SoC01 Elimu bure iondolewe tupunguze tatizo la ajira

Stories of Change - 2021 Competition

DustBin

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2021
Posts
609
Reaction score
604
Janga la ukosefu wa ajira linaloikumba nchi yetu limepelekea kushuka thamani kwa elimu na kudharauliwa wenye elimu. Watu wamefikia kusema huku mtaani kwamba hakuna haja ya kusomesha watoto kama wakimaliza tunaendelea kukaa nao nyumbani na hawaajiriwi. Lakini kwa upande wa waajiri katika sekta binafsi nao wamezidi kiburi kwa wafanyakazi wao kwa kuona kuwa hawana namna nyingine kwani serikali haitoi ajira ya kuweza kutosha wahitimu wa vyuo. Nimesikitishwa kusikia kwenye shule moja ya binafsi ndugu zetu wahitimu wa vyuo vikuu wanalipwa chini ya laki moja ikiwa ni mshahara wao kwa mwezi. Na hawana chaguo isipokua kuendelea kutumika kama nguvu kazi rahisi (cheap labor).

Sasa kijana ambae wazazi wake walijinyima kwa kumhudumia masomo yake tangu anaanza darasa la kwanza, anamaliza chuo kikuu anapata kazi kwenye sekta binafsi mshahara wake wa kwanza ni chini ya laki moja. Unafikiria ni nini kitakachotokea hapo? Kumbe ndio maana matukio ya kujinyonga, na kujiua kwa sumu yameongezeka, hii inaweza ikawa ni sababu moja wapo. Hali hii ni huko kwenye sekta ya elimu, sijajua huko kwenye sekta zingine hali ipoje.

Nilishangaa sana mwaka jana kusikia kwenye jimbo fulani idadi ya waliochukua fomu ya kuwania ubunge imefika mia moja. Hao ndio vijana wahitimu wa vyuo vikuu baada ya kuona maisha ya mtaani yamezidi kubana wakaona huenda huko kwenye ubunge labda wataweza kupata unafuu. Na hivyo hivyo hali ilikua kwenye ngazi ya udiwani, hasa wakifikiria wabunge hawana kodi kwenye malipo yao ya mshahara basi hamasa inakua kubwa sana.

Wengi wametoa maoni yao kutatua janga hili au kupunguza hii hali. Mimi muono wangu umeakisi kwenye hili la elimu bila malipo (EBM). Ninavyoona ni kana kwamba suala la elimu bila malipo liliwekwa kisiasa lakini kwa namna hali ya utekelezaji unavyoendelea hivi sasa inaonesha kabisa serikali imeelemewa na mzigo huo mzito. Na kwa upande mwingine huku kuna tatizo kubwa la uhaba wa ajira. Na ndio maana serikali inajaribu kubuni namna nyingine ya kuhakikisha inapata fedha angalau ikaweza kujikwamua mpaka tukaletewa tozo za miamala.

Kwa utafiti nilioufanya kwa kutumia sampo ya eneo ninaloishi hapa mjini familia nyingi zinajiweza kugharamia malipo ya shule kama ada itarejeshwa wanao uwezo wa kuwalipia watoto wao na wakasoma bila matatizo yeyote. Ijapokuwa zipo familia chache zinahitaji msaada. Nalisema hili kwa sababu nimeona kwenye baadhi ya shule kunakuwa na sherehe kadhaa katika mwaka ambazo zinahitaji gharama ili uweze kushiriki, kama vile mahafali na wanafunzi wanachangia kwa asilimia kubwa. Safari za kitaaluma zinazofanywa na shule pia wanafunzi huchangia ili waweze kwenda, na wanachangia fedha safari zinafanyika. Hiki ni kiashiria tosha kwamba familia zina uwezo wa kulipa ile ada (karo) ya Ths. 20,000/- kwa mwaka kama itarejeshwa.

Twakwimu za awali wakati zoezi la EBM linaanza mwaka 2016 zilionesha serikali inatoa bilioni 18.8 kila mwezi kwenda mashuleni. Nilikua nawaza endapo nusu ya wanafunzi wangeachwa wajilipie wenyewe alafu nusu tuchukulie ndio idadi ya familia masikini ina maana serikali ingepeleka bilioni 9.4 mashuleni hiyo nusu nyingine inayobaki ingeweza kuingiza kwenye ajira mpya na kulipa mishahara ya walimu/wafanyakazi wengine zaidi ya elfu kumi na tatu wenye kima cha mshahara chini ya shilingi laki saba kwa mwezi.

