Elimu ya majirani ndio inakwamisha EAC

Elimu ya majirani ndio inakwamisha EAC

Jamaa anaongea vitu halisia kuhusu elimu yetu, sie tunaleta siasa kama ilivo kawaida yetu, kweli hii elimu yetu sio mchezo, doh, kazi kuongea kiswaglish , ukiulizwa kwa kimalkia unaanza ooh nakipenda kiswahili zaidi , si tuseme tuu hatujui, ila twapenda kuongea mayai.
ila ukweli elimu yetu inahtaji marekebisho, huwezi fananisha elimu yetu na majirani, hata rwanda waliopigana vita mpaka miaka ya hivi karibuni , wana elimu nzuri kutushinda, sie kazi kukramisha maandiko
 
MK254 ondoa ushudu wako humu. Unafikiri nyie ni tofauti sana? Leta humu takwimu za literacy levels na number of students wanaocomplete each level of education!

nilishampa data huyu ndindindi..,

elimu yao upande wa literacy na reading tulishawapita toka 2009, in terms of quality as per unesco report..,

sasa hivi tutakuwa tumeshawaacha mavumbini. Hawa ni watu wa bla bla. ukiwaletea official reports lazima wakimbie., Ndio maana Muhongo hakupata nao shida kwenye show ya Uganda. Siku wakikutana na mtu kama mimi watalia na kusaga meno.
 
Upo sahihi hapo pa sisi kujituma kwa sababu ya mazingira. Nchi yetu ni ndogo, nusu yake ni kame, hivyo inabidi kila Mkenya achakarike. Watu wanakesha wakisoma, siku hizi hapa kwetu digri ya kwanza haionekani kama kitu. Watu wengi wanasaka uzamifu/Masters kabla hata haujawaza kutafuta kazi. Mimi hapa nimeamka sasa hivi, baada ya kufanyia kazi taarifa/report fula usiku wote. Hakuna mzaha wala utani, lazima ukimbie au ukimbizwe. Lakini kwa Wabongo, kila mtu anabweteka kisa ardhi ni kubwa.

Wakenya wengi tukija Bongo huwa tunahisi kama tupo kwenye holiday fulani. Na ndio maana unaona kuna wale hawataki kurudi nyumbani. Mara yangu ya kwanza kufika Bongo niliwashangaa sana Wabongo. Yaani watu hawana neno "deadline au makataa" kwenye misamiati yao. Unakuta Mtanzania anamlipia Mkenya nauli ya ndege, gharama za hoteli amfanyie kazi fulani, halafu Mkenya ndiye anaishia kumsukuma sukuma huyo Mtanzania. Maana kwenu nyie huwa hamjali hata kama mradi unachelewa kiasi gani.

Miezi yangu ya kwanza kwanza nilikua na wasiwasi sana kila nikiona miradi inachelewa chelewa halafu Wabongo hawaoenekani kujali. Yaani kama jambo la kawaida tu, mkuu wa mradi anakunywa pombe na kujiachia tu, wakati mimi inabidi nisubiri hadi usiku ndio hata ninusie chupa ya pombe. Wakati mwengine nakesha hotelini nikiandaa ripoti huku nina babaika maana muda unasogea na tunachelewa. Lakini kadiri muda ulivyosonga na ndani ya mwaka wa kwanza hata mimi nikaanza kulegea, ikawa nimeanza kuzoea kufanya vitu kibongobongo. Nikawa mvivu na mwenye vijisababu, maisha raha tu Bongo, pombe mwanzo mwisho na hakuna anayeonekana kujali wala kunipelekesha.

Mkenya ambaye ameingia katika hali hiyo, kumtoa labda kwa mapanga na hawezi kutoka hiyo Bongo, maana akirudi huku inabidi apelekeshwe. Hapa hatucheki....
Binafsi ilinibidi nichukue muda mrefu kujirekebisha, nikaacha pombe kabisa na kurejelea bidii ya maisha maana nilijikuta naharibu hela nyingi sana hiyo Bongo, vilabu watu walinifahamu kama rais wa Nairobi.

