Elimu ya Tanzania haimkomboi kijana zaidi ya kuendeleza ujinga

Elimu ya Tanzania haimkomboi kijana zaidi ya kuendeleza ujinga

Tofauti ya elimu sasa na elimu ya jadi ni kuwa elimu ya jadi mtu liipata jinsi anavoishi, analima. Anavyovua, anavyowinda nk. Mtu aliipata katika maisha ya kila siku na si kwa kukaa darasani. Ilikuwa ni elimu kamili inayojitosheleza.
Elimu ya sasa ni elimi ilopangwa na hupatikana darasani chini ya mwalimu aliyeandaliwa.
Mwanafunzi huipata darasani kama kifurushi cha vocha na hutakiwa kwenda kuitumia.
Hapa tatizo linakuja je, kifurushi ni sahihi, kuna mtandao, wa kumpigia yupo nk. Kwa hiyo kifupi elimu ya darasani ina masharti yake.
Ndio maana tunalalamika elimu hii inasaidia nini.
So, ili elimu iwe na manufaa ni lazima ihusishwe na mazingira na mahitaji ya jamii kwa ujumla. Ni lazi iangalie matatizo yaliopo na ilenge kuyatatua.
 
HIZI NDIZO SABABU KUU MBILI ZINAZO SABABISHA UMASIKINI TANZANIA NA AFRIKA KWA UJUMLA

1: UDHAIFU WA ELIMU YETU
Elimu yetu haijitosherezi wala haiendani na dunia tuliyo nayo leo tofauti na mataifa mengine kama Uingereza, Marekani, Canada n.k

Mfano mwanafunzi Alie Soma kombi ya HGK/HGL/HKL kwa level ya kidato cha sita unaweza kunambia ni kitu gani ambacho mwanafunzi huyu anakua ametoka nacho shuleni ambacho kinaweza msaidia kuja kutatua changamoto za mtaani?

Just imagine mwanafunzi alie Soma history anatoka shuleni akiwa anafahamu mambo yaliyo tokea nyuma miaka 70 iliyo pita; mfano vita vya Kwanza ya dunia, anguko la uchumi wa dunia.

Sasa ashumu mtoto anatoka shuleni amekalili mambo ya miaka 70 nyuma, mtoto anatoka shuleni anajua mambo ya kuandika insha, kujitambulisha, kutafasiri maneno na namna ya kuwasiliana (IELTS) kwenye language.

Ukija kwenye geography mtoto anakuja kasoma mambo ya ma barafu kama topic, ukiangalia barafu tunazo zisoma zinapafikana nchi za wenzetu canada, USA n.k Sasa hapa unategemea lini Africa tutajikomboa kwenye dhahama ya umasikini?

Just imagine msomi mwenye level ya form 6 anakuja nyumban kichwani akiwa amebeba 85% ya mambo ambayo hayana impact kwenye suala la kujikwamua kiuchumi. Shame.

Viongozi tunao waona leo ni zao la elimu yetu kwa aslimia kubwa, labda ukitoa elimu za juu walizo kwenda kupata huko ughaibuni.

Ushauri wangu kwenye suala la elimu, Tanzania tunahaja ya kuireform elimu yetu tusiendelee na elimu ya kukalili kujibu mitihani, Tunahitaji elimu ya kuweza kutatua changamoto tulizo nazo.

Wanafunzi wasome kama ni mambo ya kilimo, ufugaji uvumbuzi ingali wakiwa vidudu, wasome namna ya kutumia vyanzo vyetu vya maji katika kukuza secta ya kilimo kuanzia vidudu mpaka vyuoni,

Wasome namna ya kutumia kilimo chetu kulingana na mazingira ya kila kanda, huwezi amini wavyetinam walikuja Tanzania kujifunza kilimo Cha alizeti, lakin leo sisi ndio tunaagiza mafuta ya kula kwa wanafunzi wetu na alizeti yetu haina ubora tena. Inaumiza Sana.

Kama ni ufungaji wajifunze ufugaji unao patikana kwenye taifa letu na namna ya kutumia,

Tuache kukalili ufugaji ambao unapatikana ulaya na Marekani afu mwanafunzi anaenda kujibia mtihani huu ni ujinga kwa Africa nzima.

Inasemekana kwasasa kuna hatari ya kupoteza kuku asilia kutokana nakukosa ubora yaan wanakua wadogo na si wazito hivyo hukosa sifa katika soko la biashara, lakin kumbe kuku wa kitanzania akifungwa vizuri anauwezo wa kufikisha mpaka kilo 4) ila mtoto anamaliza form 6 hajui hata namna ya kufunga kuku afu Wana siasa wanao kula mshahara wa zaid ya 11ml anakuja anakwambia watoto wajiajiri, hawa ni wajinga walio zalishwa na elimu yetu.

2: SIASA NA WANASIASA (mfumo wa utawala na viongozi)
Tukatae tukubali kalibu 98% za hatima ya maisha yetu hasa ki uchumi huamuliwa na wanasiasa kwakua wao ndo hutunga sera zote za maendeleo ya taifa.

Kama nilivyo sema kwenye hoja ya elimu viongozi tulio nao Leo ni zao la elimu yetu hii tuliyo achiwa na mkoloni ambayo ni duni na haitoi hatima ya kujikomboa kama taifa.

Imekua kawaida Sana kuwa na wanasiasa ambao hawana vision kwa taifa lao wala mikakati maarumu ya kiukombozi kwa taifa letu.

Viongozi walio bahatika kupata elimu za juu, huja na maneno ya ki ulaghai, na kuwaaminisha watu kua uzalendo ni kuhakikisha unapambania chama kubaki madalakan, na kwa bahati mbaya wamefanikiwa pakubwa kutuaminisha hivyo kwa maslahi yao wenyewe.