Katika kuliendea jambo hili la kuiondoa EBM, serikali haina budi kuwa na takwimu za familia zenye umasikini wa kupindukia ambao kwa hakika hawawezi kabisa kukidhi gharama za shule. Taarifa hizo zinaweza kupatikana Tasaf au hata kwenye ofisi za halmashauri zetu.

Kufanya maamuzi haya ya kuondoa EBM ili kuongeza ajira mpya kuna faida na tija kama ifuatavyo;-

  1. Tukumbuke kuwa fedha za EBM ni fedha ambazo zikipelekwa shuleni hazirudi, tofauti na mishahara ya wafanyakazi ambayo zikishawekwa kwenye akaunti zao baada ya muda zinarudi tena serikalini kwa njia ya kodi, tozo na ankara mbalimbali ambazo wafanyakazi hulazimika kulipa kwa hali yeyote ile.
  2. Wingi wa ajira utaongeza uwezo wa familia nyingi kuweza kuhudumia wanafamilia wakiwemo na hao wanafunzi wanaosoma kwenye shule za serikali. Hivyo vijana hawa watakaoajiriwa itawasaidia kuwalipia ada ndugu zao.
  3. Kupunguza mzigo kwa serikali kwa gharama zisizo na ulazima. Kuna watu wanalipiwa gharama za elimu na serikali lakini wala hawakuhitaji huo msaada hivyo kulipiwa na serikali ni kama vile serikali inaingia gharama isiyo ya lazima.
  4. Kupunguza manung’uniko ya baadhi ya wakuu wa shule na walimu wakuu wenye shule zenye idadi ndogo ya wanafunzi. Namna fedha zinavyogaiwa mashuleni kigezo kikubwa kinachozingatiwa ni idadi ya wanafunzi, hivyo kufanya shule yenye wanafunzi wengi kupata mgao mkubwa ukilinganisha na shule zenye wanafunzi wachache. Wakati kuna baadhi ya gharama ni sawa kwa shule zote bila kujali una idadi kubwa au ndogo ya wanafunzi. Na hili ndilo lilipelekea kuwepo kwa wanafunzi hewa.
Hivyo ninaishauri serikali kuangalia kwa mara nyingine mpango wa elimu bila malipo, na ikiwezekana waufute na mfumo wa kila mwanafunzi kupa ada mwenyewe urejeshwe ili fedha hizi zitumike kutengeneza ajira mpya. Hata hivyo endapo ada na michango ya shule itarejeshwa kama awali, serikali iweke viwango maalumu vya michango. Shule zote ziwe na michango sawa kama ilivyo kwa shule za kidato cha tano na sita.

DustBin
 
Upvote 5
kaya ni nyumba. kama hauishi na wazazi wako wewe ni kaya tofauti na hio ya wazazi wako.

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
Wewe ambae umeihama kaya tunatarajia uwe umeajiriwa ili usaidie ndugu zako kuwasomesha. Sasa hujapata ajira inakuaje hapo mkuu!?? Mzigo unarudi kwa wazazi wako ambao sasa hivi wanashindwa kuwasomesha ndugu zako... Hawa ndio serikali iwape msaada. Aidha familia zinazojitosheleza warudi kwenye ada ndio uzalendo wenyewe huo
 
DustBiKu
Mi nazani katika taiga swala la Elimu linafaa kuwa kipaumbele cha kwanza, pamoja na utafiti wako kuitoa EBM kutapunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya wasomi nchini mwetu, idadi ya wanafunz waliokuwa wanajiunga kbla ya ebm na sasa ni tofauti kubwa. Apo utagundua umuhimu wa ebm. Luna namna nyingi sana za kuwezesha fedha zikapelekwa kwenye bajeti ya ajira mpya,, mfano viongoz wetu wanalipwa mishahara mikubwa na posho ndefu,, Serial inafaa kuangalia namna ya kupata fedha za kuajir pasipo kuathiri Wananchi wanyonge
 
kukosa ajira hakuhusiani na elimu bure bali ni kukosa ubunifu wa kutafuta mbadala wake.

