Elimu ni ufunguo wa Maisha, Diamond anamsomesha mtoto wake Braeburn International school, chekechea ada milioni 20

Elimu ni ufunguo wa Maisha, Diamond anamsomesha mtoto wake Braeburn International school, chekechea ada milioni 20

Unapaswa ufahamu kuwa Feza hiyohiyo unayoijua wewe Kuna upande wa pili wanafata mtaala wa Cambridge na ada zao huwa ndefu pia.
Wazazi pia vizuri kuzijua hizo shule vizuri zingineni huitwa International School lakini huwa na matokeo mabaya sana mitihani ya. Kimataifa ya Cambridge

Shule nzuri mfano zinazotumia mfumo wa NECTA huwa tunazijua kwa kuangalia matokeo ya mitihani ya NECTA

Ni vizuri pia mzazi kujiridhisha na matokeo ya mitihani ya Cambridge ya Shule husika kabla kujitosa kichwa kichwa kupeleka mtoto

Uzuri shule za kimataifa ziko nchi nyingi pesa akiwa nayo aweza peleka iliyo nzuri yenye matokeo mazuri mitihani ya Cambridge popote Africa hata nje

Kuna wazazi hilo hata huwa hawaangalii akiona ina kibao International School anaishia hapo

Vizuri kucheki
 
Sema kweliii.
Yaani, we acha tu...😂
Hata kama ukipata viza ya kusoma UK, unaweza kuleta familia yako na watasoma bure
Wahindi wanapambana hasa kwenda Europe kwa dhumuni moja tu, kusomesha watoto wao.
Wafanyakazi wa balozi za bongo, huwa wanasomba mpaka vitukuu, lakini wakitumbuliwa ndio mwisho wake🤣
 
Unapaswa ufahamu kuwa Feza hiyohiyo unayoijua wewe Kuna upande wa pili wanafata mtaala wa Cambridge na ada zao huwa ndefu pia.
Ukisoma mtaala wa Cambridge yaani ndio unakuwa so powerful ama just Ile human ego distinguished in classic.yaani mfano mathematics amaa physics Ni mbali na hii ya necta,hii mie nimeuliza nielezewe. Mie Kuna watu wamemaliza hapa necta wakaenda Oxford , Cambridge,Yale, Massachusetts,havard ,mit, hapo huwa inakuwaje wandugu
 
View attachment 2812618
View attachment 2812721
Achana na hizi shule za hapa bongo zilizojipachika majina ya international kimagumashi, Shule international haiwezi kufuata mtaala wa Necta hata kama ni Feza boys.

International school zinazofuata mitaala ya kimataifa kama cambridge, Mwanafunzi anaweza kuhama Marekani leo hii na kesho akifika Tanzanja anaendelea na masomo ya jana kama kawaida.

Ni maalum zaidi kwa watoto wa mabalozi na watoto wa wafanyakazi wa mashirika ya kimataifa wanaohama hama nchi, ada za watoto wa mabalozi zinalipiwa na serikali zao, wale wa mashirika ada zinalipwa na mashirika yao.

Ada ya hizi shule ni ndefu sana endapo ukitaka kumsomesha mtoto wako kwa pesa zako mwenyewe, hapa waliozoeleka kusomesha ni wafanyabiashara na wanasiasa wenye pesa zao na exposure (unaweza kuwa na pesa ila kama huna exposure ama kuzungukwa na watu wenye exposure utaishia kusomesha shule za Necta)

International schools ni levels nyingine, hata marekani wana shule zao za serikali na private kama huku kwetu lakini hazifikii international.

Ada ya mwaka kwa chekechea ni dola 8,395, kwa pesa za kitanzania ukizidisha kwa shilingi 2,500 ni takribani shilingi milioni 21.

Faida za kusomesha shule za international:

