Elimu ni ufunguo wa Maisha, Diamond anamsomesha mtoto wake Braeburn International school, chekechea ada milioni 20

Elimu ni ufunguo wa Maisha, Diamond anamsomesha mtoto wake Braeburn International school, chekechea ada milioni 20

Na huu ndio ukweli usiopingika wa maisha: Usiwasomeshe watoto wako kuwa matajiri, wafundishe kumjua Mungu,Yeye atawapa utajiri. Kwa njia hiyo watakuwa na furaha ya kweli. Kwa njia hiyo pia watakapokuwa wakubwa watajua thamani ya vitu na sio bei.
Hayo ni mawazo ya kimasikini

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
View attachment 2812618
View attachment 2812721
Achana na hizi shule za haoa bongo zilizojipachika majina ya international kimagumashi, Shule international haiwezi kufuata mtaala wa Necta.

International school zinazofuata mitaala ya kimataifa kama cambridge, Mwanafunzi anaweza kuhama Marekani leo hii na kesho akifika Tanzanja anaendelea na masomo ya jana kama kawaida.

Ni maalum zaidi kwa watoto wa mabalozi na watoto wa wafanyakazi wa mashirika ya kimataifa wanaohama hama nchi, ada za watoto wa mabalozi zinalipiwa na serikali zao, wale wa mashirika ada zinalipwa na mashirika yao.

Ada ya hizi shule ni ndefu sana endapo ukitaka kumsomesha mtoto wako kwa pesa zako mwenyewe, hapa waliozoeleka kusomesha ni wafanyabiashara na wanasiasa wenye pesa zao na exposure (unaweza kuwa na pesa ila kama huna exposure ama kuzungukwa na watu wenye exposure utaishia kusomesha shule za Necta)

Ada ya mwaka kwa chekechea ni dola 8,395, kwa pesa za kitanzania ukizidisha kwa shilingi 2,500 ni takribani shilingi milioni 21.

Faida za kusomesha shule za international:

  • Mtoto anapata exposure ya kuishi na watu wa mataifa mbali mbali, shuleni kuna waarabu, wahindi, wachina, wabrazil, wanaijeria, n.k.
  • Darasa moja halizidi wanafunzi 20
  • Mtoto anafundishwa kuongea lugha za kimataifa kama kiingereza, kifaransa na spanish kwa ufasaha, kama ni yai wanatema lile original (hata Wema Sepetu pamoja na utukutu wake yai analicharaza), asikudanganye mtu hizi shule za english medium tumezisoma ila tulichoambulia ni kuweza kuandika na kusoma kiingereza kwa level ya kawaida sana, kwenye kuzungumza tunapata sana taabu kwa hizi lafudhi za kibantu (ze boi, ze geli, do zis) na ndio maana mzungu wa Marekani au Uingereza akiongea wengi hawaelewi inakuwa ni kuotea tu baadhi ya maneno
  • Mtoto ana chance kubwa ya kuja kusoma vyuo bora duniani kama Havard, Oxford, Cambridge, n.k.
  • kusafiri nje ya nchi kwajili ya trips.
  • watoto wanapata connections za watoto wenzao wazito, huwa zinawasaidoa sana hasa wakianza maisha ya kujitegemea, sehemu ambayo mtu unaweza kuchukua mwaka kuingia wao ni suala la kupiga simu tu.
  • Kibiashara hizi shule ni nzuri kuwaandaa watoto kuja kusimamia biashara za familia ama kuanzisha zao, Kama baba ni tajiri wa mashamba ya maparachi anayouza kwa wakenya basi mtoto kwa connections na exposure atazopata huko anaweza kupata masoko ya ulaya moja kwa moja, kwenye kuanzisha biashara nako tumewaona watu kama kina Benjamin Fernandez wamekataa mishahara ya milioni 40 kaanza biashra zake kwa kudhaminiwa mitaji, sio kirahisi rahisi tu kupata wadhamini inabidi uwe na connections.
  • Ajira zenye maokoto marefu, kwa wale wataoamua kufanya ajira mara nyingi hufanya kazi mashirika ya kimataifa kama UN, AU, EAC, Google, Microsoft, n.k. exposure wanayopata na connections walizonazo zinawabeba.
Kila mtu hujikuna anapojipata
 
