Alfa king jr
New Member
- Jul 28, 2022
- 3
- 3
ELIMU, VIJANA NA MAENDELEO
Sekta ya elimu imeleta mchango mkubwa katika kuendeleza na kujenga uchumi wa nchi na maisha kwa ujumla toka kipindi cha uhuru mpaka sasa. Sekta ya elimu imechangia kwa kiasi kikubwa kuleta maendeleo ambayo tunayashuhudia sasa katika nyanja zote, kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Elimu inategemewa kuleta mabadiliko changa katika maisha ya vijana na kuwasaidia kujikwamua katika wimbi kubwa la umaskini na ukosefu wa ajira. Ongezeko kubwa la wasomi limefanya soko la ajira kuwa finyu ukilinganisha na mahitaji halisi ya jamii hususani wimbi kubwa la vijana wanaohitimu masomo katika vyuo mbalimbali nchini katika fani mbalimbali.
Tukiwa kama vijana tunakabiliwa na changamoto nyingi hasa zile za kiuchumi. Hali inayosababishwa na misingi isiyo imara hasa katika familia zetu pamoja na ukosefu wa elimu kombozi ambayo itamtoa kijana kutoka katika wimbi kubwa la umaskini na utegemezi wa fikra katika katika kuajiriwa na pia kumsaidia kijana kujipambanua katika uhalisia wa maisha kupitia hiyo elimu anayoipata.
Ongezeko kubwa la wasomi wasio na kazi linazidi kua tishio mwaka hadi mwaka, uchache wa nafasi za kuajiriwa ni changamoto kwa vijana wengi. Ingawa kwa upande wa mwingine kumekuwa na fursa nyingi za kujikwamua kiuchumi ikiwepo mwamko katika matumizi changa ya mitandao ya kijamii na intaneti, kujiunga na kuanzisha vikundi mbalimbali vya kujikwamua kiuchumi, kujishughulisha katika shughuli za kilimo na ufugaji ingawa mwamko wa vijana umekua mdogo sana katika kujikita kwenye shughuli za kilimo.
Kundi kubwa wamejiingiza kwenye bodaboda, michezo ya bahati nasibu na kamali ili tu kujikwamua angalau kupata hata uhakika wa kula. Mwamko wa vijana katika kutafuta fursa halisi za kujikwamua haijawa mzuri bado na kizingiti kikubwa kukiwa ni utayari pamoja na ukosefu wa mitaji.
Nguvu kazi ya taifa inategemea zaidi mwamko wa vijana katika fursa mbalimbali za kiuchumi na hivyo basi kuna haja ya kuweka mazingira rafiki kwa vijana ili kunusuru wimbi kubwa la vijana kupotelea katika misingi mibovu ya maisha, matatizo ya kisaikologia na misongo ya mawazo pamoja na ongezeko la magonjwa ya kuambukiza na ngono kama Janga la UKIMWI.
Kumekuwa na ongezeko kubwa la matumizi ya madawa ya kulevya, vitendo vya kiharifu kama wizi, ukabaji, uporaji na mengineyo. Kuongezeka kwa matumizi vya mitandao ya kijamii pia kumeleta manufaa kwa vijana ingawa pia imechangia madhara mbalimbali ikiwemo, uharifu wa kimtandao, utapeli pamoja na matumizi mabaya kinyume na misingi ya jamii zetu. Yote hayo yanasababishwa na vijana wengi kushindwa kutafuta fursa halisi za kujikwamua kiuchumi na kuamua kujitafutia njia mbadala zenye kuhatarisha ustawi na jamii kwa ujumla.
Haya yote yanatupa maswali mengi ya kujiuliza ni kwa namna gani tutatumia sekta ya elimu katika kuwanusuru vijana na kutengeneza hazina bora na nguvu kazi ya hapo badae. Ni jinsi gani mfumo wa elimu unaenda kunusuru upotevu mkubwa wa nguvu kazi inayopotelea katika madawa ya kulevya, kamali na tabia za ajabu. Bila shaka kuna haja ya serikali, wadau binafsi, na mtu mmoja mmoja kufikiria hili kwa upana na kujaribu kutengeneza mfumo na ufumbuzi yakinifu ili kunusuru upotevu mkubwa wa rasilimali watu unaongezeka katika jamii zetu.
Sisi vijana kwa nafasi yetu kwa kutambua umuhimu wetu katika kukuza uchumi wa taifa tusikubali kupotelea gizani. Tutumie elimu tuliyopata katika kupata fursa halisi za kuleta manufaa na kujenga nuru yetu ya badae. Hatuna haja kukata tamaa kwani hakuna barabara ndefu isiyovna kona, licha ya changamoto mbalimbali siku moja tutafika panapostahili. Sisi ni nguzo ya taifa la sasa na la badae tusimame imara kujenga maisha yetu ya leo na baadaye yetu kwa ajili ya ustawi wa jamii na taifa letu.
Maendeleo vya elimu yaende bega kwa bega na mapinduzi makubwa katika maisha yetu vijana. Kufeli kwa vijana katika kujipambanua kifursa ni matokeo ya misingi dhaifu mbalimbali ikiwepo mfumo wa elimu na fikra, mitazamo ya jamii serikali na wadau mbalimbali.
Mafanikio ya sekta ya elimu sio tu kuongeza idadi ya wahitimu katika vyuo vyetu bali ni kuleta mapinduzi makubwa katika jamii. Kumwezesha kijana kutawala mazingira yake yanayozunguka katika kujinufaisha mwenyewe.
Kushindwa kwa vijana wengi katika kujikomboa kiuchumi inayonyesha udhaifu uliopo katika mfumo wetu wa elimu, na mtazamo wa jamii na vijana wengi kuhusu elimu na maendeleo.
Kumbe ili kuleta mabadiliko makubwa katika maisha ya vijana tunahitaji mapinduzi makubwa katika mfumo wa elimu na fikra na mitazamo ya vijana.
Mapinduzi hayo yataletwa na na jitihada ya pamoja kati ya jamii serikali na wadau. Kwakubadilisha mfumo na fikra ili kuwàanda vijana kujitambanua katika fursa mbalimbali za kiuchumi na si kumtafuta mchawi au kurushia lawama upande mwingine kuwa sababu ya hili. Daima mabadiliko huanza na sisi tubadilike vijana, serikali na wadau pamoja na jamii kwa ujumla kujenga kizazi imara na taifa imara.
Alfa king jr.

Upvote
5