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
Mfumo wa elimu yetu haumuandai anaesoma kuajiriwa. Hata wanaosema sema vijana wajiajiri wao wenyewe wapo kwenye ajira.
Kujiajiri ni complex process inayohitaji muda. Kuna watu tulisoma nao primary walipofeli wakajichanganya ktk kujihangaisha saivi wamesimamia. Mimi ndio namaliza chuo mwaka huu ili nimfikie yule inabidi nipate muda wa miaka kama niliyoitumia kwenye kusoma ndio nami niweze kusimama. Hivyo watu wasiwaze tuna kusema vijana wajiajiri wakati hali ya ajira binafsi enyewe tia maji
 
Wewe ambae umeihama kaya tunatarajia uwe umeajiriwa ili usaidie ndugu zako kuwasomesha. Sasa hujapata ajira inakuaje hapo mkuu!?? Mzigo unarudi kwa wazazi wako ambao sasa hivi wanashindwa kuwasomesha ndugu zako... Hawa ndio serikali iwape msaada. Aidha familia zinazojitosheleza warudi kwenye ada ndio uzalendo wenyewe huo

yani mi naweza kumlipia mwanangu ada ila serikali iseme ada bure halafu nijifanye kiherehere niende kutangaza sihitaji msamaha wa ada? mi ntakua zamwamwa.
wao wanashindwa kuonesha uzalendo kwenye mishahara yao minono isiyokatwa kodi mimi mkatwa kodi nioneshe uzalendo?

HAKUNAGA

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Viongozi wetu wawe wazelendo, walipwe fedha kidogo ili na wengne waajiriwe waongeze nguvu kuijenga nchi,, pia mifumo ya elimu kwanzia chini iboreshwe Wasomi wawe wanauwezo was kujiajiri.. Educating Child to live a better life, not to be employed
 
Mi nazani katika taiga swala la Elimu linafaa kuwa kipaumbele cha kwanza, pamoja na utafiti wako kuitoa EBM kutapunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya wasomi nchini mwetu, idadi ya wanafunz waliokuwa wanajiunga kbla ya ebm na sasa ni tofauti kubwa. Apo utagundua umuhimu wa ebm. Luna namna nyingi sana za kuwezesha fedha zikapelekwa kwenye bajeti ya ajira mpya,, mfano viongoz wetu wanalipwa mishahara mikubwa na posho ndefu,, Serial inafaa kuangalia namna ya kupata fedha za kuajir pasipo kuathiri Wananchi wanyonge
Upo sahihi ila nikusahishe sehemu moja. EBM haijaongeza idadi ya wasomi, bali imeongeza idadi ya wahitimu wa darasa la saba na kidato cha nne. Wahitimu ambao hawana msaada kwa sababu hawana ujuzi na elimu yao ni tia maji tia maji. Hili ni kwa sababu wamesoma kwenye shule zenye uhaba wa walimu. Walimu ambao wangeajiriwa wakaongeze nguvu kazi fedha za kulipa mishahara yao imeenda kwenye EBM
 
yani mi naweza kumlipia mwanangu ada ila serikali iseme ada bure halafu nijifanye kiherehere niende kutangaza sihitaji msamaha wa ada? mi ntakua zamwamwa.
wao wanashindwa kuonesha uzalendo kwenye mishahara yao minono isiyokatwa kodi mimi mkatwa kodi nioneshe uzalendo?

HAKUNAGA

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
Aahahhhahaa... Nishakuelewa mkuu..! Wewe upo nami ila umepita njia ya kujizungusha...! Hahahhhhaaahah. Big up sana
 
Viongozi wetu wawe wazelendo, walipwe fedha kidogo ili na wengne waajiriwe waongeze nguvu kuijenga nchi,, pia mifumo ya elimu kwanzia chini iboreshwe Wasomi wawe wanauwezo was kujiajiri.. Educating Child to live a better life, not to be employed
Safi kabisa. Tuanze na wabunge..., wakatwe kodi kwenye mishahara...!!
 
Upo sahihi ila nikusahishe sehemu moja. EBM haijaongeza idadi ya wasomi, bali imeongeza idadi ya wahitimu wa darasa la saba na kidato cha nne. Wahitimu ambao hawana msaada kwa sababu hawana ujuzi na elimu yao ni tia maji tia maji. Hili ni kwa sababu wamesoma kwenye shule zenye uhaba wa walimu. Walimu ambao wangeajiriwa wakaongeze nguvu kazi fedha za kulipa mishahara yao imeenda kwenye EBM
Kwanini tutumie fedha ya ebm tu? Kwanin tusipunguze fedha za kuwalipa wabunge tukawalipa hao walimu wapya? Ili tuwe na wasomi wengi wenye tija?
 
