Bonheur Travels Tanzania
JF-Expert Member
- Dec 29, 2020
- 252
- 499
- Thread starter
- #141
Swali la nyongeza katika hili jibu.
Ni muda gani(time limit) unaoruhusiwa kukata tiketi kabla ya siku ya safari?
Yaani 1 week, Month or year to travel day?
Swali zuri mkuu Mwifwa,
Inategemea na umbali wa safari na utaratibu wa shirika husika. Mara nyingi kwa safari za ndani, unaweza kukata ticket hata masaa machache kabla ya safari. Kwa safari za nje pia inawezekana hata masaa 3 kabla, muhimu uwe tayari tu.
Ni muhimu kuzingatia kwamba gharama za ticket hupanda zaidi kadri unavyokata karibu na muda wa safari, hivyo inashauriwa kukata wiki au miezi michache kabla kama safari sio ya dharura. Japo inatokea mara nyingine kupata ticket kwa bei rahisi ukikata muda mchache kabla ya safari, ila ni nadra sana.
Asante.