Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Tajiri namba moja duniani anayemiliki mtandao wa Starlink ameiambia wazi wizara ya ulinzi ya Mareknani kuwa sasa itabidi waanze kugharamia mawasiliano hayo kwa Ukwani.Amesema kama ni sadaka tayari keshatoa zaidi ya dola milioni 80 kwa ajili ya vfaa 20000 ambavyo vimekuwa ni nguzo ya mawasiliano ya jeshi la Ukraine baada ya minara yote ya mitandao ya simu za mkononi kubomolewa na Urusi.
Akizidi kuipasha Pentagon Musk amesema iwapo kasi itakuwa hii kwa misaada yake ifikapo mwishoni mwa mwaka itakuwa ametumia dola milioni 100,Siwezi tena.....
Taarifa hiyo si ya mdomo na kupitia twitter yake pekee bali tayari ameshaiandikia Pentagon tangu mwezi uliopita.
Kuonesha jinsi vifaa hivyo vilivyo muhimu kwa Ukraine mshauri wa raisi Zelensky,Mykhailo Podolyak amebainsisha serikali yake itafanya kila juhudi ili mawasiliano hayo yaweze kuendelea.Akasema Musk amewasaidia sana kwa muda mrefu na biashara yake ina haki ya kuendelea kujimudu.