Labda kwenye huu uongozi wa Magufuli, mtabadilika. Naskia katumbua waziri chapombe, ndio taswira huko hata waziri haoni jambo kubwa kuingia bungeni akiwa mlevi na kujibu maswali kwa jeuri.

Kujisifia upuuzi.

Inawezekana efficiency yako ni ziro kabisa.
 
That has nothing to do with the argument at hand buddy. This is why I prefer arguing with educated fellows.

NairobiWalker
Hehehe!! Man you're damn merciless, handle with care Omera.... Ripping her apart so vociferously, this will discourage her from warming our threads....
 
Jamaa anaongea vitu halisia kuhusu elimu yetu, sie tunaleta siasa kama ilivo kawaida yetu, kweli hii elimu yetu sio mchezo, doh, kazi kuongea kiswaglish , ukiulizwa kwa kimalkia unaanza ooh nakipenda kiswahili zaidi , si tuseme tuu hatujui, ila twapenda kuongea mayai.
ila ukweli elimu yetu inahtaji marekebisho, huwezi fananisha elimu yetu na majirani, hata rwanda waliopigana vita mpaka miaka ya hivi karibuni , wana elimu nzuri kutushinda, sie kazi kukramisha maandiko

Inauma kweli.... Watu wengi humu ni elitist ambao wananufaika pakubwa kwenye mfumo unaowanyima raia wengi elimu ya uwezo wa kuhoji.
Ndio utaona mada kama hii wanatiririka kwa kila aina ya pumba na mapicha ili kuzuia mjadala wenye mantiki. Wapo kikazi, njia rahisi ni kuwapuuza.
 
NairobiWalker
Hehehe!! Man you're damn merciless, handle with care Omera.... Ripping her apart so vociferously, this will discourage her from warming our threads....
Hahaha...........saa zingine mtu anaquote post zako alafu anapost vitu kama mtu asiye na elimu hadi inabidi umwambie ukweli.
 
Kiongozi, taarifa inaongea kuhusu matokeo ya elimu yenu kwa miaka ya hivi majuzi. Hata mwaka jana... Sasa hao ndio Watanzania mnaojiita wa leo jameni kwenye mfumo duni kiasi hicho. Bora hao wazee wa hapo awali, kidogo walizingatia elimu, sidhani kama waliachia mwanafunzi anafikia kufanya mtihani wa mwisho kama hajui kusoma wala kuandika.

Hatari, maana inawafanya mnawaogopa Wakenya linapokuja suala la kufanya chochote kwa pamoja. Hadi mnasuasua kwa kila hatua.
MK254 wakenya mmesoma sana na elimu yenu ni nzuri but plse tumieni hiyo elimubyenu kuijenga kenya moja mumtoe zimwi wa ukabila kwanza ndio muangalie majirani.
 
usis
Yule nyoka aliyemdanganya Hawa kule bustanini alitokea KENYA that's why they have behaved like that!!

usisahau tower of babel pia ilikiwa kenya maana hapo kila mtu na lugha yake yaani na kusoma kote wanakojisifu wameshindwa kuwa wamoja kila mtu anaangalia kabila kwanza then kenya baaadae.
 
Nchi zetu zinahitajiana kwa njia moja au nyingine, lakini ndio pawe na uwiano wenye manufaa baina yetu, ni bora elimu ingekua mfumo wa kutuunganisha. Lakini kwa tulivyo sasa, itakua kila siku mnasuasua kwa kila hatua, kumbe tatizo ni elimu.
Tutakua tunawalaumu kwa mwendo wenu wa kobe bila kujua tatizo lipo hapo kwenye vitabu.

Nashauri tuunganishwe kielimu, tuwe na mtaala mmoja, mfumo mmoja wa elimu.

Mkiona tunawagomea kila kitu mjue hatuwahitaji, c muendelee na mambo yenu mbona mnalazimisha kuwa na sisi? Wapo wengi tu kama rwanda, congo, uganda na wengine wengi tu tutashilikiana nao sio lazima nyinyi.
Mbona CoW imekufa na hamuongei, walishaona nyinyi hamfai wamerudi walipotoka. Tunawapenda sana mjirani zetu na ndio maana huweizi sikia ug au rw wakiipiga vita tz sababu wanajua kuishi na watu na kukumbuka fadhira lkn sio nyinyi.
Tumechoka na kelele zenu, hebu fanyeni yenu nasi tufanye yetu muone kama kuna mtu atawafuatilia mambo yenu.
 
