Elon Musk ainununua Twitter, atimua viongozi wa juu

Wewe mwenye ukubwa mbona hakuna chochote cha maana ulicho achieve duniani.
Nimeachieve vingi mno. Yaani furaha yangu nikiwa naingia kwenye chumba cha mgonjwa mfano mgonjwa anaongea na simu ananiona kwenye kioo cha mlango naingia anamwambia anaeongea nae usikate huyu yupo kind. That's my achievement. Nikimaliza kumuattend mgonjwa ananiuliza na kesho ni wewe upo zamu ?Yaani that is my biggest achievement. Furaha yangu ni biggest achievement. Sihitaji kuwa billionea ndo nione kuwa nimeachieve in life. To be honest nimeachieve vingi mno kuliko huyo Elon mwenye stress. Anasema anaondoka twitter mara huyo anarudi, inaonyesha hawezi kujicontroll.Mara awaambie watu waondoke WhatsApp wajiunge telegram kisa tu anamuonea wivu Mark.Unajua kwa nini hana account insta wala fb wala WhatsApp ?Chuki zake kwa Mark .Iam sure jinsi Mark anavyopitia magumu kwa sasa .Elon atakuwa anafurahia mno.
 

Kwahiyo Trump kina kanye watarudi [emoji23][emoji23][emoji23] twitter itachangamkaa haswaaa
 
Hauwezi kuufikia huo ubilionea maisha yako yote mkuu. Labda umuandae mwanao.

Awe smart sana kama hao kina Musk,

halafu aondoke Bongo akaishi nchi za Magharibi huko kisha aje na idea inayohitajika dunia nzima pamoja.
Unakaa jamii forum na kupoteza muda uwezi pata utajiri huo
 
Yah hata mimi halafu ana na ujanja ujanja jana baada ya kuinunua aliingia makao makuu ta Twitter akiwa amebeba sink sijui alikuwa anamaanisha anaenda kuondoa uchafu ambao ndio hao viongozi aliowatumbua
Ile kubeba sink in humor, sasa si kila binadamu ana akili ya kutafsiri humor au si kila mtu ana sense of humor.

Kubeba sink alimaanisha let it sink in. Sasa nakupa assignment , katafute maana ya sentensi isemayo
LET IT SINK IN
 
Unakaa jamii forum na kupoteza muda uwezi pata utajiri huo

Unafikiri akina Musk hawatumii social networks? Kutumia social networks si kupoteza muda (Panga ratiba zako vizuri) na kujifanya uko busy 24/7 hakutakupa utajiri wa kiwango cha Elon.
 
Taratibu dadaangu.

Kuna tofauti moja kubwa sana kati yako wewe na Elon Musk.

Wewe unahitaji kutuambia mafanikio yako, ila Musk hahitaji kufanya hivyo. We all know what he has done to this damn world. All humans are equal, but Elon Musk is "More equal" than other humans.

Alafu aliekuambia Elon Musk ako na stress ni nani? Wewe deal na wagonjwa wako (and I really appreciate your service), ila kijana Elon Musk sio mtu kwa sasa, amefikia kua taasisi. Wanapigana Ukraine na Russia, Musk is involved through his satellite services. Talking about global free speech, amevunja kibubu 44 billion USD ili walimwengu tubwabwaje kwa uhuru.


Utakua mwehu kama bado utaamini you have achieved more than him!

Pass my humble greetings to your patients, wish them a quick recovery on my behalf!
 
Sababu ya kupata Twitter ni kwa sababu ni muhimu kwa mustakabali wa ustaarabu kuwa na eneo la kawaida la mji wa kidijitali, ambapo imani mbalimbali zinaweza kujadiliwa kwa njia nzuri, bila kutumia vurugu,” Musk aliandika. "Kwa sasa kuna hatari kubwa kwamba mitandao ya kijamii itagawanyika katika vyumba vya mwangwi vya mrengo wa kulia na kushoto ambavyo vinazalisha chuki zaidi na kugawanya jamii yetu."
 
Inabidi afanye kazi ya ziada sana,kama amedhamiria ataweza,maana baada ya kutweet 'the bird is free nowe' jamaa wa Jumuia ya Ulaya wakamwambia ndege wako afuate sheria zetu tu vinginevyo atakumbana na kibano.
 
Inabidi afanye kazi ya ziada sana,kama amedhamiria ataweza,maana baada ya kutweet 'the bird is free nowe' jamaa wa Jumuia ya Ulaya wakamwambia ndege wako afuate sheria zetu tu vinginevyo atakumbana na kibano.
Hahah kwahyo saivi EU/ UN inaana kufuatilia content za mitandao ya kijamii?
 
Huwa ninamuona ana utoto flani. Kuna kipindi bwana alisema anapumnzika kutweet. Kwani aliweza basi ?Mara pap karudi Twitter. Kainunua Twitter ili kumkomoa Mark wa Meta.
Rahisi kumiliki but atakapoanza kuitwa congress ndio atajua mkono wa serikali utamuumiza pakubwa..

Ana mizaha na utoto fulani mwingi

Zack alisiginwa na congress hana hamu yupo kama hayupo…
 
Rahisi kumiliki but atakapoanza kuitwa congress ndio atajua mkono wa serikali utamuumiza pakubwa..

Ana mizaha na utoto fulani mwingi

Zack alisiginwa na congress hana hamu yupo kama hayupo…
Elon yeye anasema twitter itakuwa na uhuru watu waandike wanavyotaka.Kama ulivyosema kweli anajidanganya kwanza anaweza sababisha twitter iblokiwe nchi nyingi.Unajua Meta kuna limits otherwise kina Mange angekuwa hafungiwi insta. Sasa Elon anataka iwe kama jalala watu watukane wanavyotaka.
 
Bado hajarudishwa, ile acc ni kama Parody though limekuwa verified. Fatilia vizuri wanasiasa wa Marekani wanabet/guess juu ya Trump anaweza kurudishwa Twitter au Laah!

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…