Embassy Hotel na Motel Agip: Nini hasa kilitokea?

Embassy Hotel na Motel Agip: Nini hasa kilitokea?

Kuna ile Motel Agip Hotel pia imeachiwa imekufa hivi hivi ilikuwa bomba sana na misosi yao ilikuwa si ya kawaida.
Kweli kabisa. Wewe una kumbukumbu nzuri ya Motel Agip hasa kuhusu misosi. Hadi leo hii mimi binafsi, sijashuhudia hotel ya kiwango chake kwenye eneo la vyakula.
 
Kweli kabisa. Wewe una kumbukumbu nzuri ya Motel Agip hasa kuhusu misosi. Hadi leo hii mimi binafsi, sijashuhudia hotel ya kiwango chake kwenye eneo la vyakula.
Chinese restaurant pale under ground ya kitega uchumi
 
Nipo hapa mitaa posta mpya najaribu kuvuta siku ipite kutafuta riziki, maana kuna usemi wa wahenga unasema riziki ya mbwa ipo miguuni kwake.

Sasa ndugu zangu nimegeuza macho naona hili jengo naambiwa ilikuwa hotel moja kali sana miaka ya 80 kwa jina Embassy Hotel Dar es salaam, Lakini hapa kuna uzio wa mabati na nikicheki kupitia madirishani naona makorokoro kama viti, meza makochi nk.

Hili eneo ni very potential, wakongwe tujuzeni kuna nini kuhusu hii Hotel iliyotamba mno miaka hiyo leo kugeuka na kuwa kiota cha bundi?

Ni hayo tu kwa asubuhi hii.
 
Hotel Hizo na Mali kadhaa za Umma zilipitia hujuma kubwa zikauzwa kwa bei chee...Hiyo ikachukuliwa na Wale jamaa wanaomiliki Wet n Wild....Lakini Imekua doro mpaka leo.
Mkuu bado sijaridhika, yaani hata JPM na urudishaji wake mali za umma alikwama kuigusa? haiwezekani
 
1627634366738.png
 
Hii hotel ilikuwa na hadhi sana ilikuwa inashindana na New Africa Hotel miaka ya 80, kulikuwa na supermarket karibu hapo, maeneo ya hapo Posta palikuwa tulivu sana na pasafi, Askari Monument naye alikaa vzr miaka hiyo.

Timu nyingi za mipira na timu za Taifa nchi mbalimbali zilifika hapo Embassy Hotel na wageni wengi kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi walifikia hapo.

Embassy Hotel, nakukumbuka sana kwa Huduma zako nzuri, ulikuwa unakimbizana na mpinzani wako New Africa Hotel na jirani mwingine Kilimanjaro Hotel
 
Poor management nayo ilichangia,nakumbuka kuna mrembo alikuwa reception mid 90s alikuwa mpigaji mzuri sana wa dola na kupangisha vyumba akishirikiana na walinzi.

imagine mshahara wake ulikuwa elfu themanini lakini alikuwa anarudi home na kama laki nne kwa siku baadaye mkinga wa Peacock akamchukua.

pale napo akapiga sana na hivi mkinga alikuwa mshamba anamwambia usichukue malipo kwa dolaaa ndiyo akapata mwanya mwingine wa kupiga.RIP Dada Uncle wangu alikupenda sana.
 
Ni kati ya mali za umma zilizoangukia mikononi mwa mafisadi. Maamuzi ya kuziendeleza yalikwama siku nyingi kwa sababu wahusika wakuu kwenye huo mgogoro ni wakubwa tu wenye maslahi yao ambao waliishastaafu.

Siyo hiyo tu, Kuna nyingine mbili zilizokuwa Icône ya Jiji .... Twiga Hotel na Motel Agip zote zimebakia kuwa magofu ya Serikali....Skyway Continental zote zimebaki majina tu.
 
mkuu bado sijaridhika, yaani hata JPM na urudishaji wake mali za umma alikwama kuigusa? haiwezekani
Jpm ndio alitaka mji uwe mchafu hivyo,enzi za nyuma posta palikuwa mahali patakatifu,sio siku hizi eti unakuta mtu yuko posta kavaa dera anachoma mihogo kwa kuni,mbele kuna benki pembeni jengo la ubalozi,zamani machinga mwisho kariakoo.
 
Hata kariakoo hakukua na machinga, maana walikua wanawindwa na migambo wa city.
 
Ni kati ya mali za umma zilizoangukia mikononi mwa mafisadi. Maamuzi ya kuziendeleza yalikwama siku nyingi kwa sababu wahusika wakuu kwenye huo mgogoro ni wakubwa tu wenye maslahi yao ambao waliishastaafu.
Siyo hiyo tu, Kuna nyingine mbili zilizokuwa Icône ya Jiji .... Twiga Hotel na Motel Agip zote zimepakia kuwa magofu ya Serikali....Skyway Continental zote zimebaki majina tu.
Nasubiri nione Ngorongoro mountain lodge itaangukia wapi?.
 
Kwa kweli imebaki Gofu tu... Hakuna Hata anayejishughulisha na hiyo Hotel....

Inasikitisha.....
 
Back
Top Bottom