Hakuna nchi yoyote jirani yenu ambayo huwapiga vita nyie, tatizo lenu huwa mna babaika na kuwa na wasiwasi kwa kila kitu, na pia wivu kwa kila anayejituma. Hao Rwanda mumewazingua sana pale walipoonekana kujituma zaidi yenu.
Fahamu CoW ni muungano wa kuharakisha maendeleo ya pamoja na kila nchi imealikwa, haupo kwa ajili ya Tanzania wala nini.
Nchi zote zimealikwa ilmradi zisiwe za kusuasua, na kila nchi ina uhuru wa kuungana na nchi yoyote ile nje ya muungano bila wengine wetu kulialia. Kwa mfano, leo hii Rwanda ina miradi yake na Tanzania, Uganda ina miradi na Tanzania, Kenya ina miradi na Tanzania, lakini pia tuna miradi ya pamoja ndani ya CoW.

Mnachofaa kufanya ni kuboresha miundo mbinu na utendaji wa kazi, maana hilo la kwamba madereva wa malori wanatokea Rwanda kuja hadi Mombasa inadhihirisha mlivyo wavivu kwenye bandari yenu.
 
They need us more than the way we do, they are envious of our land, Kilimanjaro, Diamond Platinum hata na Daraja. They can even still Magufuli they will have a chance.
My pointy end needs a dip in your honey jar.
 
By Augustine Oduor Updated Sun, March 27th 2016 at 00:00 GMT +3 SHARE THIS ARTICLE A class in session at Nachurur primary school in Tiaty Sub County on January 15 2016. The school has only two permanent structures. PHOTO:KIPSANG JOSEPH
Read more at: 8-4-4 education system may be scrapped this week

baada ya ugatuzi mambo tofauti sana. what you are posting tukianza ya umaskini Tz tutakesha niache hayo. pata haya tu...
13244809_1603612749930336_545083536467475150_n.jpg

kliniki ya hapo kijijini kwale mpakani wa kenya na tz
13226801_1603091656649112_2731695834010174667_n.jpg

13177529_1599987496959528_5287162898385123079_n.jpg

zima moto kijijini kwale
248717_1738356303065748_507098117377091295_n.jpg

12065643_1689292114638834_3250793480407687320_n.jpg

12046982_1689291504638895_7863980925263652694_n.jpg

11217185_1689291054638940_2038795984944151380_n.jpg

12049372_1689290881305624_3185433713119925213_n.jpg

12039487_1687833078118071_5368693711794087731_n.jpg

12002971_1687832648118114_253121584817643518_n.jpg

11702873_1681230355445010_1415406497785456249_n.jpg

11059938_1681230318778347_4762139030086770303_n.jpg

11988290_1681230675444978_6460684446130361179_n.jpg

11949445_1681230698778309_3267839132254536168_n.jpg
 
EAC ina kila kitu na kila sababu za kupaa na kuwa ukanda bora Afrika, lakini mojawapo wa sababu zinazofanya tukwame ni elimu duni ya baadhi ya majirani zetu kwenye huu muungano. Na hii imechangia sana kuona watu wana kauli za kiajabu hata huku Jamii Forums.

Mfano hai, majirani zetu Tanzania, unakuta mwanafunzi anafikia hadi darasa la saba halafu anafanya mtihani wa mwisho wakati hajui kusoma wala kuandika. Haingii akilini, yaani afikie hadi kwenye mtihani wa mwisho akiwa kilaza bila uwezo wa kusoma wala kuandika. Halafu wanaachiwa na kuingia sekondari/upili na kuendelea, hatimaye ndio hawa wanapata simu baadaye na kuingia kwenye mitandao ya kijamii na kutuzingua kila siku.

