ELIMU: Gari yenye Cc 650 kutumia mafuta kuliko gari yenye Cc 1300

Na ww nkumalize hakuna passo ya cc950
 
Mimi Nilikuwa nafanya kazi mahali kama Dereva Binafsi, Boss wangu alikuwa na Gari mbili Moja ni LAND CRUISE VXR 2016 Na LANDCRUISE TX 2015 Model,
Tx ya Mwaka 2015, petrol Ni balaa haitumii ufunguo inawaka kwa Batani tu hata Hivyo nilishangaa sana licha ya kuwa na engine kubwa inatumia mafuta kidogo sana.
KAWE BEACH- BAGAMOYO ni Mafuta ya 30,000 kwenda na kurudi na yanabaki mengine ya Kwenda Sinza- na kurudi kawe, Licha ya Mafuta kuwa 2350 per litre.
2. KIBITI PWANI - KAWE mafuta nilitumia ya 50,000 kwenda na kurudi na njiani speed kama nakimbiza Amburance..
Kwahiyo naamini kabisa kwamba Kuna gari licha ya kuwa na Engine kubwa lakini umeme unazalishwa Na kutumika mwingi zaidi ya Mafuta.
 
Hivi mtu unauliza kama gari inakula mafuta sasa wew ulitaka ile maji wakati yenyewe inatumia mafuta
Hakuna gari inayokula mafuta Bali matumizi yako ya gari ndio kipimo sahihi cha ulaji wa mafuta
Mm na kaa mbezi ya kimala
Na wew unakaa mbezi ya kimala
Wew unatumia Haria mm natumia Suzuki Escudo
Weka lita 10 na mm niweke 10 twende poster nakirudi halafu uone hayomafuta Kama yanatofauti


Unakuta mtu Anazunguka tu mjini bila sababu mara huku Mara kule
Halafu baadae utasikia Sarah gari inakula mafuta
Kwa nini isile nawakati wew unazunguka tu
 
...anazunguka tu mjini bila sababu.....!
 
Huenda alichanganya fuel injection vs carburetor ndio kamaanisha inatumia umeme...

Ila sidhani kama from the 90s kuna gari za carburetor

Bado iko tatizo kwenye haya maelezo
 
kwa mfano bmw mini cooper.kina cc chache halafu dashbord inasoma 240km.

hapa lazima kuna umwagaji wa tui.
 
Mkuu acha kubisha unajua mfumo wa vvti kwa Toyota unavyofanya kazi? Kama ungejua wala usingebisha
 
Aisee, mzee umevunja vunja sana hapo.

Ni hivi, iIi injini ya gari ifanye kazi vizuri (efficient) inatakiwa kuwa na uwiano mzuri kati ya mwendo na mzunguko wa injini (revolution per minute - rpm). Kwa kiasi kikubwa uwiano huu hufanywa na transmission (gearbox).

Hata hivyo tukiweka kila kitu sawa, kama unasafiri kwa mwendo mkubwa au unapanda mlima, injini ndogo itatumia mafuta mengi kuliko injini kubwa kwa kuwa injini ndogo itabidi izunguke sana (high rpm) ili kutengeneze msukumo sahihi (torque) kuiwezesha gari kwenda mwendo huo.
 
Mkuu acha kubisha unajua mfumo wa vvti kwa Toyota unavyofanya kazi? Kama ungejua wala usingebisha
Ni wazi wewe ni wale wale nafikiri hilo neno vvti ndio linakuzuzua. Btw sibishani na mtu yeyote. Haya nipe elimu ya vvti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…