SoC01 Elimu ya Fedha kwa vijana ndio siri ya Mafanikio

SoC01 Elimu ya Fedha kwa vijana ndio siri ya Mafanikio

Stories of Change - 2021 Competition

Taric Hiyari

Member
Joined
Jul 26, 2021
Posts
5
Reaction score
3
Asilimia kubwa ya vijana waliokuwa katika mifumo rasmi ya Elimu hutumia takribani muda wa zaidi ya Miaka 17 kutumikia katika ngazi tofauti tofauti za elimu zao lakini ndio kundi kubwa la watu ambao wenye elimu ya vyeti lakini ubunifu na maarifa madogo katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii zao ama zetu.

Hakuna binadamu yoyote katika ulimwengu wetu wa sasa anaehangaika huku na kule ila tu kutafuta kitu kinachoitwa "Fedha" kwa kua ndio chanzo kikuu cha kufanya na kutimiza mambo tofauti tofauti katika Maisha ya kila siku ya Mwanadamu, lakini Ndio Mwiba Mchungu unaowachoma wengi hasa wale vijana na Famalia zao ambao hutumia Fedha nyingi kusomesha vijana wao katika Ngazi tofauti tofauti za elimu lakini inakua ni ngumu kurudisha zile fedha zilizowekezwa kwa kijana huyo pindi alipokua masomoni na hata zikifanikiwa kurudi haziwezi kurudisha thamani ya kile kilichotolewa, hii inatokana

Kwanza na Mifumo yetu ya elimu hasa kwa vipindi hivi vya miaka ya karibuni, haitoi Uhakika kwa kile ambacho mtu anachokisomea, Mfano: Je bado kina uhai katika mazingira husika.

Pili hakuna Takwimu elekezi ambayo inayoonyesha kwa kipindi na kipi ni sahihi kuna Uhitaji wa kundi gani la Elimu ambalo litaendana na uhitaji wa soko husika la wahitimu, hivyo basi kuna uhitaji wa kufanyiwa tathmini vitu mfano wa hivi ili kuipa thamani ya yule mtu aliyetumia wakati na rasilimali mbalimbali katika kufanikisha thamani ya elimu yake, Kwa kuwa tunajionea sio tu wale walioajiriwa bali pia hata wale waliopo mtaani ambao hawakupata mfumo rasmi wa Elimu tunaona kila kukicha wakilalama kuhusu ugumu wa Maisha kwa Kusema "Hali imekua ngumu".

Hapa unapata Maswali kwa kujiuliza Je kuna tofauti gani kati ya yule aliyepata elimu rasmi na yule ambaye hakupata licha ya rasilimali tofauti tofauti zinazotuzunguka, Jibu utakalopata ni Moja ambalo kwa haraka zaidi ambalo litaweza kujibu maswali Mengi yatakayokua yakikutatiza kwa kujiuliza tatizo ni nini ?.....

Ni kuwa Vijana Wengi Tunakosa Elimu ya Nidhamu ya Fedha tunaendeshwa na tabia katika Matumizi mbalimbali ya fedha zetu hatuna Mbinu mbalimbali zenye kuleta mabadiliko katika ubadilishaji wa Maisha yetu kama zile za Uwekezaji na kuhifadhi wa kile kidogo tunachokipata "Saving" na hata tukipata bado tunaona hazitoshi hivo kumsababishia kijana kila kukicha kulalamika shida ilhali ni mwenye Uwezo wa kuweza kuzitatua.

Cha kufanya kwanza kama vijana tuanze na mabadiliko binafsi kwakua Mabadiliko huanza na sisi, katika tabia za matumizi ya fedha na kutafuta mbinu mbalimbali za kuweza kumkwamua kijana na Wimbi la Umaskini kwa kua Elimu pekee ya darasani vyuoni pekee haitoshi na hilo limedhihirika wazi na sio tu hao hata wale ambao hawakupata mfumo rasmi nao ni vyema ukawepo mfumo au warsha mbalimbali ambazo zitajikita katika Masuala ya Fedha na namna za kuitumia ili kuweza kukwamua jamii zetu.
 
Upvote 2
Mkuu Bandiko lako ni zuri sana ila lingependeza zaidi kama ungetuelezea kwa mifano hai namna tunavyoweza kupata hizo fedha. Ulichokiandika hakina tofauti na Alichokisoma kijana kwa Miaka 17 huko shuleni.. "nadharia tu"
Kama unataka kutukwamua vijana kifkra leta suluhisho la kupata hizo fedha mkuu, lectures zinachosha akili
 
Back
Top Bottom