Kweli ni hatari, maana eti ndio kizazi kinachotegemewa kuhusika katika ushirikiano wa kesho baina ya nchi zetu hizi. Hapo unakuta watu wananuna kwa kila azimio, kumbe tatizo ni elimu. Juzi wametutukana sana baada ya kusikia watoto wetu wa darasa la kwanza wanapata laptops.

Taarifa kamili hii hapa

Wanafunzi wasiojua Kusoma na Kuandika wanafaulu vipi Mtihani wa Darasa la Saba? | Fikra Pevu

KILA mwaka zimekuwa zikitolewa takwimu za idadi kubwa ya wanafunzi wanaofaulu darasa la saba na kuendelea na masomo ya sekondari, lakini tukielezwa kwamba hawajui Kusoma, Kuandika na Kuhesabu.

Kwa hakika kabisa, ni jambo ambalo linaumiza kichwa kwa sababu katika mfumo rasmi wa elimu katika nchi hii, kuna mitihani ya kupima uelewa wa wanafunzi kuanzia darasa la nne, ambayo lengo lake ni kuwachuja wanafunzi wanaopaswa kuendelea na masomo ya darasa la tano, kabla ya kuufikia mtihani wa Taifa wa darasa la saba.

Kutokana na mfumo huo, maana yake ni kwamba wanafunzi wote waliopita darasa la nne na hatimaye kufika darasa la saba, wana uwezo kitaaluma. Kwa hiyo, zinapokuwepo taarifa za wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza, ambao hawawezi hata kuandika majina yao, hilo kwa kiasi fulani linakuwa ni jambo la kushangaza.

Agosti 14, 2013, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, akizungumza kwenye Warsha ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa, iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya watendaji wa elimu ngazi ya kanda, mkoa na wilaya, naye alikiri kushangazwa sana na taarifa za kuwepo na wanafunzi wanaofika hadi darasa la saba wakati hawajui kusoma wala kuandika.

“Halafu Ofisa Elimu unawateua wanafunzi wa aina hiyo kwenda Sekondari. Tatizo liko wapi? Uteuzi wenu unazingatia vigezo vipi? Je, hakuna namna ya kuthibitisha wale waliochaguliwa wanajua kusoma na kuandika? Maofisa Elimu mnashirikiana vipi na walimu wakuu katika hili?”alihoji Dk Kawambwa katika warsha hiyo.

Kwa sasa, Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi kila mwaka bila kuwa na stadi za kujua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK), huku baadhi yao hao wakifikia hata kuchaguliwa kuanza kidato cha kwanza.

Takwimu kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) zilizokusanywa katika mikoa yote ya Tanzania Bara katika miaka ya hivi karibuni, ambazo FikraPevu inazo, zinaonyesha kwamba wastani wa chini kabisa wa idadi ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba bila kuwa na stadi za KKK katika kila mkoa ni 200, huku wastani wa juu ukiwa ni wanafunzi 400.

Aidha, akijibu maswali ya wabunge bungeni mwaka huo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo alisema katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2010, asilimia 88 ya wanafunzi wote waliomaliza mwaka huo, walipata daraja la nne na sifuri, huku asilimia 12 tu wakipata daraja la kwanza hadi la tatu, huku akibainisha pia kwamba asilimia 31 ya Watanzania wote nchini walikuwa hawajui kusoma na kuandika.

Wanafunzi-wa-darasa-la-awali-wapatao-90-katika-shule-ya-msingi-Puulu-wilayani-Nyasa-mkoani-Ruvuma-hali-inachangia-kukosa-stadi-za-KKK1.jpg

Wanafunzi wa darasa la awali wapatao 90 katika shule ya msingi Puulu wilayani Nyasa mkoani Ruvuma hali inachangia kukosa stadi za KKK

Takwimu zote hizo TET na Wizara, ni ushahidi tosha kwamba kuna jitihada za ziada zinazotakiwa kuikomboa nchi hii kutoka kwenye dimbwi la ujinga. Ongezeko la wanafunzi wanaopata daraja sifuri, linakwenda sambamba na ongezeko la watu wasiojua kusoma na kuandika.