Sisi kama taifa tunaongozwa na maono ya mtu mmoja, katiba yetu ya Tanzania imempa mamlaka makubwa Sana kiongozi wetu mkuu wa nchi yeye ndo muamzi wa kila kitu, mfumo wetu wa utawala na uongozi ni mmbovu kuanzia ngazi ya chama mpaka serikali, katika chama silaumu Sana maana mfumo unaminufaisha chama na wala sio taifa.

Yaan kwamba rais anakua mwenyekiti wa chama na Bado ni kiongozi wa taifa na ni amiri jeshi mkuu.

Katiba yetu inampa kiongozi wa nchi mamlaka makubwa na kuwekewa kinga, huu ni udhaifu kama taifa. Kwakua muwekezaji anauwezo wa musoma katiba yetu leo na sheria zetu za nchi akagundua udhaifu wetu kama nchi upo wapi na ni sehem gani pa kupitia.

Mfano mwekezaji akipitia katiba sheria zetu akagundua udhaifu wetu sisi ni kutoa mamlaka yote kwa rais na kumpa kinga, yeye atawaza namna ya ku deal na rais akimuweza rais ujue ameweza taifa.

Yatatokea yale ya kiongozi mmoja aliye kuja na sera za ubinafshaji, kwenye mgodi wa geita Tanzania ikawa inachukua 3%, kampuni GGM 70% zileeeee 27 utajua mwenyewe aliye kua anazichukua.

Just imagine yaan taifa linapata 3% kweli? Shame

Hapa kama taifa ndipo kuna udhaifu.

Ushauri wangu kwenye inshu ya siasa

Sisi kama watanzania wenye uchungu na nchi yetu maamuzi yetu ni hatima ya taifa letu, tunawajibu wa kuyatafakari maisha yetu na haya ya wana siasa, tuna wajibu wa kutuliza akili na kukuunga mkono kila mwenye hoja ambayo unaona utalikomboa taifa, tukubari tuwe na katiba mpya

ukiachana na hizi siasa za mahaba za apa tanzania zilizojumlishwa na elimu mfano (BIG RESULTS NOW): elimu unayosoma its almost the same as sehem ingine duniani wanayosoma! 1+1= 2 , hakuna sehem duniani wanasoma ni 3!

hakuna sehem yoyote duniani waishawahi kuajiri wananchi wote na ni kitu hakiwezekani hata mkishirikiana na private sector no where ajira znaweza kupatikana za namna hio, ela yenyewe ni limited na haitakiwi kila mtu awe na ya kutosha kwa sababu ya kuleta uvivu

vitu ambavyo hujui hata nchi zingine watu hukimbia shule kuanza biashara zao wenyewe
wapo watanzania wengi tu wameenda kusoma nje ya nchi na wamerudi bongo, hio elimu waliokuja nayo ni same same hatuwaoni wakitumia izo elimu kujiajiri kama mnavoisema vibaya elimua ya tanzania
 
Mifumo mibovu imeletwa na CCM

we jamaa una hasira sana na ccm ila i can tell you mambo mengi tu ni sisi wananchi wenyewe tunakwama! suala la elimu wapo wengi tu wanasema elimu ya tanzania mbovu na wanaenda kusoma nje, wakirudi nini cha maaana wanafanya?
 
we jamaa una hasira sana na ccm ila i can tell you mambo mengi tu ni sisi wananchi wenyewe tunakwama! suala la elimu wapo wengi tu wanasema elimu ya tanzania mbovu na wanaenda kusoma nje, wakirudi nini cha maaana wanafanya?
Toa mfano 20
 
Toa mfano 20

mamlaka ya vyuo vikuu vya nje ina rekodi ya wanafunzi wangap walioenda kusoma nje ya nchi? private sectors znazopeleka wanafunzi nje ya nchi zina miaka mingap apa tanzania? what have we achieved so far zaidi ya kua kwenye interview wanasema wanauza makande?
 
mamlaka ya vyuo vikuu vya nje ina rekodi ya wanafunzi wangap walioenda kusoma nje ya nchi? private sectors znazopeleka wanafunzi nje ya nchi zina miaka mingap apa tanzania? what have we achieved so far zaidi ya kua kwenye interview wanasema wanauza makande?
Kula ulale sister ako kaivisha
 
Tatizo la elimu ni dogo. Ukubwa wa tatizo unatokana na vijana kutokujielewa, wengi wamejisahau na kubaki kuwa misukule ya watu ndio maana wanasiasa hawawaheshimu.

Leo bodaboda, au msanii anaheshimika kuliko wewe graduate kwasababu wao wanacho cha kutoa kwa wanasiasa.

Mfano: Graduate ni msukule lialia wa Diamond kiasi kwamba yeye maisha yake hayapi kipaumbele, Wanasiasa wakimpata Diamond wameshampata na huyo graduate, sasa why huyo graduate asudharaulike ?

Ukimpata Gwajima, umepata waumini wake wote.

Ukiipata BAkWATA umepata waumini kibao wa kiislamu.

Graduate are no where to be seen.

Bora hata machinga serikali ikitaka kuwaletea ujinga inawaza mara mbili mbili.

Tena sasa hivi ni TRENDS,

Kuna wajanja wachache wanatengeneza lundo la wafuasi lialia halafu wanaliuza kwa wanasiasa,

1- Kamati ya amani ( Malasusa )

2- Mama sema na mwanao ( steve Nyerere )

Jobless vijana zindukeniiiiiii. Angalieni kwanza vipaumbele vyenu kabla hamjawa wafuasi lialia wa wanasiasa, wasanii au viongozi wa dini.
 
Back
Top Bottom