Na huu ndio ukweli usiopingika wa maisha: Usiwasomeshe watoto wako kuwa matajiri, wafundishe kumjua Mungu,Yeye atawapa utajiri. Kwa njia hiyo watakuwa na furaha ya kweli. Kwa njia hiyo pia watakapokuwa wakubwa watajua thamani ya vitu na sio bei.
Mawazo ya kimasikini haya yanayohubiriwa na wachungaji wanaokusanya sadaka zenu kununulia V8 huku nyie waumini mpo hoi.

Maarifa ni muhimu na Mungu nae ni Muhimu
 
Mil 20 kwa Mwaka si pesa ndefu kwa huyo Jamaa, ila kwa Mimi kapuku.. aisee huo ni mkopo wa miaka 8 nakatwa kila mwezi mpk hela ya watu irudi..🤣

Diamond mbali sana

MC GARAB tu anaipata hiyo hela mwezi mmoja tu.

Mpuuzi kama Mwijaku anaipata hiyo hela ndani ya miezi mitatu tu.

Hiyo hela ni ndogo sana ukiwa unafanya kazi na watu wengi ama taasisi nyingi tofauti

Shida wengi tumejifunga na ajira zetu tunategemea mshahara wa mwajiri mmoja
 
Uzi na kilichozungumzwa ni vitu viwili tofauti.

Unapoizungumzia "Elimu ni ufunguo wa maisha" sio lazima iwe ya International school... huenda Point yako ulitaka kutuhabarisha kwamba mtoto wa bwana Diamond anasoma Braeburn, sasa sijui tukuchinjie mbuzi au tukupigie makofi. Unajua mwenyewe

Hatuna Rais, Makamo, PM wala kigogo yoyote mwinginewe aliyesoma huko... na wanaishi ndani ya true definition of "Elimu ni ufunguo wa maisha"

Hayo mengine yote ni jeuri ya Pesa tu! Ila hatutakuja kupata rais alisoma IST na huko Braeburn. Kama unabisha subiri.
Mkuu huko tuendako watoto wa hawa viongozi wa sasa ndo wanaenda kuwa viongozi wa hili taifa na kwa taarifa yako ni kuwa sio upinzani wala CCM ni kwamba vigogo wote wanasomesha watoto hizi shule kali. Kama huamini fuatilia UVCCM ya sasa viongozi wake ni kina nani... tayari wa kishua Jokate ni boss UWT. Mbowe nae anamrithisha chama mwanae aitwae James ambaye kasoma Nje. Acha hizo fikra zilizopitwa na wakati
 
Mkuu huko tuendako watoto wa hawa viongozi wa sasa ndo wanaenda kuwa viongozi wa hili taifa na kwa taarifa yako ni kuwa sio upinzani wala CCM ni kwamba vigogo wote wanasomesha watoto hizi shule kali. Kama huamini fuatilia UVCCM ya sasa viongozi wake ni kina nani... tayari wa kishua Jokate ni boss UWT. Mbowe nae anamrithisha chama mwanae aitwae James ambaye kasoma Nje. Acha hizo fikra zilizopitwa na wakati
Sio kwamba Fikra zimepitwa na wakati... hilo la vigogo kusomesha shule kali watoto wao nalijua pia.

Hunielewi na huwezi kunielewa na hautanielewa. Nchi kuongozwa na kiongozi wa aina fulani kunataka protokali mzee ambazo katu hutakaa ukazijua wewe mwananchi wa kawaida.

Tuombeane uhai uone kama nchi itakujwa kuongozwa na waliosoma IST na Braeburn... unafkiri sisi ni mazwazwa sana? 😀😀😀

Wataishia hukohuko ilipopataja, kuwa Rais kuna nidhamu zake bwamdogo. Huwezi katu kuyajua hayo mpaka uwe kwenye game
 
Back
Top Bottom