Ikumbukwe kuwa katika miaka ya 1970 na 1980, Tanzania iling’ara katika nchi za Bara la Afrika, hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara, kutokana na kasi ya kupunguza idadi ya wananchi wake wasiojua kusoma na kuandika.

Chini ya Sera ya Elimu ya Watu Wazima, nchi iliongeza idadi ya watu wanaojua kusoma na kuandika kila mwaka. Manufaa yake yalionekana bayana kwa kuwa watu waliweza kupambana na changamoto zinazowakabili, ikiwa ni pamoja na kuongeza uzalishaji wa mazao mashambani kutokana na kuzingatia elimu ya kilimo bora, sambamba na kuongeza uelewa wa kujikinga na maradhi mbalimbali.

Hadi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere anang’atuka madarakani mwaka 1985, idadi ya Watanzania waliokuwa hawajui kusoma na kuandika ilikuwa ni takriban asilimia tisa (9) tu. Kwa hiyo, kama Taifa, kama tungefanikiwa kuendeleza kasi hiyo ya wakati wa Mwalimu hadi mwaka 2010, tungekuwa na angalau asilimia 95 ya Watanzania wanaojua kusoma na kuandika, sawa na asilimia tano (5) ya wasiojua kusoma na kuondika.

Kuongezeka kwa idadi ya wananchi wasiojua kusoma na kuandika kutoka asilimi tisa mwaka 1985 hadi asilimia 31 mwaka 2010, ni ushahidi tosha kwamba Taifa hili linarudi nyuma kwenye ujinga badala ya kusonga mbele. Historia ya Elimu ya Watu Wazima inaonyesha kwamba ilipofika Agosti mwaka 1975, Tanzania ilikuwa ni nchi ya kwanza ulimwenguni kufanya mtihani wa kisomo kwa watu wazima wapatao zaidi ya milioni 3.8, sawa na asilimia 77 ya watu wazima wote waliokuwa wanahudhuria madarasa ya kisomo hicho.

Aidha, mwaka 1981, Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza katika nchi za ulimwengu wa tatu, kuanzisha kampeni ya kitaifa ya kisomo cha kujiendeleza iliyohusisha watu wazima zaidi ya milioni 1.4 waliofuzu kisomo katika hatua ya nne. Ingawa hivi sasa juhudi zimeanza upya, huku mipango thabiti ikiwa imeandaliwa kwa lengo la kufufua upya kisomo cha kujiendeleza, uchunguzi uliofanywa na FikraPevu umebaini kuwa Taifa hili linakabiliwa na tatizo kubwa la ujinga wa kutojua kusoma na kuandika kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya Tanzania.

Kwa mujibu wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2002, pamoja na matokeo ya tafiti mbalimbali zilizopo, ilikadiriwa kwamba idadi ya watu wazima waliokuwepo katika nchi hii, ambao walikuwa hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu, walikuwa ni milioni 5.5, sawa na asilimia 32 ya Watanzania wote wa mwaka huo. Miaka 10 baadaye, kwa maana ya matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012, idadi ya watu ambao hawakuwa wakijua kusoma, kuandika na kuhesabu, ilifikia jumla ya watu takriban milioni 11, sawa na ongezeko la ujinga mara mbili ya ule wa mwaka 2002.

Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa katika Sekta ya Elimu, ambao umeamua kuwaondolea mrundikano wa masomo wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili, na kuwabakiazia masomo matatu tu ya Kuandika, Kusoma na Kuhesabu, pengine ni mikakati unaoweza kusaidia kupunguza tatizo hili la wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza bila kuwa na stadi yoyote ya KKK.

