View attachment 2812618
Achana na hizi shule za haoa bongo zilizojipachika majina ya international kimagumashi,
Shule international haiwezi kufuata mtaala wa Necta.
International school zinazofuata mitaala ya kimataifa kama cambridge, Mwanafunzi anaweza kuhama Marekani leo hii na kesho akifika Tanzanja anaendelea na masomo kama kawaida.
Ni maalum zaidi kwa watoto wa mabalozi na watoto wa wafanyakazi wa mashirika ya kimataifa wanaohama hama nchi, ada za watoto wa mabalozi zinalipiwa na serikali zao, wale wa mashirika ada zinalipwa na mashirika yao.
Ada ya hizi shule ni ndefu sana endapo ukitaka kumsomesha mtoto wako kwa pesa zako mwenyewe, hapa waliozoeleka kusomesha ni wafanyabiashara na wanasiasa wenye pesa zao na exposure.
Ada ya mtoto wa chekechea pekee ni milioni 10 na nusu (10,500,000),
Faida za kusomesha shule hizi:
1. Mtoto anapata exposure ya kuishi na watu wa mataifa mbali mbali.
2.Mtoto anafundishwa kutema yai original la uingereza na marekani, asikudanganye mtu hizi shule za english medium tumezisoma ila tulichoambulia ni kuweza kuandika na kusoma kiingereza cha kawaida, kwenye kuzungumza tunaongea chenye lafudhi ya kibantu, mzungu akiongea wengi hawaelewi.
3. Mtoto ana chance kubwa ya kuja kusoma vyuo bora duniani kama Havard, Oxford, Cambridge, n.k.
4. kusafiri nje ya nchi kwajili ya trips.
5. watoto wanapata connections za watoto wenzao wazito, huwa zinawasaidoa sana hasa wakianza maisha ya kujitegemea, sehemu ambayo mtu unaweza kuchukua mwaka kuingia wao ni suala la kupiga simu tu.
6. Ajira zenye maokoto marefu, kwa wale wataoamua kufanya ajira mara nyingi hufanya kazi mashirika ya kimataifa kama UN, AU, EAC, Google, Microsoft, n.k. exposure wanayopata na connections walizonazo zinawabeba.