Baada na hata kala ya kubuni na kusambaza tuhuma za uongo dhidi ya Ndugu John Mnyika,historia ya elimu ya Ndugu Nape Nnaye imekuwa, mara kwa mara, ikihojiwa na wafuatiliaji wa masuala ya mambo, hasa wanaojali na kuamini katika weledi, umahiri na umakini wa watekelezaji na wasimamizi wa majukumu mbalimbali katika ngazi na maeneo mbalimbali ya kiutawala..
Kwa kadiri ya ufahamu wangu,ningependa kuweka wazi kabisa kuwa Ndugu Nape amepata kusoma katika ngazi ya Kidato cha Sita na hatimaye kupata daraja sifuri. Kwa matokeo hayo, ni dhahiri kuwa Nape hana Elimu ya Kidato cha Sita.Kwa kuwa inafahamika kuwa Nape alipata daraja la Nne (IV) la pointi 29 katika mtihani wa Kidato cha Nne na kwa kuwa mantiki ya kawaida inaweka sharti la mtahiniwa yeyote wa Kidato cha Sita kuwa na angalau credits tatu katika matokeo ya Kidato cha Nne; basi, inafuata kimantiki, kuwa, Ndugu Nape amepata kufanya Mtihani wa marudio kwa minajili ya kupata alama ambazo zingemwezesha kuweza kumpa sifa ya kuweza kufanya mtihani wa Kidato cha Sita.
Katika hali ya isiyojulikana msingi wala nia yake, Ndugu Nape amekuwa si muwazi na mkweli hata kidogo katika historia yake ya kielimu na kitaaluma ingawa yeye mwenyewe amejivika jukumu la kuhoji viwango vya Elimu vya wananchi wengine. Kutokana na hali hiyo, wafuatiliaji wa elimu yake wamekosa majibu sahihi na yenye kujitosheleza.
Aidha mtu huyu amethubutu hata kudanganya umma mara kadhaa kuwa amepata kusoma katika Shule ya Sekondari Mwenge iliyopo iliyopo Singida, na kuhitimu Kidato cha Sita mwaka 2000. Hii si kweli. Baadhi yetu tunajua ,yeye mwenyewe anajua, ndugu zake wanajua na hata Utawala wa Shule kuwa huu ni uongo wa wazi. Nape, ingawa anaijua vema shule hiyo kongwe kabisa iliyopo Mjini hapo, hakupata kuwa mwanafunzi katika shule hiyo. Ukweli ni kuwa alifanya mtihani wa kidato cha Sita,kama mtahiniwa wa kujitegemea katika shule hiyo na kupata daraja sifuri.
Aidha, Nape katika miaka ya mwanzoni mwa 2000 alikuwa na kawaida ya kwenda katika shule hiyo kwa shughuli za Uinjilisti, akiwekeza katika kuwalea wanafunzi kiroho wa kikundi cha CASFETA shuleni hapo. Sasa, kama kufundisha dini tu mara moja kunampatia mhusika hadhi ya uanafunzi katika shule basi tunao wanafunzi na wahitimu wengi katika nchi hii kuliko tunaowajuai!
Mwisho kabisa ningependa kumsihi Nape ajenge utamaduni na tabia ya kusema ukweli maana ukweli, daima, utamuweka huru. Hii ni muhimu kwa kuwa haiwezekani kuwa mtu mwenye hadhi ya mtumwa katika kasri la Mfalme kupanga na kuratibu mkakati na mbinu za kuwatoa watumwa wengine wa kweli na wa uongo kutoka katika vifungo vya utumwa.