The Genius
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 822
- 2,095
Adv. Taslima Kaijage
+255 715 / 784 / 774 - 161820
1. Ukinunua ardhi(nyumba,kiwanja,shamba)hakikisha unafannya transfer(kuhamisha umiliki kutoka aliyekuuzia kwenda jina lako Mnunuzi) mara moja kadri uwezavyo.
Wengi mkinunua kwasababu hakuna anayekulazimisha kufanya transfer kwa haraka basi mkishakabidhiwa hati na mikataba ya mauziano mnakaa nazo hata miaka 2 au 3 mkisema nikipata hela ndio nitafanya trasnsfer. Usifanye hivyo.
Mjue kuwa kama hujafanya transfer uwezekano wa aliyekuuzia kukuzunguka na kukuchezea ni mkubwa sana.
Mfano mmoja ni kuwa, aliyekuuzia anaweza kutoa taarifa ya kupotelewa na hati na hivyo kupatiwa taarifa ya Kupotea(lost report).
Kisha, akafanya Tangazo gazeti la kawaida na lile la Serikali(GOVERNMENT GAZETTE@GN).
Kisha, akafanya maombi ya kupatiwa hati mpya kupitia Form No. 3 Chini ya Kifungu cha 38 cha Sheria ya Usajili wa Ardhi, Sura ya 334.
Kisha, atapatiwa hati nyingine mpya. Kwahiyo kutakuwa na hati mbili katika ardhi moja, ile aliyokupa we mnunuzi na hii mpya ya kwake. Huu tayari ni mgogoro mkubwa kwako mnunuzi usiye na hatia(bonafide purchaser).
Akishakuwa na hati hayo mengine anaweza kuyakataa kirahisi, na pengine watu wa namna hii hata zile saini anazokuwa amekuwekea kwenye nyaraka nyingine zinakuwa sio zake.
Lakini mbaya zaidi ni kuwa, usipofanya transfer na wakati umeshanunua, shughuli zote zinazohusu ardhi hiyo, mfano kulipia kodi za ardhi, vibali vya ujenzi, tathmini, tozo na kila kitu kinaendelea kusoma jina la aliyekuuzia na kinafanyika kwa jina la aliyekuuzia.
Maana yake ni kwamba, ushahidi wote wa risiti na nyaraka nyinginezo unaendelea kumtambua aliyekuuzia kuwa mmiliki halali ambapo anaweza kutumia ushahidi huo dhidi yako
Ataonesha risiti zinamsoma yeye na atasema nilikuwa nilipia, atachukua hata kibali cha ujenzi bila we kujua na atakionesha kinamsoma yeye nk, nk.
Ndugu yangu wewe hapo kutoboa katika mazingira hayo unahitaji tu kudra za mwenyezi Mungu kama utabahatika kuzipata hata kukiwa na shauri mahakamani nakala zake zitakua na nguvu ya kisheria wakati wewe utaonekana mwizi au umefoji nakala hizo ulizouziwa
Lakini kama umefanya transfer mchezo huu ni mgumu sana na pengine usiowezekana, na hata ukiwezekana kwa nguvu ya rushwa ama mamlaka bado unaponyeka(curable) kwasababu system huonesha umiliki ulivyokuwa ukihama hadi mmiliki wa mwisho.
Ninachotaka kuwashauri mkafanye transfer haraka mnaponunua. Najua mnaogopa gharama hasa Capital Gain ambayo ni 10%. Lakini hii mbona inazungumzika na huwa inapungua.
Anyway mna uhuru wa kuchagua kati ya shari kamili ya kudhulumiwa ardhi yote au nusu shari ya hiyo 10%.
2. Mkinunua hakikisha mikataba yenu inashuhudiwa na mawakili. Nimeona ule wa Makonda na Gharib ulishuhudiwa na Wakili aitwaye Ibrahim Shineni. Huyu kwasasa ni nguzo muhim mno, yaan mno katika huu mgogoro.
Wakili kwa cheo chake ni afisa wa Viapo(Commissioner for Oaths), ni Mthibitishaji wa Umma(Notary Public), na pia ni afisa wa Mahakama.
Akiwa kwenye mkataba wako wa manunuzi ya ardhi ni mtu muhimu mno na shahidi wako muhimu anayeaminiwa sana na Mahakama.
Basi haya mawili yakufunzeni.
Kipindi kijacho tutakuja na swala la manunuzi ya gari na utaratibu wake kisheria
Ahsanteni sana na Niwatakieni Siku Njema
NB:SWALA LA PICHA KUWA JUU YA MIHURI HILO ACHANA NALO LISIKUUMIZE,NI SWALA LA MAKONDA HILO