Elimu ya Nape Nnauye

Elimu ya Nape Nnauye

Chama

Kwani katibu wa Uenezi wa CCm ana msemaji wake?. Naona wewe umekuwa msemaji wa Nape humu. Swala la msingi, muache nape mwenyewe aje humu (yeye ni mwanachama pia), atueleze ni kwa vipi baada ya kupata Divison Four ya 29, aliwezaje kufika chuo na kupata Bachelor na hadi Masters.

Hii itaweza kuwasaidia pia au kuwapa mwanga, hawa wadogo zetu waliopata division four kama ya nape, nakujua ni kwa jinsi gani, ukifeli form four unaweza kuendelea na ukapata elimu ya juu zaidi.

Pia, inakupasa utambua, kupata division four, sio dhambi, ni uwezo tu wa akili wa mtu, ambao Mungu amempatia. Kwa hiyo ingekuwa vyema, ungeacha kumtetea huyo nape na yeye mwenyewe, aje atupe experience yake ya maisha, baada ya kufeli form four....
 
Halafu bado tunaendelea kujiuliza kwa nini kiwango cha elimu kinashuka, Kama a form four failure like Nape can soldier on to acquire a masters degree without passing to the Advanced level of secondary school and hence ascend to the top post in the contries leading political party, why should they bother to study hard while you can make it into life without passing?
.
 
Acheni ujinga nyie...form six,masters,b achelor hazitusaiii na wala sioo vigezo pekee vya kupima watu....angalieni deliverables.....Nape anadeli ver vipi na Mnyika anadeliver vip?
 
Kilaza ni nani mwenye masters? Au mwenye elimu ya kidato cha 6

Chama
Gongo la mboto DSM

Jamani masters hizi za Mzumbe ni masters gani ? mbona chuo hiki kina aibisha maana kuna watu wengi ambao ni vilaza kabisa lakini wana masters za Mzumbe. Mie namjua daktari moja kilaza kabisa na amesoma masters Mzumbe na sasa yupo kwenye siasa.ni kilaza kabisa naye alisoma kwa kuungauga.
Nadhani chuo hiki kina sifa ya kuwaungisha watoto wa vigogo ili wawe na cv za makaratasi lakini kichwani pumba
 
Tuliomfahamu Nape tulikaa kimya,mana tulijua anafukunyua kitu asichokiweza!!Nape alikuwa Mkristo mzuri sana,alifahamika kama mpendwa,muimba kwaya na mpiga gitaa mzuri...!alienda Kivukoni akapata cheti,then baadae akatumia cheti kupata Diploma...akatumia cheti cha Diploma kuchukua Degree ya Journalism India...then Masterz ya Mzumbe!
 
Huyo chama atakuwa ni nape mwenyewe anawazingua.haiwezekani umtete na kumsemea mwanaume mwenzio au utakuwa bwabwa lake.maana hata comment zake kama shoga , si rizki
 
Last edited by a moderator:
Tunazungumzia elimu hapa kama kupresent paper ndio digrii hilo nimekubaliana na wewe

Chama
Gongo la mboto DSM

unavyojitutumua kujibu kwi kwi kwi utafikiri wewe ndio nape, mnyika alikuja hapa akajibu , why not nape to do the same? Unakomaaa vidole vitapata sugu hivyo we want to hear from Nape unless u-verify kuwa wewe ndio msemaji wake!
 
i start to believe nape and chama could be one and the same person
 
najua elimu ina matter ila jamani na uwe mtendaji kazi.unaweza ukawa na elimu yako,ikakupa jeuri ila masuala ya kazi ukawa si mtendaji wa kazi na ukapitwa,kwa wale wenye elimu ya chini zaidi yako.kuna sehemu nilikuwa nafanya tempo,kuna dada alipunguzwa kazi kwa sababu ya elimu ndogo.ila huyo dada alikuwa kazi anaijua na anaiweza kuliko hao wenye elimu zao.
 
Mkuu Chama ni vyema
ukatuambia ana masters ya nini; kwani yawezekana siku hizi Mzumbe
wameacha kutoa masters za Ki-china na kuanza kutoa Masters za
MATUSI.

