Amon Mtekateka
JF-Expert Member
- Jun 4, 2014
- 1,225
- 333
hawa jamaa kwasababu wao walifeli bac wakiona wenzao wanafaulu kwa wingi.
wanakua na wivu kweli.
wanakua na wivu kweli.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Acha dharau dogo nan alifeli? Mm menyewe nina dogo langu hapa limepiga PCB mwaka huu Lina b+*3 lenyewe hata haliamin amin.... Acha ku attack watu jadili hoja hapo juu ni nn kilichoongezwa mpaka brn watu watusue kiasi hiki?
Nakumbuka hii issue ya nyie kutusua ilianzaga pale necta ilipofuta matokeo na kusahihisha upya ndipo utusuaji ulipoanzia mpaka leo
We umeangalia tu idadi ya ufaulu kuongezeka bila kuangalia alama za ufaulu (PRINCIPLES) kushuka..... teh teh teh teh! hakika unajadili kisiasa na sio kitaaluma! Mfano, C yazanani kwa sasa ni sawa na D.Ukiangalia matokeo ya form VI toka BRN ianzishwe yamekuwa yakipanda mwaka hadi mwaka. Mimi binafsi huwa najiuliza ni nini kinacho boost matokeo yao ikiwa walimu morali yao ya kufanya kazi iko vile vile kutokana na kudai haki zao nying tu. Pia syllabus ni zile zile, topics ni zile zile, sasa ni kitu gani kilichobadil upepo wa matokeo? Kabla ya hii BRN mtu wa PCB alikuwa akipata ccc 1.9 alikuwa na uhakika wa kusoma MD chuo chochote alichohitaji leo hii mtu huyo huyo kupata hiyo MD ni mbinde. Je ndo kusema wanafunzi wa sasa wana bidii sana kwenye masomo yao kuliko wale wa kabla ya hii BRN?
Naomba tujadili wakuu.
Inashangaza sana miundo mbinu ile ile eti iliyokua inatumika miaka yote eti baada ya miaka ya BRN ufaulu umepanda ghafla Bini vuu. Hii si kweli kabisa mi haya matokeo kuanzia form four na form six ni ujanja ujanja tu na lazma wajiandae kukosa chuo hao.Good observation! Ni siasa tu na ndio maana Ndalichako alikataa kuchakachua matokea ili shule za kata zionekane zimefaulu sawa na za binafsi. Wakamuondoa! Huyu wa sasa mpuuzi anasema kwa majivuno eti shule za wanainchi ziko sawa na za binafsi wakati likijua fika kuwa wamechakachua marks!
We umeangalia tu idadi ya ufaulu kuongezeka bila kuangalia alama za ufaulu (PRINCIPLES) kushuka..... teh teh teh teh! hakika unajadili kisiasa na sio kitaaluma! Mfano, C yazanani kwa sasa ni sawa na D.
mkuu F6 wanafurahia sana matokeo yao ila mda si mrefu wataanza kuitupia lawama TCU kwa kuwaacha wahitimu wengi huku wana sifa na vigezo vya kwenda vyuo vikuu baada ya admission capacity ya vyuo kujaa.Tatizo linarudi palepale kuwa serikali imeleta mpango wa BRN bila kuandaa miundombinu ya kupokea mazao ya mpango huo,mfano ni ongezeko la ufaulu wa wanafunzi hasa tunavyoona sasa wanafaulu sana masomo ya sayansi na ndio lilikua lengo lakini ukiangalia vyuo vikuu vilivyoongezeka tangu mpango huo uanzishwe ni vichache hususani vyuo vya afya kwa ngazi ya degree.Mfano mzuri ni mwaka jana tuliona jinsi idadi ya PCB na CBG walivyokosa vyuo vya afya kwa sababu ya competition na mwaka huu itakua zaidi ya mwaka jana maana wapo baadhi hawakwenda vyuoni wanaapply mwaka huu kwa hiyo mwezi wa kumi itakua ni lawama kwa TCU wakati hawana kosa lolote tatizo ni Necta.Kwa hiyo serkali imeleta brn bila kuandaa miundombinu ya kupokea mazao ya mpango huo
Ukiangalia matokeo ya form VI toka BRN ianzishwe yamekuwa yakipanda mwaka hadi mwaka.
Naomba tujadili wakuu.
Inashangaza sana miundo mbinu ile ile eti iliyokua inatumika miaka yote eti baada ya miaka ya BRN ufaulu umepanda ghafla Bini vuu. Hii si kweli kabisa mi haya matokeo kuanzia form four na form six ni ujanja ujanja tu na lazma wajiandae kukosa chuo hao.
Raisi ajae atie mkazo kwenye kuwekeza kwenye elimu sio kuongeza ma GPA eti ili kuonyesha ubora wa ufaulu. Yani ningekua na mtoto siwezi kumwacha asome shule zenye division five bora hata Kenya.
