Elimu ya Tanzania haimkomboi kijana zaidi ya kuendeleza ujinga

Tofauti ya elimu sasa na elimu ya jadi ni kuwa elimu ya jadi mtu liipata jinsi anavoishi, analima. Anavyovua, anavyowinda nk. Mtu aliipata katika maisha ya kila siku na si kwa kukaa darasani. Ilikuwa ni elimu kamili inayojitosheleza.
Elimu ya sasa ni elimi ilopangwa na hupatikana darasani chini ya mwalimu aliyeandaliwa.
Mwanafunzi huipata darasani kama kifurushi cha vocha na hutakiwa kwenda kuitumia.
Hapa tatizo linakuja je, kifurushi ni sahihi, kuna mtandao, wa kumpigia yupo nk. Kwa hiyo kifupi elimu ya darasani ina masharti yake.
Ndio maana tunalalamika elimu hii inasaidia nini.
So, ili elimu iwe na manufaa ni lazima ihusishwe na mazingira na mahitaji ya jamii kwa ujumla. Ni lazi iangalie matatizo yaliopo na ilenge kuyatatua.
 

ukiachana na hizi siasa za mahaba za apa tanzania zilizojumlishwa na elimu mfano (BIG RESULTS NOW): elimu unayosoma its almost the same as sehem ingine duniani wanayosoma! 1+1= 2 , hakuna sehem duniani wanasoma ni 3!


 
Mifumo mibovu imeletwa na CCM

we jamaa una hasira sana na ccm ila i can tell you mambo mengi tu ni sisi wananchi wenyewe tunakwama! suala la elimu wapo wengi tu wanasema elimu ya tanzania mbovu na wanaenda kusoma nje, wakirudi nini cha maaana wanafanya?
 
we jamaa una hasira sana na ccm ila i can tell you mambo mengi tu ni sisi wananchi wenyewe tunakwama! suala la elimu wapo wengi tu wanasema elimu ya tanzania mbovu na wanaenda kusoma nje, wakirudi nini cha maaana wanafanya?
Toa mfano 20
 
Toa mfano 20

mamlaka ya vyuo vikuu vya nje ina rekodi ya wanafunzi wangap walioenda kusoma nje ya nchi? private sectors znazopeleka wanafunzi nje ya nchi zina miaka mingap apa tanzania? what have we achieved so far zaidi ya kua kwenye interview wanasema wanauza makande?
 
Kula ulale sister ako kaivisha
 
Tatizo la elimu ni dogo. Ukubwa wa tatizo unatokana na vijana kutokujielewa, wengi wamejisahau na kubaki kuwa misukule ya watu ndio maana wanasiasa hawawaheshimu.

Leo bodaboda, au msanii anaheshimika kuliko wewe graduate kwasababu wao wanacho cha kutoa kwa wanasiasa.

Mfano: Graduate ni msukule lialia wa Diamond kiasi kwamba yeye maisha yake hayapi kipaumbele, Wanasiasa wakimpata Diamond wameshampata na huyo graduate, sasa why huyo graduate asudharaulike ?

Ukimpata Gwajima, umepata waumini wake wote.

Ukiipata BAkWATA umepata waumini kibao wa kiislamu.

Graduate are no where to be seen.

Bora hata machinga serikali ikitaka kuwaletea ujinga inawaza mara mbili mbili.

Tena sasa hivi ni TRENDS,

Kuna wajanja wachache wanatengeneza lundo la wafuasi lialia halafu wanaliuza kwa wanasiasa,

1- Kamati ya amani ( Malasusa )

2- Mama sema na mwanao ( steve Nyerere )

Jobless vijana zindukeniiiiiii. Angalieni kwanza vipaumbele vyenu kabla hamjawa wafuasi lialia wa wanasiasa, wasanii au viongozi wa dini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…