Emergency fund: Unatumia njia ipi kujiwekea aina hii ya akiba?

Mkuu, Emergency Fund ni muhimu kuwekwa kwende acc ambayo itakua easily accessed lakini sio ya matumizi yako ya kawaida.
Unaweza ijaza mara moja au ukawa unaijaza kila baada ya mda (maybe monthly) kutokana na ukubwa wa majukumu yako, mazingira au maana ya emergency kwako. Mfano emergency fund ya mtu ukiwa na familia (lets say mke na watoto) inatofautiana na akiwa mwenyewe.

N.B. Emergency Fund inahitaji discipline sana kuitunza ila ni muhimu sana kuwa nayo. Wengi hua wanajikopesha emergency fund na hawarudishi 😅
Basi mwenyewe nawekaga kwenye wallet laki halafu jumatatu najikuta na alf 30,, emergency fund kibongobongo ni bima ya afya tu,, mengine tusidanganyane ingawa ni muhimu sana hii kitu,,
 
😅😅
 
Inawezekana ila inahitaji nidhamu kubwa ya hela. Kuweka kwenye wallet ni kujitia majaribuni mwenyewe. Usiziweke kwenye hela za matumizi. Weka kwenye separate acc.
 
Kuweka Akiba ya dharura huwa nafanya hivi

Bank ua naweka Mil 1 hii huwa haitoki hata iweje inakaa kwa ajili Kama itatokea dharura isaidie kununua Chakula , cha miezi 6.

Na katika account ya kawaida huwa najitahidi isikose hela ya kutumia miaka 3

Katika simu huwa inakaa hela ya kununua chakula kila mwezi unga, mchele mafuta ,gas n.k

Ndani kwangu huwa inakaa hela ya mboga , kununua dawa za maumivu,vocha, sabuni na mambo madogo madogo.

Mfukoni huwa natembea na hela ndogo Sana haizidi buku tano.
chai + ujivuni + Ego

Hakuna uhalisia hapo.
 
Emergency fund kama pesa kwa kweli sijaweza kufanikiwa kuwa nayo.

Nachofanya ninavyo Vito vya thamani hasa dhahabu( Pete na mikufu) vinasaidia sana ikitokea dharura.

Ukihitaji pesa ya haraka haraka unaenda kwa sonara unaweza kito chako cha thamani wanakipima unachukua pesa yako fasta bila kusumbuana na mtu.

Kwa ufupi hiyo ndio njia ya kujiokoa mkwamo ukitokea kwa sisi wa kariakoo, ilala na magomeni.

Dhahabu au Vito vya thamani vya dhahabu havijawahi kushuka thamani.
 
Sonara huwa anademand ya hizo products muda wote.

Kwenye emergency fund naona msisitizo mkubwa ni mtu kuwa na liquid assets ( assets zinazoweza kugeuzwa cash faster bila mzunguko), Nyumba au viwanja hizo sio Liquid assets, unaweza ukafa njaa na unanyumba.
 
Upo sahihi kabisa.
Vijana wa zamani, mabaharia au watoto wa mjini walikuwa wakivaa hereni za dhahabu au cheni nzito za thamani kama liquid asset ndio maana kipindi kile ukivaa cheni au mkufu, wakiuona na wakikuona zoba unakabwa au kupigwa loba.

Baharia au mjanja yoyote mtoto wa mjini ilikuwa ni lazima umiliki Vito vya thamani na endapo ikitokea umepata umauti au umeugua basi wenzako watachukua Vito vyako watavithaminisha kwa sonara wanapata cash inakusaidia. Ulishawahi kusikia mabaharia au vijana wa enzi hizo wakichangishana au kutembeza vibakuli vya michango wakipata msiba au majanga? Jibu ni hapana walikuwa wakitegemea asset zao ni ilikuwa ni lazima au utamaduni kila mtu kuwa na asset zake.

Fanya tafiti ndogo nunua kito cha thamani halisi sio English gold katika jewelry yoyote kariakoo ukitoka nenda katika jewelry nyingine utauza fasta na utapata pesa
 
Wazo zuri sana. Nitalìafanyia kazi. Maana sisi watu wa imani, tunaamini haya waliyokuwa wanafanya maharia ndio alikuwa anafanya babu Ibrahim. Alipotaka kununua plot kwa ajili ya kumzikia mke wake aliuza sehemu ya assets zake na dhahabu zilikuwa ni sehemu ya pato lake.
 
Back
Top Bottom