Eliud Kipchoge avunja rekodi yake mwenyewe na kuwa mwanariadha wa kwanza kukimbia KM 42 kwa chini ya saa 2

Eliud Kipchoge avunja rekodi yake mwenyewe na kuwa mwanariadha wa kwanza kukimbia KM 42 kwa chini ya saa 2

Sasawa mr. Vi emoji..
Haya rudi kwenye mada...
Manake kw kupenda mipasho, hujambo..
Thread zote unazo comment 99% huaga upo nje ya mada
Tatizo huwa mnatumia makwapa kufikiria ndio maana hamuwezi kuona kitu,
Mfano mdogo jana niliwaambia mthibitishe kitu mmeshindwa, bla bla nyingi.
 
Huku Bongo sipati Picha yaani CCM nazani wakina Polepole wangekuwa kila Dakika wanafanya Press na kusema huyo anaiwakilisha CCM.

Sijasikia Mkenya akisema eliud kipchoge anawakilisha chama fulani.

CCM jifunzeni kutoka kwa Eliud kipchoge. Pale anawakilisha nchi sio Chama
Yaani unamlinganisha eliud na makonda..ufipa mna utapiamlo wa akili..
Mfananishe eliud na samata...
 
Ni ngumu kumeza hii, huyu Mkenya anataka kufanya kitu ambacho hakiingii akilini, sijui nini anawaza muda huu, neno 'badass' litapata maana na tafsiri mpya leo.

Mbio zenyewe ataanza 09:15am
Kwa watani wetu wa Kusini, ili kuwapa picha ya umbali anaokimbia chini ya masaa mawili, ni kama kutoka Dar hadi Mlandizi, kwa ndugu zangu hapa Kenya hiyo ni kama kutoka Nairobi hadi Lari.

TV nyingi duniani zitapeperusha moja kwa moja mubashara, hata zetu hapa Kenya naona zimeweka live, anajadiliwa kitaani nyumba kwa nyumba. Muhimu sana maana inawapa hamasa vijana wengi kwamba linawezekana na itawezekana.

Pia kampuni ya Youtube inapeperusha mubashara

----UPDATE----

Eliud Kipchoge ran a staggering 1:59:40, shattering the mythical sub-two marathon barrier as he completed the #INEOS Challenge in majestic fashion on the streets of Vienna

--
ELIUD KIPCHOGE: MWANARIADHA WA KWANZA KUKIMBIA KM 42 KWA CHINI YA SAA 2


Mwanariadha raia wa Kenya, Eliud Kipchoge ameweka rekodi ya kuwa Mwanariadha wa kwanza Duniani kumaliza mbio za marathon kwa muda wa chini ya saa mbili
View attachment 1230550
Kipchoge mwenye miaka 34, amekimbia Kilometa 42.2 kwa kutumia muda wa saa 1, dakika 59 na sekunde 40 kwenye michuano ya Ineos 1:59 huko Vienna, Australia

Hata hivyo, rekodi hiyo haitatambuliwa kama rekodi rasmi Ulimwenguni kwasababu ameweka rekodi hiyo katika michuano isiyo ya wazi

Aidha, katika jaribio lake la mwisho kutaka kuweka rekodi hiyo mnamo mwaka 2017 alishindwa kwa sekunde 25


Kelele zooote kumbe haitambuliki...hata mie nina rekodi yangu ila haitambuliki...
 
Hivi ni kweli kipchoge ana miaka 34 tu !!!!! ???? ni macho yangu au nae anatumia maji ya mende kwa sana
 
Aiseee dahh ni sheedah mazeee...jamaa anatupiga promo ya hatareeeee, ila dah kwa wenzetu naona safari tv inawaonesha wahdzabe wakikula kobee!!😁🐸
Safi sana.. kumbe mnaangalia safari tv. Sisi huku hatuna taimu na tv za kenya.
 
Hahaa mavuvuzela wa ccm ungesikia wakisema ni juhudi za rais...wakti kenyata kampa 60m KSH kama zawadi ingekua jiwe angempa 10m na kiwanja burigi
[emoji23][emoji23][emoji23] eti Burigi nimecheka da!
 
Jamaa alikuwa anakimbia sawa na mtu anayeendesha mountain bike.
 
Watanzania na wivu
IMG_20191012_140347.jpeg
 
Dah kumbe tunaomfuatilia huyu jamaa tuko wengi! KIPCHOGE anakimbia balaa hana masikhara, kuna moja nilimuona MO-FARAH anajaribu kuleta ushindani lakini raundi ya mwisho alitepeta jamaa akamaliza mbio wa kwanza.
 
Ile ya AUSTRIA jana aliwaacha mbali sana wenzie na kuvunja record ya dunia, dah jamaa anastahili tuzo zaidi ya ile aisee anawakilisha Africa kwenye riadha.. WABONGO TUNASHINDWA WAPI? MAANA HATUNA MCHEZO TUNAOONGOZA.
 
Back
Top Bottom