Elimu kwa Umma: Maswali na Majibu kuhusu Safari za Ndege na Changamoto zake

Elimu kwa Umma: Maswali na Majibu kuhusu Safari za Ndege na Changamoto zake

Asante kwa kuuliza mkuu.

Tunahusika na tiketi, visa processing, accommodation, usafiri kutoka Airport (cab) na kwa wasafiri wanaokuja nchini tuna baadhi ya maeneo tunaweza kuwaandalia kwenda kutalii kama watahitaji.

Kwahiyo jibu ni ndiyo, tunatoa huduma ya kumsaidia abiria kupata visa ya nchi yoyote.
Shukrani kwa majibu mazuri.
 
Naulizia utaratibu wa kusafirisha maiti kwenye ndege

Swali zuri.

Kusafirisha maiti unaweza kukodi ndege binafsi au ya abiria na maiti ikasafiri kama mzigo. Mwili wa mtu ukishafariki, unahesabiwa kama mzigo mwingine tu (Cargo).

Muhimu unatakiwa kuwa na nyaraka zifuatazo:

1. Embalming Certificate: Hii ni hati ya uthibitisho kuonyesha kuwa mwili wa marehemu umekuwa treated na madawa (chemikali) ili uweze kuua wadudu, kutoa harufu na kuepuka umwagikaji wa majimaji "fluid". Hapa inajumuisha kumwagia manukato marehemu, kumvisha begi la plastiki kuondoa uwezekano wa damu na maji kumwagika kwenye ndege.

2. Death Certificate: Hii ni nyaraka mojawapo inayotakiwa. Bila shaka inajulikana kwanini hii inahitajika na wapi inapatikana.

3. Affidavit: Hii husainiwa na Daktari aliyethibitisha kuwa mgonjwa/mtu amefariki kweli.

4. Handling Fee (takribani laki 2): Hii hutolewa kwa ile kampuni itakayoishughulikia maiti inapofika eneo la mizigo kama vile kuipima kilo na hatimaye kuikokota mpaka kwenye ndege.

5: Malipo ya maiti kwa kilo: Gharama za usafirishaji huwa inategemea na uzito wa maiti. Kadri maiti inavyokuwa na mwili mzito ukijumlisha na uzito wa jeneza, ndivyo gharama nayo inaongezeka. Gharama iliyozoeleka ni elfu 7 kwa kilo. Kuna uwezekano imepanda au imeshuka kidogo.

Ni matumaini yetu umepata mwanga hata kama kuna vigezo vinaweza kuwa vimebadilika lakini huu ndio utaratibu unaotumika nchini Tanzania.

Muhimu: Majibu haya yameongezewa kutoka kwa maelezo ya mkuu barafu yaliyowahi kuchapishwa hapa jukwaani.

Asante.
 
Kama tujuavyo binadamu hatufanani maumbile, je ikitokea mtu ana umbile linaloweza kuchukua nafasi zaidi ya iliyowekwa kwa abiria mmoja je ni utaratibu gani hufanyika?
 
Karibu mkuu.

Mchanganuo wa gharama hutokana na shirika la ndege ambayo abiria huchagua kusafiria na viwango vya bei za tiketi kwa safari husika.

Tunaweza kukuangalizia gharama kwa makadirio ya muda huu kati ya mashirika mawili, kisha utachagua inayoendana na bajeti yako.

Tutakutumia gharama hizo PM muda si mrefu kutoka sasa.

Asante.

UPDATE: Tumeangalia gharama za safari ya Dubai kwa tarehe husika.

Gharama (Go & Return) ni:
1. Ndege ya Shirika la Fly Dubai (USD 710)
2. Ndege ya Shirika la Etihad (USD 590).

Gharama hizi ni kama utakata tiketi kipindi hiki mapema. Zaidi ya hapo gharama zinaweza kupanda au kushuka, mara nyingi gharama za tiketi hupanda kadri siku ya safari inavyokaribia.

Tunajaribu kufuatilia na gharama za mashirika mengine pia.

Asante.
 
Kama tujuavyo binadamu hatufanani maumbile, je ikitokea mtu ana umbile linaloweza kuchukua nafasi zaidi ya iliyowekwa kwa abiria mmoja je ni utaratibu gani hufanyika?

Asante kwa swali zuri.

Swali lako ni mjadala mkubwa ambao umekuwa ukiibuka mara kwa mara duniani, huku mashirika na taasisi za haki za binadamu zikipigia kelele "unyanyapaa" unaofanyika kwa watu wenye maumbile makubwa katika huduma mbalimbali, zikiwemo za usafiri.

Kujibu swali lako: Sera za mashirika ya ndege kuhusu maumbile ya abiria zinatofautiana. Hata hivyo, ni kawaida kwa mashirika mengi kutoza Abiria kulipia siti ya ziada, ikiwa hatoshei katika siti yake na mkanda.

Asante.
 
Kweli huu ni mjadala.. ikiwa kuna huduma za kubook safari online hiyo tozo ya ziada hutokea wakati gani? Na je mtu anaweza kuahirishiwa safari yake kwa sababu za umbile lake?

naomba kuuliza kwenye gharama za do and return utaratibu wake unakuwaje ,nikimaanisha kwamba je ni siku ngapi tiketi yangu inakuwa invalid
au kuweka vizurj hio ticket ni kwambani ndege hio hio itakaporudi ndio natakiwa kurudi nayo siku inayofuata au vipi?