Hii ni changamoto mpya kwa Serikali, kupitia Wizara ya Elimu katika kuhakikisha kwamba mtaala huo mpya wa kujenga stadi za KKK katika shule za msingi, unatekelezeka kwa vitendo ili kuinusuru nchi hii kutoka katika wimbi kubwa la watu wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu.

baada ya ugatuzi mambo tofauti sana kenya. ya watanzania kuishe kwa self denial!!
13244809_1603612749930336_545083536467475150_n.jpg

kliniki ya hapo kijijini kwale mpakani wa kenya na tz
13226801_1603091656649112_2731695834010174667_n.jpg

13177529_1599987496959528_5287162898385123079_n.jpg

zima moto kijijini kwale
248717_1738356303065748_507098117377091295_n.jpg

12065643_1689292114638834_3250793480407687320_n.jpg

12046982_1689291504638895_7863980925263652694_n.jpg

11217185_1689291054638940_2038795984944151380_n.jpg

12049372_1689290881305624_3185433713119925213_n.jpg

12039487_1687833078118071_5368693711794087731_n.jpg

12002971_1687832648118114_253121584817643518_n.jpg

11702873_1681230355445010_1415406497785456249_n.jpg

11059938_1681230318778347_4762139030086770303_n.jpg

11988290_1681230675444978_6460684446130361179_n.jpg

11949445_1681230698778309_3267839132254536168_n.jpg
 
Hakuna nchi yoyote jirani yenu ambayo huwapiga vita nyie, tatizo lenu huwa mna babaika na kuwa na wasiwasi kwa kila kitu, na pia wivu kwa kila anayejituma. Hao Rwanda mumewazingua sana pale walipoonekana kujituma zaidi yenu.
Fahamu CoW ni muungano wa kuharakisha maendeleo ya pamoja na kila nchi imealikwa, haupo kwa ajili ya Tanzania wala nini.
Nchi zote zimealikwa ilmradi zisiwe za kusuasua, na kila nchi ina uhuru wa kuungana na nchi yoyote ile nje ya muungano bila wengine wetu kulialia. Kwa mfano, leo hii Rwanda ina miradi yake na Tanzania, Uganda ina miradi na Tanzania, Kenya ina miradi na Tanzania, lakini pia tuna miradi ya pamoja ndani ya CoW.

Mnachofaa kufanya ni kuboresha miundo mbinu na utendaji wa kazi, maana hilo la kwamba madereva wa malori wanatokea Rwanda kuja hadi Mombasa inadhihirisha mlivyo wavivu kwenye bandari yenu.

Na kwanini wasilalamike hao warwanda uje ulalamike wewe kwa niaba yao kama tuliwazingua, na utueleze tuliwazingua kwa lipi? Acha kushoboka wewe!
Kama hiyo CoW ni ya kuharakisha maendeleo mbona hatuoni iki exist?
Mlishadai uchumi wetu mdogo na mambo mengine meengi, sasa kwanini msitafute mnayelingana naye mkaendelea na mambo yenu, kwanini kila siku tz,? Mnaweza tu kuendelelea na mambo yenu, hizo shobo ss tumeshazichoka sasa, mbona wagumu kuelewa nyinyi viumbe?
 
Tatizo lenu ni moja tu, mnatafuta u big brother EA kitu ambacho hakitokuja kutokea.
 
baada ya ugatuzi mambo tofauti sana. what you are posting tukianza ya umaskini Tz tutakesha niache hayo. pata haya tu...
13244809_1603612749930336_545083536467475150_n.jpg

kliniki ya hapo kijijini kwale mpakani wa kenya na tz
13226801_1603091656649112_2731695834010174667_n.jpg

13177529_1599987496959528_5287162898385123079_n.jpg

zima moto kijijini kwale
248717_1738356303065748_507098117377091295_n.jpg

12065643_1689292114638834_3250793480407687320_n.jpg

12046982_1689291504638895_7863980925263652694_n.jpg

11217185_1689291054638940_2038795984944151380_n.jpg

12049372_1689290881305624_3185433713119925213_n.jpg

12039487_1687833078118071_5368693711794087731_n.jpg

12002971_1687832648118114_253121584817643518_n.jpg

11702873_1681230355445010_1415406497785456249_n.jpg

11059938_1681230318778347_4762139030086770303_n.jpg

11988290_1681230675444978_6460684446130361179_n.jpg

11949445_1681230698778309_3267839132254536168_n.jpg
Safi sana naona baada ya miaka kaa mitano hivi tutakua mbali sana.hawa jamaa kazi kupost expired pictures.
 
Back
Top Bottom