Kwani wabunge wapo wangapi mpaka ionekane fedha zao zitakazokatwa zitoshe? EBM inatumia fedha nyingi ndio maana kuna hitajio la kuiondosha. Lakini bado hoja ya wabunge kukatwa kodi naiunga mkono
 
Kama lengo ni kupunguza wasomi uchwara wanaolilia ajira, ni vema EBM ifutiliwe mbali ili wachache wenye uwezo wa kulipia elimu tu ndo watahitimu na hivyo kupata ajira.

Kuliko kusomesha watu wote kwa gharama kubwa halafu wakitegemea uwaajiri, na hatuna mpango nao.[emoji1614][emoji36]
 
Halafu illiteracy rate iongezeke mkuu au vp?? Kwanza huu uzi ufutwe UPUUZI
 
Hhahahhaa hii komesha
 
Janga la ukosefu wa ajira linaloikumba nchi yetu limepelekea kushuka thamani kwa elimu na kudharauliwa wenye elimu. Watu wamefikia kusema huku mtaani kwamba hakuna haja ya kusomesha watoto kama wakimaliza tunaendelea kukaa nao nyumbani na hawaajiriwi. Lakini kwa upande wa waajiri katika sekta binafsi nao wamezidi kiburi kwa wafanyakazi wao kwa kuona kuwa hawana namna nyingine kwani serikali haitoi ajira ya kuweza kutosha wahitimu wa vyuo. Nimesikitishwa kusikia kwenye shule moja ya binafsi ndugu zetu wahitimu wa vyuo vikuu wanalipwa chini ya laki moja ikiwa ni mshahara wao kwa mwezi. Na hawana chaguo isipokua kuendelea kutumika kama nguvu kazi rahisi (cheap labor).

Sasa kijana ambae wazazi wake walijinyima kwa kumhudumia masomo yake tangu anaanza darasa la kwanza, anamaliza chuo kikuu anapata kazi kwenye sekta binafsi mshahara wake wa kwanza ni chini ya laki moja. Unafikiria ni nini kitakachotokea hapo? Kumbe ndio maana matukio ya kujinyonga, na kujiua kwa sumu yameongezeka, hii inaweza ikawa ni sababu moja wapo. Hali hii ni huko kwenye sekta ya elimu, sijajua huko kwenye sekta zingine hali ipoje.

Nilishangaa sana mwaka jana kusikia kwenye jimbo fulani idadi ya waliochukua fomu ya kuwania ubunge imefika mia moja. Hao ndio vijana wahitimu wa vyuo vikuu baada ya kuona maisha ya mtaani yamezidi kubana wakaona huenda huko kwenye ubunge labda wataweza kupata unafuu. Na hivyo hivyo hali ilikua kwenye ngazi ya udiwani, hasa wakifikiria wabunge hawana kodi kwenye malipo yao ya mshahara basi hamasa inakua kubwa sana.

Wengi wametoa maoni yao kutatua janga hili au kupunguza hii hali. Mimi muono wangu umeakisi kwenye hili la elimu bila malipo (EBM). Ninavyoona ni kana kwamba suala la elimu bila malipo liliwekwa kisiasa lakini kwa namna hali ya utekelezaji unavyoendelea hivi sasa inaonesha kabisa serikali imeelemewa na mzigo huo mzito. Na kwa upande mwingine huku kuna tatizo kubwa la uhaba wa ajira. Na ndio maana serikali inajaribu kubuni namna nyingine ya kuhakikisha inapata fedha angalau ikaweza kujikwamua mpaka tukaletewa tozo za miamala.

Kwa utafiti nilioufanya kwa kutumia sampo ya eneo ninaloishi hapa mjini familia nyingi zinajiweza kugharamia malipo ya shule kama ada itarejeshwa wanao uwezo wa kuwalipia watoto wao na wakasoma bila matatizo yeyote. Ijapokuwa zipo familia chache zinahitaji msaada. Nalisema hili kwa sababu nimeona kwenye baadhi ya shule kunakuwa na sherehe kadhaa katika mwaka ambazo zinahitaji gharama ili uweze kushiriki, kama vile mahafali na wanafunzi wanachangia kwa asilimia kubwa. Safari za kitaaluma zinazofanywa na shule pia wanafunzi huchangia ili waweze kwenda, na wanachangia fedha safari zinafanyika. Hiki ni kiashiria tosha kwamba familia zina uwezo wa kulipa ile ada (karo) ya Ths. 20,000/- kwa mwaka kama itarejeshwa.