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Kweli huu ni mjadala.. ikiwa kuna huduma za kubook safari online hiyo tozo ya ziada hutokea wakati gani? Na je mtu anaweza kuahirishiwa safari yake kwa sababu za umbile lake?

Mashirika mengi ya ndege yanapendekeza kwamba ikiwa unajiona una mwili mkubwa sana kuliko siti yako, unapaswa kulipia na siti ya pili wakati unafanya booking. Yapo Mashirika ya ndege hutoa punguzo ya siti ya nyongeza au kurudisha gharama ikiwa ndege haijajaa, lakini katika "case" nyingi abiria wenye miili mikubwa hulazimika kulipa mara mbili ya bei.

Sasa ukikata tiketi ya mtu mmoja halafu ukaenda kwenye siti ukaona hutoshei, unaweza kukatishiwa safari na usirudishiwe pesa yako kama tu walitoa tahadhari mapema.

Asante.
 
Hongera mkuu, unajibu maswali vizuri sana na kitaalamu kuliko wenzako wa kwenye thread za kule juu zenye rangi tofauti. Kama ni maksi wewe ungepata 99.8, TANESCO angepata 90, halafu NMB na Vodacom wangegawana maksi 15 yaani F au pointi za kushuka daraja.
 
Asante sana kwa majibu. Kwa nyongeza tuu nilichogundua katika usafiri wa angani.. vigezo na masharti ni vitu muhimu sana kuvijua kabla yakuanza mipango ya safari husika kuepuka changamoto zinazoweza kuepukwa.
 
naomba kuuliza kwenye gharama za do and return utaratibu wake unakuwaje ,nikimaanisha kwamba je ni siku ngapi tiketi yangu inakuwa invalid
au kuweka vizurj hio ticket ni kwambani ndege hio hio itakaporudi ndio natakiwa kurudi nayo siku inayofuata au vipi?

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app

Asante kwa kuuliza mkuu singanojr

Tiketi huwa zina muda wake wa safari ambao unakuwa umejaza. Ikifika tarehe ya safari unatakiwa kwenda kuitumia, usipoitumia na muda ukapita inakuwa invalid. Lakini endapo utatoa taarifa mapema kwamba hutasafiri tarehe husika, basi kuna uwezekano ukabadilishiwa ila utatakiwa kulipa ada fulani.

Kwa kuongezea, tickets hutofautiana katika kuisha kwa muda wake (expiry). Kuna zinazodumu kwa mwezi, miezi mitatu hadi mwaka.

Na haya yote ndio yanaonesha umuhimu wa kutumia travel agency. Agent anakusaidia kusoma na kuzielewa taratibu za ticket kwa shirika la ndege husika na sera zake. Travel Agent anasaidia pia kukushauri, kukukumbusha, kukujazia fomu na mambo yote yanayohusu safari yako hadi ikamilike kuepuka usumbufu na hasara.

Asante.
 
Hongera mkuu, unajibu maswali vizuri sana na kitaalamu kuliko wenzako wa kwenye thread za kule juu zenye rangi tofauti. Kama ni maksi wewe ungepata 99.8, TANESCO angepata 90, halafu NMB na Vodacom wangegawana maksi 15 yaani F au pointi za kushuka daraja.

Shukrani sana mkuu Chen Hu
 
Asante kwa kuuliza mkuu singanojr

Tiketi huwa zina muda wake wa safari ambao unakuwa umejaza. Ikifika tarehe ya safari unatakiwa kwenda kuitumia, usipoitumia na muda ukapita inakuwa invalid. Lakini endapo utatoa taarifa mapema kwamba hutasafiri tarehe husika, basi kuna uwezekano ukabadilishiwa ila utatakiwa kulipa ada fulani.

Kwa kuongezea, tickets hutofautiana katika kuisha kwa muda wake (expiry). Kuna zinazodumu kwa mwezi, miezi mitatu hadi mwaka.

Na haya yote ndio yanaonesha umuhimu wa kutumia travel agency. Agent anakusaidia kusoma na kuzielewa taratibu za ticket kwa shirika la ndege husika na sera zake. Travel Agent anasaidia pia kukushauri, kukukumbusha, kukujazia fomu na mambo yote yanayohusu safari yako hadi ikamilike kuepuka usumbufu na hasara.

Asante.
Swali la nyongeza katika hili jibu.

Ni muda gani(time limit) unaoruhusiwa kukata tiketi kabla ya siku ya safari?

Yaani 1 week, Month or year to travel day?
 
Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa menejimenti na uongozi wa JamiiForums kwa kuuthibitisha ukurasa wetu.

Bonheur Travels Tanzania tupo rasmi sasa (verified) hapa jamvini.

Shukrani kwenu nyote pia mnaoendelea kutuuliza maswali na kushiriki nasi kwenye uzi huu kwa maslahi ya umma.

Tunaendelea kupokea maswali, maoni na mengine yote yahusuyo safari za ndege.
 
Back
Top Bottom