ElimuTiba: Jinsi ya kujieleza kwa Daktari


kweli kabisa madaktari wengi wa Tanzania wakiona kuna wateja wengi hulipua kazi kwa kudanganya kwani Mwezi uliopita nusura nikione kifo baada dr. Wa hospital moja binafsi kuniphma kwa haraka haraka na kusema nina Malaria 3 na kunipa dawa zake ila baada ya masaa mawili nilizidiwa sana na kukimbizwa hospital nyingine na kukutwa na Malaria imezidi mwilini na doctor kugomba sana na kusema huyo aliyenipa dozi ya Malaria 3 kafanya kosa sana, na ningechelewa kidogo tu mbona ningekwenda ila namshukuru Mungu na huyo doctor kwa kunipigania hadi kuokoa maisha yangu
 
Kumuona Daktari: Orodha ya unachohitaji kujua

Itakuwamiujiza ikiwa madaktari watawahudumia kila mgonjwa, kwa kuchunguza

historia yao ya afya na jamii zao, wakiuliza maswali ya kujenga uhusiano

kama:Wahitaji msaada gain kutoka kwa daktari? Je waweza kuzungumzia kuhusu

historia ya afya yako bila uoga? Mbona ulimuacha au hukwenda kumuona daktari

wako wa mwisho? Ukweli: Wagonjwa ni wengi na muda ni haba na madaktari lazima

wafanye kazi kwa madhubuti, ufasaha na haraka.


Kwa hivyo, labda uwe ni miongoni mwa matajiri walio na uwezo wa kuwasiliana na


wauguzi kwa simu(ni ndoto nzuri), lazima ujiandae kukutana na daktari ukifahamu

vyema unachotarajia na kufatilia kana kwamba afya yako inakitegemea.



Kabla hujamuona daktari


Ni vyema kufahamu unavyojihisi na uhakikishe unaweza kuelezea mambo muhimu

yanayokusumbua kabla ya kumuona.Uweze kuelezea dalili za maradhi na lini

yalikuanza.Ikiwa huwezi kujieleza vizuri, ziandike au andamana na rafiki

unayemthamini au jamaa yako ili akusaidie.


Hapa kuna baadhi ya vitu vichache ambavyo unatarajia daktari kuuliza, jitayarishe

kwa miadi naye kwa kuweza kujibu.


Ufahamu:


  • Majina ya madawa, miti shamba na vitamini unayotumia.
  • Uwe na historia ya afya ya jamaa yako, pamoja na historia ya shinikizo ya damu, kisukari, ugonjwa wa moyo, saratani na magonjwa mengine.
  • Eleza hali yako ya afya zamani na sasa, dalili au upasuaji wowote uliofanyiwa.
  • Eleza kwa kina ikiwa umewahi kulazwa kwa vyumba vya dharura, lini, wapi, kwa nini na jinsi ulivyofatilia na muuguzi wako wa kawaida.
  • Eleza majina, anwani na simu za madaktari walio kutibu zamani na wale wanaokutibu sasa.
  • Eleza kwa kina mzio wowote ulionao kwa madawa, chanjo, mazingara pamoja na pumu, ukurutu na kadhalika.
  • Elezea kuhusu pombe, sigara na madawa yoyote yasiyotoka kwa mtaalamu au hospitalini.
  • Toa habari kuhusu bima yako
 
pia dr. anawajibika kupata taarifa muhimu zinazo mpeleka kwenye utatuzi wa tatizo, hata kama mgonjwa hana uwezo wa kujieleza!
 
Dokta ninatatizo la mguu huwa nikisimama zaidi ya dakika tatu huwj mguu unaniuma kwa ndani na si kwenyemisuli naomba ushauri wako
 
Kuna tatizo limemtokea mdogo wangu ameota meno mawili ya juu ya fidhi na yamekuwa makubwa kiasi ambacho yanaonekana je a naweza kuyatoa? Na akiyatoa hayana madhara? Kwa baadae?
 