Twakwimu za awali wakati zoezi la EBM linaanza mwaka 2016 zilionesha serikali inatoa bilioni 18.8 kila mwezi kwenda mashuleni. Nilikua nawaza endapo nusu ya wanafunzi wangeachwa wajilipie wenyewe alafu nusu tuchukulie ndio idadi ya familia masikini ina maana serikali ingepeleka bilioni 9.4 mashuleni hiyo nusu nyingine inayobaki ingeweza kuingiza kwenye ajira mpya na kulipa mishahara ya walimu/wafanyakazi wengine zaidi ya elfu kumi na tatu wenye kima cha mshahara chini ya shilingi laki saba kwa mwezi.

Katika kuliendea jambo hili la kuiondoa EBM, serikali haina budi kuwa na takwimu za familia zenye umasikini wa kupindukia ambao kwa hakika hawawezi kabisa kukidhi gharama za shule. Taarifa hizo zinaweza kupatikana Tasaf au hata kwenye ofisi za halmashauri zetu.

Kufanya maamuzi haya ya kuondoa EBM ili kuongeza ajira mpya kuna faida na tija kama ifuatavyo;-

  1. Tukumbuke kuwa fedha za EBM ni fedha ambazo zikipelekwa shuleni hazirudi, tofauti na mishahara ya wafanyakazi ambayo zikishawekwa kwenye akaunti zao baada ya muda zinarudi tena serikalini kwa njia ya kodi, tozo na ankara mbalimbali ambazo wafanyakazi hulazimika kulipa kwa hali yeyote ile.
  2. Wingi wa ajira utaongeza uwezo wa familia nyingi kuweza kuhudumia wanafamilia wakiwemo na hao wanafunzi wanaosoma kwenye shule za serikali. Hivyo vijana hawa watakaoajiriwa itawasaidia kuwalipia ada ndugu zao.
  3. Kupunguza mzigo kwa serikali kwa gharama zisizo na ulazima. Kuna watu wanalipiwa gharama za elimu na serikali lakini wala hawakuhitaji huo msaada hivyo kulipiwa na serikali ni kama vile serikali inaingia gharama isiyo ya lazima.
  4. Kupunguza manung’uniko ya baadhi ya wakuu wa shule na walimu wakuu wenye shule zenye idadi ndogo ya wanafunzi. Namna fedha zinavyogaiwa mashuleni kigezo kikubwa kinachozingatiwa ni idadi ya wanafunzi, hivyo kufanya shule yenye wanafunzi wengi kupata mgao mkubwa ukilinganisha na shule zenye wanafunzi wachache. Wakati kuna baadhi ya gharama ni sawa kwa shule zote bila kujali una idadi kubwa au ndogo ya wanafunzi. Na hili ndilo lilipelekea kuwepo kwa wanafunzi hewa.
Hivyo ninaishauri serikali kuangalia kwa mara nyingine mpango wa elimu bila malipo, na ikiwezekana waufute na mfumo wa kila mwanafunzi kupa ada mwenyewe urejeshwe ili fedha hizi zitumike kutengeneza ajira mpya. Hata hivyo endapo ada na michango ya shule itarejeshwa kama awali, serikali iweke viwango maalumu vya michango. Shule zote ziwe na michango sawa kama ilivyo kwa shule za kidato cha tano na sita.

DustBin
Huna akili
 
elimu bure inapaswa kutolewa bure tena kwa quality nzuri zaidi ya hii iliyopo! Binafsi sioni mahusiano ya elimu bure na ajira, shule hazifundishi ajira tuanenda shuleni kutoa ujinga ili tupate maarifa tupambane vizuri. Serikali inatimiza wajibu wake wa kutoa elimu lakini tutambua kua serikali haikufundishi ili kesho ikuajiri/ujajiriwe!

kurudisha gharama za elimu hasa kwa familia maskini ni kuzitwisha mzigo usio weza kubebeka, pamoja na elimu kua bure bado kuna familia zinashindwa kutoa hata elfu tano kuhudumia watoto wao kwenye masuala ya shule

