Elimu kwa Umma: Maswali na Majibu kuhusu Safari za Ndege na Changamoto zake

Elimu kwa Umma: Maswali na Majibu kuhusu Safari za Ndege na Changamoto zake

Ninapokata ticket kupitia nyinyi huwa kuna gharama natakiwa kuwalipa?

Hapana mkuu. Gharama unayolipa kwetu ni ya tiketi pekee. Kazi yetu ni kukusaidia kupata usafiri wa uhakika kwa haraka zaidi na kuhakikisha safari yako inakamilika salama.

Isitoshe, sisi tuna mahusiano ya kibiashara na mashirika kadha wa kadha ya ndege, hivyo tunaweza kukusaidia kupata tiketi zenye gharama rafiki kulingana na bajeti yako.

Kimsingi, tunakusaidia kuokoa muda na wakati mwingine kukuepusha kulipa gharama kubwa endapo utaamua kukata moja kwa moja.
 
1. Ukisafiri na mtoto ndani ya ndege unaweza kumpakata ama ni lazima ulipie ticket yake.

2. Traveling insurance gharama yake zikoje

1. Sio lazima, ila kuna umri wa mtoto lazima umlipie siti yake kulingana na utaratibu wa shirika la ndege husika.

2. Gharama zinatofautiana baina ya wakala na wakala. Kwetu tuna package maalum kwa bei rafiki, kama unahitaji unaweza kuwasiliana nasi moja kwa moja.

Karibu.
 
Kwahiyo Mtoto wa kupakatwa anapanda bure?
 
Mala nyingi ndege hulipuka na kuua abiria pale tu inapopata hitilafu huko juu,.. sijawahi kusikia abiria wameruka Kwa parachuti au miamvuli unaweza kututoa hofu hapo?

Ripoti mbalimbali zinaonesha wapo watu huokoa maisha yao kwa kutumia parachutes. Hata hivyo, ni ukweli usiopingika kuwa ajali nyingi za ndege huwa ni milipuko na nyingine hutokea kwa haraka sana hivyo abiria hupanic na kukosa muda wa kujiandaa kukabiliana na hatari, hatimae kupelekea vifo.

Asante.
 
Kwasasa Sina swali, lakini naomba tu nikupongezeni kwamba ninyi ni kati ya watoa huduma wachache sana wenye uwezo wa kujibu maswali kwa ueledi na pasipo kukasirika hapa Jf....
Hongereni sana na nina wapongeza kwa hilo.

Shukrani sana kwa pongezi mkuu Ushimen. Lengo letu ni kuhakikisha tunashirikishana uelewa wa pamoja.

Karibu kwa maswali au maoni muda wowote.
 
Napenda kuuliza air tz dreamliner engine yake ina ukubwa gan
Je ina cylinder gap
Na Je ni type gan stock engine

Asante kwa maswali mkuu.

Kwa bahati mbaya, hatuna taarifa za kiufundi za ndege hiyo. Tutajaribu kufuatilia au unaweza kuangalia kwenye tovuti rasmi za kampuni zinazotengeneza ndege husika au ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kama zimewekwa.

Asante.
 
Naomba kujua kiwango cha mwisho cha pesa kusafiri nacho kwenye ndege.
 
Naomba kujua kiwango cha mwisho cha pesa kusafiri nacho kwenye ndege

Swali zuri.

Kiwango cha juu cha pesa unachoweza kusafiri nacho inategemea nchi na nchi.

Kwa Marekani, unaruhusiwa kusafiri na kiwango chochote kile cha pesa kwa sharti la kutoa taarifa kwa mamlaka zinazohusika.

Kwa Tanzania, ukiwa unasafiri na kiasi cha pesa kuanzia kuanzia Dola 10, 000/= (Shilingi Milioni 23) utatakiwa utoe taarifa TRA.

Asante.
 
Hati ya kusafiria( passport) kwanini lazima uwe nayo hata kwa safari za ndani ya nchi?
Ni takwa la kisheria na utaratibu rasmi uliowekwa katika kufanya safari za ndege. Ndio maana ikaitwa hati ya kusafiria, yaani ni nyaraka ambayo lazima uwe nayo ili uweze kufanya safari za ndani na nje ya nchi.

Pia, ni moja ya nyaraka muhimu za utambulisho wa uraia na husaidia wakati wa dharura au upelelezi kwa kufuatilia taarifa za safari za anayemiliki passport husika.

Asante.
 
Hapana mkuu. Gharama unayolipa kwetu ni ya tiketi pekee. Kazi yetu ni kukusaidia kupata usafiri wa uhakika kwa haraka zaidi na kuhakikisha safari yako inakamilika salama.

Isitoshe, sisi tuna mahusiano ya kibiashara na mashirika kadha wa kadha ya ndege, hivyo tunaweza kukusaidia kupata tiketi zenye gharama rafiki kulingana na bajeti yako.

Kimsingi, tunakusaidia kuokoa muda na wakati mwingine kukuepusha kulipa gharama kubwa endapo utaamua kukata moja kwa moja.
Sawa
 
Ni kweli kwenye safari ndefu kuna wakati marubani huwa wanauchapa usingizi, ndege ikabaki inajiongoza peke yake
 
Uzi murua kwa sisi tusio na uzoefu na safari za ndege. Hope one day nitawacheki nikwee pipa hata kwenda Chato.
 
Hili ni suala la kiufundi na kitaalamu.

Hata hivyo, zipo dondoo za usalama (safety tips) ambazo hutolewa kwa abiria mapema ili inapotokea hitilafu basi waweze kujihami wakati hatua nyingine za usalama zikichukuliwa.

Njia za haraka zinazofahamika inapotokea hitilafu angani (japo inategemea na level) ni pamoja na;

.- Ndege kutua kwa dharura katika eneo lolote elekezi

- Kutoa taarifa kwa vikosi vya uokozi ardhini ili kupokea abiria kutokea angani (evacuation)

- Abiria kutakiwa kuvaa jackets au miamvuli aina ya parachutes

- Mengineyo.

Asante.
Mkuu abiria kuvaa parachutes?? [emoji848][emoji848][emoji848]
Nimepanda ndege nyingi ila sijawahi ona maelekezo ya kuvaa hizo parachutes, pia utatoka vp na hilo parachute lako kwenye ndege ya abiria?? Na mlango utafunguliwa vp? Please maelezo kidgo hapa, labda ndge ya kijeshi.
 
Back
Top Bottom