Explanatory modal..
Cool subject ...ila still wanaojua kujieleza ni wachache mno na tena ukiwaangalia sana ni wale waloendelea..a mean educated..

Wazo langu...daktar anatakiwa awe mtulivu kisha aumuulize mgonjwa kilaza swali mojamoja mpaka ajiridhishe na ugonjwa huo..wa huyo mtu...
As far as you know wabongo wengi wamezoesha na mila zao kuwa mganga ni kuhani..just you go there..keep quite..then doctor aanze kuelezea matatizo yako kama wafanyavyo sangomaaa...
Thanx ni hayo tu..
 
Mimi nilichogundua Watanzania wengi hatuwezi kujieleza popote tu si kwa Daktari tu, hiyo inasababisha na daktari awe harsh, mfano mgonjwa anaingia kwa Daktari anaulizwa unaumwa nini? kichwa ananyamaza, akiulizwa na nini? na mgongo, kingine nakohoa, kingine ninamafua, ulianza lini? juzi. Hapo Daktari anajua kuna foleni huko nje inamsubilia yeye aihudumie halafu mgonjwa mmoja tu anamaliza lisaa lizima, kwanini umchoshe daktari kwa kukuuliza maswali mengi ambayo ungefika ukajieleza tu ninaumwa hiki na hiki nilianza siku flani nakadhalika, hapo unamrahisishia dkt na unaokoa mda na utamfanya akuhudumie vizuri kwasababu hujamchosha.
 
Nashukuru sana kiongozi, Umenipa picha nzuri namna ya kuuliza maswali kwa mgonjwa pia kupata maelezo ya ugonjwa wake. Panapo uzima na neema za Mungu baada ya miaka 3 nitaongeza nguvu huku Sewahaji!
 
Ninasumbuliwa na uvimbe wa moyo upande wa kushoto sehemu ya chini ya moyo, nimeangalia ecg na ecko ikagundulika hivyo, nitumiea dawa gani
 
Ninasumbuliwa na uvimbe wa moyo upande wa kushoto sehemu ya chini ya moyo, nimeangalia ecg na ecko ikagundulika hivyo, nitumiea dawa gani

Mkuu hilo neno 'Uvimbe wa Moyo' si la kawaida sana katika mawasiliano kati ya daktari wa kitanzania na mgonjwa wake.
Hata hivyo naamini kabla ya kufanya vipimo hivyo ulimuona daktari especially daktari wa magonjwa ya kawaida(ndani) aka phycisian.Ni vizuri ukayarejesha majibu hayo kwa daktari husika ili mjadili na kupeana aina ya matibabu yanayofaa.
 
Mkuu Nimecheka sana kuhusu hilo jina lako :smile-big::smile-big::smile-big:


Nini Maana ya Neno (Meningitis)?



Meningitis ni uvimbi wa bongo.[SUP][1][/SUP] Kuvimba huku kunasababishwa na virusi, au bakteria au hata

pia kutumia dawa fulani. Meningitis ni maradhi yanayoweza kuuwa kwa ajili ya kuwa uvimbe huu

hufanyika karibu na bongo; kwa hivyo ugonjwa huu ni dharura umwone daktari.Dalili kuu za

ugonjwa huu ni kuumwa na kichwa na shingo, pamoja na homa na kuchanganyikiwa kwa akili,

kutapika na kutoweza kustahamili mwangaza na kelele.


 

mkuu hii siyo tafsiri sahihi ya 'meningitis' labda ndio sababu ukacheka.
 
Some time minaona Dakitari ndo akuu ulizee hayo maswali nawew ndoo uyajibu naujielezee unavyo jisikia kan kazi yake Dakitar niipi bana ? Yani wee ufikee tunakuanzaa kujisimuliaa siatakuambia mbona unajua kilakitu si ujipime nakujitibu peke ako yani ni hatua kwa hatua bana minaona unaulizwa nawe ujibu ndo utapata msaada mzuri apo nayeye akakueleza inavyo takiwa ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…