Serikali inatimiza wajibu kufundisha watu na wao watimize wajibu wao kujiajiri kwani sio lazima kuajiriwa, hakuna graduate anaweza kosa kitu cha kufanya na kumuingizia kipato ktk nchi hii! wanaweza watu ambao hawajui hata kusoma wao kwanini washindwe! Graduate anakimbia kijijini kwao kuna resources tele anakimbilia mjini kuzunguka na mabahasha, huko ni kupoteza mda unakuta mtu pesa alizotumia kuzunguka kufanya ma applications angeweza kufungua barber shop hata ya laki tu akapata buku mbili tatu zikamsogeza huku anatafakari nmengine
graduate wengi mitazamo yao ni kuanza na mtaji wa mamilioni kitu ambacho ni ngumu

sioni mahusiano ya elimu bure na ajira! tujiongee
 
Halafu illiteracy rate iongezeke mkuu au vp?? Kwanza huu uzi ufutwe UPUUZI
Hivi hiyo illiteracy rate una ifahamu? Umefuatilia tangu mwaka 2016 ilipoanza EBM na hapo kabla ya kuwepo ipoje hiyo illiteracy rate unayoisema?
 
elimu bure inapaswa kutolewa bure tena kwa quality nzuri zaidi ya hii iliyopo! Binafsi sioni mahusiano ya elimu bure na ajira, shule hazifundishi ajira tuanenda shuleni kutoa ujinga ili tupate maarifa tupambane vizuri. Serikali inatimiza wajibu wake wa kutoa elimu lakini tutambua kua serikali haikufundishi ili kesho ikuajiri/ujajiriwe!

kurudisha gharama za elimu hasa kwa familia maskini ni kuzitwisha mzigo usio weza kubebeka, pamoja na elimu kua bure bado kuna familia zinashindwa kutoa hata elfu tano kuhudumia watoto wao kwenye masuala ya shule

Serikali inatimiza wajibu kufundisha watu na wao watimize wajibu wao kujiajiri kwani sio lazima kuajiriwa, hakuna graduate anaweza kosa kitu cha kufanya na kumuingizia kipato ktk nchi hii! wanaweza watu ambao hawajui hata kusoma wao kwanini washindwe! Graduate anakimbia kijijini kwao kuna resources tele anakimbilia mjini kuzunguka na mabahasha, huko ni kupoteza mda unakuta mtu pesa alizotumia kuzunguka kufanya ma applications angeweza kufungua barber shop hata ya laki tu akapata buku mbili tatu zikamsogeza huku anatafakari nmengine
graduate wengi mitazamo yao ni kuanza na mtaji wa mamilioni kitu ambacho ni ngumu

sioni mahusiano ya elimu bure na ajira! tujiongee
Kuna point nadhani sijaeleweka. Tatizo si kwamba serikali haina nafasi za ajira, hapana! Serikali inahitaji sana kuajiri watu kwa mfano kuna baadhi ya shule hazina walimu wa sayansi mpaka hivi sasa, kinachoshindikana ni kuwa serikali kwa sasa haina uwezo wa kutoa ajira hizo shida ni mishahara ya kuwalipa watatoa wapi?? Kama hivyo ndivyo, alternative iliyopo ni kwa serikali kuongeza makusanyo ya fedha kwa kutumia kodi na tozo mbali mbali au kupunguza matumizi. Miongoni mwa matumizi ambayo serikali inaweza kupunguza ni kuiondoa EBM, na kusimamisha baadhi ya miradi mikubwa.

Awali mpango wa EBM uliletwabukiwa na msukumo wa kisiasa. Mwaka 2015 EL alipita Tanzania nzima kunadi sera yake ya Elimu Bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu. JPM naye akaja na hii tuliyonayo sasa ili aendane na kani ya uchaguzi. Tulipoingia kwenye utekelezaji wa hili haikua rahisi. Huwenda msijue ugumu unaopatikana kwenye hiki kinachoitwa EBM. Niwakumbushe tu huu haukua ktk mpango mkuu wa maendeleo, ulikuja ktk harakati ya uchaguzi.....!

Kabla ya kuingia ktk utekelezaji kama ungekua ni mpango mkakati wa maendelea wa muda mrefu tungejifunza kwanza kwa chi za wenzetu wamewezaje na ilikuaje mpaka wakafikia kuutabikisha mpango huo...
Napenda tufahamu kuwa unemployment ni tatizo la kitaifa, sio la mtu mmoja mmoja kama tunavyodhani; na ni jukumu la serikali kuhakikisha inalisawazisha tatizo hilo. Mimi nimetoa wazo la kupunguza government expenditures kuipa serikali nafasi ya kupunguza tatizo hilo. Mahusiano yapo mbona ya wazi kabisa
 
Back
Top Bottom