Elimu bure, watoto wa wanyonge wakataliwa kuandikishwa shule huko Makambako.

Elimu bure, watoto wa wanyonge wakataliwa kuandikishwa shule huko Makambako.

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2018
Posts
17,499
Reaction score
25,295
Kengele imepigwa, muhula umeanza vituko vya zima moto kwenye elimu za watoto wa wanaoitwa masikini navyo vimeanza. ni viroja alimuradi kura zipatikane hata kwa kukwiba hapo 2020.

kuna ambao wamechaguliwa kujiunga na masomo ya sekondary lakini hawajulikani walipo, sijui taarifa za kiintellijensia zinasemaje? au nao ni hewa?

wapo waliochaguliwa lakini hajaambiwa wanaenda kusoma wapi? madarasa hakuna, ni mwendo wa kununua ndege zinazopokelewa kwa mbwembwe, tambo na mipasho mingii kana kwamba wananunua kwa pesa zao mifukoni kumbe za kwetu sie wamachinga.

Twaambiwa ni awamu ya sisis wanyonge, nasi twatembea vifua mbele hata kama mifukoni tu kapa kama matumbo yetu.

Huko makambako wananchi ambao watoto wao wamefaulu kujiunga na kidato cha kwanza WANAKATALIWA Kujiunga na Shule hadi walipie FOMU za kujiunga.(kunani tena wanyonge kunyongwa)

Alipoulizwa na wandishi Kiongozi anasema ni utaratibu wa kuchangia maendeleo. tunahoji si ELIMU BURE? Mbona mwatuchapa kwa kutuuzia fomu sisi WANYONGE si ni awamu yetu?
(chanzo cha habari hii ni UTV jana)

Hakuna nchi iliyowahi kuendelea bila kuwekeza kwenye elimu hata uwe na rasilimali nyingi kiasi gani biala elimu utatembea KIFUA MBELE MPAKA MBINGUNI UKIWA KIFUA WAZI hupati maendeleo
 
Serikali ya wanyonge bado tupo kwenye ndege kwanza, mengine yasubiri maana sio kipaumbele chetu
 
Walimu hawapandi madaraja!unafikiri watalia wapi????Ngoja kesho nidai hela za mlinzi,nembo na uji!!!SITAKAGI UJINGA MIMI!!!
 
Back
Top Bottom