  • Mtoto anapata exposure ya kuishi na watu wa mataifa mbali mbali, shuleni kuna waarabu, wahindi, wachina, wabrazil, wanaijeria, n.k.
  • Darasa moja halizidi wanafunzi 20
  • Mtoto anafundishwa kuongea lugha za kimataifa kama kiingereza, kifaransa na spanish kwa ufasaha, kama ni yai wanatema lile original (hata Wema Sepetu pamoja na utukutu wake yai analicharaza), asikudanganye mtu hizi shule za english medium tumezisoma ila tulichoambulia ni kuweza kuandika na kusoma kiingereza kwa level ya kawaida sana, kwenye kuzungumza tunapata sana taabu kwa hizi lafudhi za kibantu (ze boi, ze geli, do zis) na ndio maana mzungu wa Marekani au Uingereza akiongea wengi hawaelewi inakuwa ni kuotea tu baadhi ya maneno
  • Mtoto ana chance kubwa ya kuja kusoma vyuo bora duniani kama Havard, Oxford, Cambridge, n.k.
  • kusafiri nje ya nchi kwajili ya trips.
  • watoto wanapata connections za watoto wenzao wazito, huwa zinawasaidoa sana hasa wakianza maisha ya kujitegemea, sehemu ambayo mtu unaweza kuchukua mwaka kuingia wao ni suala la kupiga simu tu.
  • Mtoto anapata moto mkali vibaya mno akisoma hizo shule hawezi kuridhika anavyoitwa wa kishua na rafiki zake wa kibongo, anaingia rasmi kwenye tabaka la malengo ya kuingiza walau milioni 20 kwa mwezi ili aweze kuja kuendana na wenzake, sio kuwaza mishahara ya milioni 3
  • Kibiashara ni shule zinazoweza kukuza biashra za familia, Kama baba ni tajiri wa mashamba ya maparachi anayouza kwa wakenya basi mtoto kwa connections na exposure anaweza kupata masoko ya ulaya moja kwa moja na hata kuanzisha kiwanda cha bidhaa, kusoma hizi shule ni sawa na mtu alieishi sana Dar anaenda kijijini anaweza kuona fursa kibao.
  • kwenye kuanzisha biashara kwa wale wasio na biashara za familia zinawasadia, wana uwezekano mkubwa wa kupata wadhamini / grants hasa katika nchi zetu hizi masikini, wana connections za wenzao wa mashirika ya kimataifa na wana exposure, Mfano ni Benjamin Fenandes app yake ni ya kawaida tu lakini imejipatia misaada ya pesa ndefu sana, na hivi sasa kaihamishia huko Kenya, connections na kuwa na exposure ya kuishi nchi zingine kunasaidia.
  • Ajira zenye maokoto marefu, kwa wale wataoamua kufanya ajira mara nyingi hufanya kazi mashirika ya kimataifa kama UN, AU, EAC, Google, Microsoft, n.k. exposure wanayopata, kuzicharaza lugha za kimataifa na connections walizonazo zinawabeba.
Uzi wote huu umeandika kisa mtoto wa Chibu au kuna lingine??

Kazi ipo.
 
Education is better than money

v/s

Money is better than education


Ukiwa shuleni unapangwa
v/s
ukiwa mtaani uhalisia unajulikana

Mwambieni mtoto wa Mo apambane abadilishe ile hali ya maisha pale kwao ni dhiki kubwa ile [emoji16]
 
Sio kwamba Fikra zimepitwa na wakati... hilo la vigogo kusomesha shule kali watoto wao nalijua pia.

Hunielewi na huwezi kunielewa na hautanielewa. Nchi kuongozwa na kiongozi wa aina fulani kunataka protokali mzee ambazo katu hutakaa ukazijua wewe mwananchi wa kawaida.

Tuombeane uhai uone kama nchi itakujwa kuongozwa na waliosoma IST na Braeburn... unafkiri sisi ni mazwazwa sana? 😀😀😀

Wataishia hukohuko ilipopataja, kuwa Rais kuna nidhamu zake bwamdogo. Huwezi katu kuyajua hayo mpaka uwe kwenye game
Na kwa hiyo katiba ni uongo kabisa inavyoelekeza kuwa mtu kugombea urais anatakiwa kuwa na miaka 40 na pia awe na akili timamu.. kumbe kuna masharti mengine yapo😄
 
Kila mtoto anaesoma Braeburn ni mtoto wa kishua haswa pengine huyo Diamond ndo miongoni mwa maskini hapo kwahiyo kila mtoto hapo ni hela lakini jiulize kwanini hawaendi kuteka
Suala la ulinzi limezingatiwa labda akatekwe akiwa mikononi kwa babaake
Sana,
Hapo ni wakishua tu,

Hivi kwanini international school nyingi zipo Arusha ? ,Niliwai angalia list zao ni Arusha na Dar ya pili ,
Sijajua kwanini nyingi ziko Arusha,
 
Mawazo ya kimasikini haya yanayohubiriwa na wachungaji wanaotembeea ma V8 huku waumini hawana uhakika hata wa mlo wa usiku.

Maarifa ni muhimu na Mungu nae ni Muhimu
Hata Mimi ,nampingaaa
Eti ,
"Usisomeshe watoto kuwa Matajiri"

Huo,itakuwa ni upungufu wa akili,

Kuna ,
Utajiri WA Maarifa ya kimwili
Utajiri WA Maarifa ya kiroho

Vyote Muhimu, vinategemeana,pia
 
Back
Top Bottom