.Suala la ajira ni matokeo ya mapokeo ya elimu husika kwa mnufaika na halina uhusiano na elimu bila malipo .

Hivyo, hakuna ulazima wowote wa kusitisha elimu bila malipo kwa upande wa Serikali. Napendekeza elimu iendelee kutolewa bure kwa ngazi husika na ngazi za juu ambazo bado hazijaguswa ili Taifa liwe na wananchi wengi Walioelimika.
 
Au shule za sekondari ziondolewe kwenye mpango. Serikali ihudumieshule za msingi tu. Sekondari tuendelee na kulipa ada kama kawaida
ukimaanisha wanafunzi wa sekondari wazazi wao ndo wana uwezo wa kuwalipia ada na wazazi wa watoto wa shule ya msingi hawana uwezo?

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
DustBin nashauri uweke mada yako kwenye Dustbin kwani haina mchango chanya kwa msomaji na Taifa kwa ujumla.Licha ya kuelimishwa inaonekana bado haujaelimika !.Inasikitisha sana!.Ebu nikusaidie kidogo.

Lengo kuu la elimu ni kumuwezesha mnufaika wa elimu husika kufanya maamuzi sahihi ya kiujumla na maamuzi sahihi kwenye maeneo ambayo mnufaika amepata elimu husika.Suala la ajira ni matokeo ya mapokeo ya elimu husika kwa mnufaika na halina uhusiano na elimu bila malipo .

Hivyo, hakuna ulazima wowote wa kusitisha elimu bila malipo kwa upande wa Serikali. Napendekeza elimu iendelee kutolewa bure kwa ngazi husika na ngazi za juu ambazo bado hazijaguswa ili Taifa liwe na wananchi wengi Walioelimika.
Kuna point nadhani sijaeleweka. Tatizo si kwamba serikali haina nafasi za ajira, hapana! Serikali inahitaji sana kuajiri watu kwa mfano kuna baadhi ya shule hazina walimu wa sayansi mpaka hivi sasa, kinachoshindikana ni kuwa serikali kwa sasa haina uwezo wa kutoa ajira hizo shida ni mishahara ya kuwalipa watatoa wapi?? Kama hivyo ndivyo, alternative iliyopo ni kwa serikali kuongeza makusanyo ya fedha kwa kutumia kodi na tozo mbali mbali au kupunguza matumizi. Miongoni mwa matumizi ambayo serikali inaweza kupunguza ni kuiondoa EBM, na kusimamisha baadhi ya miradi mikubwa.

Awali mpango wa EBM uliletwabukiwa na msukumo wa kisiasa. Mwaka 2015 EL alipita Tanzania nzima kunadi sera yake ya Elimu Bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu. JPM naye akaja na hii tuliyonayo sasa ili aendane na kani ya uchaguzi. Tulipoingia kwenye utekelezaji wa hili haikua rahisi. Huwenda msijue ugumu unaopatikana kwenye hiki kinachoitwa EBM. Niwakumbushe tu huu haukua ktk mpango mkuu wa maendeleo, ulikuja ktk harakati ya uchaguzi.....!

Kabla ya kuingia ktk utekelezaji kama ungekua ni mpango mkakati wa maendelea wa muda mrefu tungejifunza kwanza kwa chi za wenzetu wamewezaje na ilikuaje mpaka wakafikia kuutabikisha mpango huo...
 
Back
Top Bottom