Eliud Kipchoge avunja rekodi yake mwenyewe na kuwa mwanariadha wa kwanza kukimbia KM 42 kwa chini ya saa 2

Eliud Kipchoge avunja rekodi yake mwenyewe na kuwa mwanariadha wa kwanza kukimbia KM 42 kwa chini ya saa 2

Huku Bongo sipati Picha yaani CCM nazani wakina Polepole wangekuwa kila Dakika wanafanya Press na kusema huyo anaiwakilisha CCM.

Sijasikia Mkenya akisema eliud kipchoge anawakilisha chama fulani.

CCM jifunzeni kutoka kwa Eliud kipchoge. Pale anawakilisha nchi sio Chama
 
Kumbe ataandika historia na sio kuvunja rekodi....na hii ni kwasababu anakimbia mwenyewe na pia uwepo wa pacemakers ambao wanaingia na kutoka. Ila all in all inatuweka vizuri wanaafrika mashariki kwenye uso wa dunia hususan kwenye michezo.
 
Kumbuka rekodi iliyopo sasa hivi ameishikilia yeye, hivyo hata kama ni kuivunja atakua anavunja rekodi yake mwenyewe.
Halafu hilo la pacemakers kubadilishana, kwangu mimi sioni kama poa, yaani kama umewahi kukimbia mbio za masafa marefu, kuna sehemu huwa unafika na kuwa kama mzimu, kiasi kwamba ukishtukizwa shtukizwa na watu wanaojiunga na kutoka itaanza kukuponza.
Mbio za masafa marefu unafaa ufike sehemu na kujisahau na kusahau mazingira yaliyokuzunguka, unajsklizia tu na kuhakikisha mguu mmoja upo mbele ya mwingine, haifai kushtukizwa kihivyo.
 
Much love from the 254[emoji1139]! M-Pesa logo.
MyXMj9hzR1XzGFo4svLPqIxIWuiMfPA_jT3qZQQfhQht74JyeDtRw7hvyGtQhFEOBBS2ZACS3q3HHL5D_ohUXVNUqrbp=s750

3D display at the KICC.
kicc_pix.jpg
 
Amefika umbali ambao marathon huanzia, yaani kilomita 30 ndio patamu maana kuanzia hapo binadamu huwa kama mzimu.
 
Kuna wadau pembeni wanajaribu kuchomoka naye nduki, ila wanazima baada ya kama hatua mia moja, hapo ndio unaweza ukaelewa ilivyo shughuli ngumu kwa jamaa. Kukimbizana naye hatua mia moja unahema kishenzi.
 
Back
Top Bottom