Kuboresha elimu sio kuongeza ufaulu kwa wanafunzi hata kama hawana vigezo. Hali ni tete sana kiukweli ka taifa tuna produce wasomi wasio na weledi kisa siasa na hivi ni mwaka wa uchaguzi. At the end of the day walalahoi ndo wataumia na uu mfumo mbovu. Warudishe ile system ya zamani ya na kutoa matokeo ki division na mitihani ya kidato cha pili.Kwel kabisa mkuu miundombinu ni ile ile tu sasa kilichobadili upepo wa matokeo mm hata Sikielewi
Hahahaha naona unaleta Utan mkuu...... Kwa taarifa yako watu walikuwa wanapiga msuli baraa hasa hiz comb za science na ndicho kilichofanya idadi kubwa wawe wanazikwepa hizo comb za science sio kama Sasa ambapo ni kimbilio la wengi ambalo nahisi ndo lengo kuu la serikal....... Kuhusu tuition zilikuwepo za kumwaga tu tena za wakali kuliko Hawa wa Sasa..... Kuna mtu alikuwa anaitwa Mkandawile,Mtiga Mchwampaka pia kuna mmoja alikuwa Makongo pale nimemsahau alikuwa a napiga biology balaa pia yupo Musa pale Mwenge na watu walikuwa Wana attend karibia zote hizo na bado huna uhakika kivile kutokana na ugumu wa masomo yenyewe
Basi nyinyi vichwa vyenu vilikua matope kama walimu walikua hawagomi ,tuition za kutosha na team work then munazngusha pole yenu
Munailaumu BRN wakati hamjui ukweli kuhusu BRN
Iyo B+ Unayoilalamikia haina tofauti na B ya enzi hizo
Na C ya BRN inatofauti kubwa na C ambayo ulisomea ww
C ya BRN =4
C uliyosomea ww =3
Kwenye BRN ukipata C tatu utakua na 12 point ambayo ni Credit .
Kwenye Elimu yako ukipata C tatu = 9 ambayo ni division two
Je uoni utofauti?
Kipindi ww unasoma D ilikua inaanza 21 mpka 40,
Ila kwenye BRN inaanzia 30-39 yaani Leo hii mtoto akipata alama 21 -29 kwenye mtihani ni failed aihesabiwi je na hapa auoni tofauti?
Hata hivyo waacheni watoto wang'ae ni wakati wao wanajituma acheni wivu
Na hii BRN inawapoteza sana watoto Wa shule za kata kwasababu wengi wao ufaulu wao uanzia alama 60 kushuka chini ,wale Wa vijijini ndio kabisa uanzia 40 kushuka chini mwisho Wa siku wanajikuta wana ZERO ila ingekua enzi zenu hakosi Div Four kutokana na D za 21,22,23,24,25 ,26 n.k
Na kinachoshangaza zaidi kuna wanafunzi wengine matokeo ni yao lakini hawayaamini anajua alichokifanya na jinsi matokeo yalivyokuja ni tofauti na makadirio yake.Mwingine alifanya mitihani kumaliza akatathmini akasema biology anaweza akapata C cha ajabu matokeo yanakuja ana B+.Ukiangalia wengi wanaobisha hapa ndio wahitimu wenyewe wa F6 2015 hawawez wakaelewa nini kinazungumzwa maana sasa wana furaha na matokeo ila muda utafika ndio watajua nini kinazungumzwa,wapo baadhi wanasema watu wana roho mbaya juu yao,wala hamna mwenye roho mbaya hapa jukwaani kwamba alitaka matokeo yawe mabovu au F6 wafeli kwa karibu 50% ya waliofanya mtihani,ila kila mtu ametoa mchango wake kulingana na alivyotathmini matokeo hayo na kuona wazi kwamba hayakustahili kwa kiasi hicho kuwa hivyo na mfumo huo ukiendelea utaharibu elimu ya hapa nchini.Wenyewe hawajiulizi mbona matokeo ya miaka ya nyuma hayazungumziwi? wapo watu humu wameshuhudia matokeo mengi ya necta kila mwaka na kulinganisha na mwaka huu kwa hiyo wanachoongea wanauzoefu nacho.Sasa wakiambiwa wanaanza kusema watu wana roho mbaya na wao mara nini....ila ni mtazamo tuu
End of the day msikariri , BRN au Zamani, ufaulu ni ufaulu tu, binafsi nafurahi sana ... Sababu mitihani ya kibongo unatungiwa ili ufeli.. Na wala sio kukupima ... Natamani A -leval waiondoe pia , maana jirani zetu wanaishia form 4 alafu chuo.
Sometimes mabadiliko yanahitajika , tulivo soma sisi miaka hiyo ni tofauti na miaka hii ya sasa ...
Kama unadhani miaka hiyo elimu ilikuwa nzuri one yako ndio iliyokuwa ya ukweli good for u.... Subiri uje uwahadithie wajukuu zako kuhusu enzi zetu...
Mkuu Saydou naona unaongea kitu usichokifahamu vizuri...... Nimekuelezea kuhusu tuition, group work, kujituma umenielewa Sasa umekuja na matope hiyo ni kashfa anyway tuache hayo ya matope........ Nasema hujui unachoongea kwasababu hiyo C ya Zaman ni Sawa na B ya brn mkuu ambapo ukiwa nazo 3 ilikuwa ni 1.9 na si div 2 kama ulivyosema....... Ukifanya comparison ya grade za Zaman na Sasa unajua inamaanisha nn?..... Jibu ni kwamba elimu ya Zaman ilikuwa bora kuliko hii ya Sasa........ Na hizo D za Zaman 21,22,23 nk ndo C ya BRN kwa sasa..... Bado hujagundua kitu tu hapo mkuu?
Hakuna kitu kama hicho D za zamani kwenye BRN ni E na hazihesabiwi ukipata E inakula kwako ,sawa B- ya BRN ni sawa na C ya zamani
Lakini kinamba B plain ya BRN ni sawa na namba 3 ambayo haina tofauti na C ya zamani ambayo kinamba ilikua inahesabika 3
Ili mwanafunzi Wa BRN apate kufaulu vizuri kwa upande wa advance inambidi apate B+ tatu angalau watu watamzungumzia