Nape ameokoka toka Nsumba Secondary hawezi kumtukana mtu
 
Wajameni mwenye andika lolote la Nape la lugha za kikoloni aliweke hapa. Mimi na uzee huu sijawahi kumsikia Nape akizungumza kimombo a.k.a english.

Tumeishaona mara kibao JK anavyopata kigugumizi linapokuja suala la kugonga yai.
 
Kilaza ni nani mwenye masters? Au mwenye elimu ya kidato cha 6

Chama
Gongo la mboto DSM
KILAZA Ni mwenye vyeti vya elimu ya juu lakini hana elimu hiyo. Hapa ni kama unaelewa maana ya ELIMU.
 
HUKO Mzumbe wengi wamepata "za Kutungua" na "za "KUAZIMWA" tukianza na Deodorius Kamara, Nchimbi na sa tunaambiwa Nape
Jamaa wanatoa Excutive Masters ndo maana wengi wanakimbilia huko....yaani hiyo masters mnaamua kituo cha mihadhara kiwe wap mwezi huu mwanza, mwezi ujao arusha ni....
wakifeli wanakimbila kwa makamu mkuu wa chuo na kuchimba beat kwa mgongo wa nafasi zao serikalini...mpaka wahadhiri wengi wanakimbia kufundisha madarasa ya watu wa Excutive Masters
 
John Mnyika alikuwa natafuta sympath kwa watu wasiosoma hakukuwa na jibu lolote la kunishtua mimi; yeye ni form 6 tu hana cha zaidi

Chama
Gongo la mboto DSM
Nilivyokuelewa wewe unathamini vyeti kuliko uelewa na ili ndilo linatuharibia nchi watu kujisifu kwa vyeti vyao bila kuelimika.
Nikuhakikishie kuwa ukiwawekea mtihani wa O'level leo hii Nape Nnauye na John Mnyika bado kilaza atakuwa yuleyule tena si ajabu utakutana na majibu ya matusi kulingana na fani ya kila mtu kwa sasa!.
 
Huyu chama atakua anasuguliwa na Nape.. Yeye ndo msemaji wake?..hyo Masters yake imemsaidia nn? Mbn uwezo wake wa kufikiri na masters yake havihusiani?
 
Last edited by a moderator:
Nape Nnauye ana masters John Mnyika ana nini?

Chama
Gongo la mboto DSM

Kiutendaji, elimu haitusaidii sana Watz, Angalia waziri wa Elimu and PHD, lakini angalia Elimu yetu inavyoporomoka kutoka mwaka hadi mwaka. Waziri wa Ulinzi Dr. Nchimbi, anglia hali ya amani ilivyo tete nchini. Rais wako ni PHD holder, anglaia nchi ilivyomshinda vibaya. Waziri wa Nishati na madini ni Professor, Muhongo, angalia umeme unavyotutesa, angalia mikataba feki ya madini na na gesi. Waziri wa Kilimo na Mifugo huyu Professor Jumanne Magembe, eti ni professor, lakini angalia Kilimo kinavyorudi nyuma mwaka hadi mwaka na angalia migogoro ya wakulima na wafugaji inavyokuwa mikubwa bila utatuzi.

Ukweli ni kwamba JJ Mnyika hana degree, wala hata hiyo masters ya Nape, lakini angalia michango yake Bungeni na Utendaji wake Jimboni. Ni Tofauti kabisa na Utendaji wa akina Magembe na Kawambwa wenye PHD na Professors wa ccm.

Kwani akina Moringe Sokoine walikuwa na elimu gani iliyowafanya wafanye kazi kwa weledi ule uliotukuka? Huwezi kufamnanisha Mnyika na Nape Kwa lolote lile, na ukisema Nape ana Masters mbele ya watu wasomi, wakilinganisha na utendaji wake wa kazi hasa matamko anayotoa, watakushangaa sana.

Poleni wote mnaodhani kuwa John Mnyika atang'oka Ubunge kwa kigezo cha Elimu. Hiyo ni ndoto, ingelikuwa hivyo, Prof. Lipumba angelikuwa kiongozi mkuu wa Taifa hili, lakini wapi, ndoto zake zinazidi kupotea kila siku.

NSWIMA J. E.
MPANDA, KATAVI.
 
Back
Top Bottom