Stud
Member
- Jun 13, 2020
- 68
- 53
Kwa muda mrefu sana tumekuwa tukidanganywa kwamba elimu ya vyeti ndio kipimo cha akili au uwezo wa mtu kufikiri. Lakini tukitazama hali halisi ya nchi yetu, tuna viongozi wengi wenye PhD, Master's, au shahada, lakini wanashindwa kufanya maamuzi ya msingi yanayowanufaisha wananchi.
Tuna walimu wakuu wa vyuo vikuu(Haswa vyuo vya biashara) ambao hawajawahi hata kuanzisha biashara ndogo tu. Tuna wasomi wanaoshindwa kueleza kwa lugha rahisi wanachojua hadi mtu wa kawaida aelewe. Halafu tunasema hawa ndio “wameelimika.”
Wakati huohuo, kuna vijana wa kawaida mitaani—hawajasoma hadi chuo, lakini wana ideas nzuri kuhusu maendeleo, biashara, na hata siasa lakini hawazingatiwi au kuwekwa kwenye mifumo dhabiti ya kitaifa ya kuleta impact moja moja kwenye jamii kwasababu hawajafikia level flani iliyowekwa kwenye mfumo wa elimu rasmi. Hawa watu wanafikiria kwa kutumia akili halisi ya maisha(limitless) na si vitabu.
Hivi ni sahihi kama Taifa kuendelea kupima akili ya mtu au uwezo wake wa kuleta matokeo chanya au kuleta suluhu kwenye Jamii, kwa kutumia vyeti vyake kama kigezo kikuu cha utambuzi?
Na kwa nini jamii inaamini mtu asiye na cheti hawezi kutoa mchango mkubwa kwenye taifa?