Embassy Hotel na Motel Agip: Nini hasa kilitokea?

Kuna moja nasikia ina mauza uza, sasa sijui ndo hiyo Embassy au Agip.

Ila ni ile iliyoko makutano ya Pamba Road na Sokoine Drive, nyuma ya New Africa.
 
Kwa muonekano wa hii iliyokuwa Embassy hotel na muda iliyokaa bila kutumika yaweza kuwa na hitilafu hivyo mmiliki hana budi kuishusha chini tu.!
 
Sasa habari imeshasema wazi kwamba hotel ina mgogoro wa kisheria, halafu tena unahoji kwanini serikali haijamnyang'anya wakati haiendelezi!!

Sasa anaiendeleza vipi wakati umeshaambiwa kuna mgogoro?!

Nakumbuka somewhere in 2012 or 2013 ilizungushiwa mabati huku tukiamini inataka kufufuliwa lakini bila shaka inashindikana kwa sababu ya huo mgogoro!!
 
Kuna ile Motel Agip Hotel pia imeachiwa imekufa hivi hivi ilikuwa bomba sana na misosi yao ilikuwa si ya kawaida.
Ile Motel Agip nadhani ilikuwa ya Mgiriki mmoja aliyekuwa mmiliki wa hotel inayoitwa Serena hivi sasa pale mwanzoni ikiitwa Sheraton, hata kile kiwanja alipojenga kilileta mgogoro kwa wananmichezo wa timu ya kikapu ya Pazi kama sijakosea pale ndio walikuwa wakifanyia mazoezi pia nadhani ilikuwa sehemu ya klabu ya Gymkhana,Mzee Rukhsa ndie alikitoa kwa yule mgiriki kama alivyotoa Loliondo(?) kwa mwarabu wa Oman, enzi za Rukhsa wenye nazo nao walijichotea kwelikweli hasa watu wa rangi.
 
Kesi zipo mahakamani wafanyakazi wanadai haki zao ...tangu isimame hadi leo unalipa ndefu duuuu
 
Agip Hotel Na Embassy hotel imekuwa "danguro" kwa watoto wa IFM.
Serikali imeva miwani mweusi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…