Elimu ipo chuo chochote, uzito upo UDSM: Wanapewa kipaumbele kwenye ajira, maofisini asilimia kubwa ya vyeo vizito ni zao la UDSM

Elimu ipo chuo chochote, uzito upo UDSM: Wanapewa kipaumbele kwenye ajira, maofisini asilimia kubwa ya vyeo vizito ni zao la UDSM

Hiyo mifano yako ungeweka na details za hao watu wamemaliza hapo Udsm mwaka gani??

Kwa sekeseke la ajira lilivyo kwa sasa ni haijalishi umesoma chuo gani mkuu.
Hicho ni chuo kongwe hapa Tz, sasa mawaziri ulitaka wasome wapi miaka ya 90??

Yaani ni sawa na useme zile shule kongwe za sekondari kama Bwiru, Songea, Ilboru, Tabora boys etc zimetoa wasomi wengi, zimepitiwa na viongozi wengi sijui mawaziri. Utakua unakosea maana miaka hiyo hakukua na shule nyingi.
 
Nenda PSRS utumishi watakupa majibu....ajira sasa hv sio umesoma wapi..ni unajua nn..pambana ujue
Kipindi cha Magu Utumishi walipewa jukumu la kusimamia ajira ila kwa sasa ajira nyingi ni mashirika / taasisi zinajisimamia.

Wakurugenzi wengi waliosoma UDSM ndio wanasimamia ajira, Unategemea nini ??

Ni maza mwenyewe ndie alieruhusu wakurugenzi wanze upya huu mfumo ambao Magufuli aliutokomeza kwa kutumia idara ya Utumishi isimamie ajira.
 
Vyuo vya Bongo havina resources na strong departments za research and development .
Badala ya kuviwezesha ili kusaidia maendeleo ya tafiti ,Science na technology , mnakaa kujadili utopolo wa udsm kuwa bora .
Yaani takataka kama udsm ina tofauti gani na vyuo utopolo vilivyojazana humu Bongo ?
Kuna lipi la maana au reseach au project ipi ya maana ambayo imeleta solution kubwa kwa jamii udsm wamefanya ?
Ndio maana hata ranking viko chini sana ,including utopolo udsm , vyuo vya Bongo ni rubbish kabisa .
 
Kachukue fomu ya ubunge ukalalamike bungeni
watu wanalamba ajira, wanalipwa mishahara na posho kwa kodi yako, wanakula tenda kwa kodi yako, maisha yanaendelea..
 
Hao uliowataja hapo ndugu mleta mada, wote familia wanazotoka si za walalahoi au za kawaida kama za watanzania wengine wengi.

Anza kupekua bibliography zao utapata majibu. Connection zilianziaga mbali sana! Pia wacha kudanganya uma. Vijana waliohitimu elimu ya ngazi ya juu chuo kikuu cha Dar es Salaam ambao hawana ajira bado ni kubwa mno!

Mwisho kabisa kama ni mfuatiliaji siku hizi huwezi kuwa kiongozi mkubwa wa taasisi fulani kama huna exposure.

Kama unabisha wanaoelewa hili wataunga mkono mchango wangu bila shaka.
 
Hicho Chuo ni kikongwe kwa hapa Tz, na hao watu uliowataja hapo juu wengi wao walisoma kipindi Vyuo hapa Tz ni vichache na preference moja wapo ni kusoma UD.

tofaut na sasa hivi vyuo ni vingi sana.... watu wapo scattered..

Hiyo Era ya hao uliowataja ikishapita I think after 15 yrs mbele BATCH yao inakuwa haipo.. au inapungua.

Utakutana na mixer humo ktk vitengo.
 
Kipindi cha Magu Utumishi walipewa jukumu la kusimamia ajira ila kwa sasa ajira nyingi ni mashirika / taasisi zinajisimamia.

Wakurugenzi wengi waliosoma UDSM ndio wanasimamia ajira, Unategemea nini ??

Ni maza mwenyewe ndie alieruhusu wakurugenzi wanze upya huu mfumo ambao Magufuli aliutokomeza kwa kutumia idara ya Utumishi isimamie ajira.
Bado unaandika hisia sio uhalisia...nadhan bado upo chuo, subiri umalize uje mtaami
 
Back
Top Bottom