Eminem aongoza orodha ya Rappers wanaotoza mkwanja mrefu kwa collabo moja

Eminem aongoza orodha ya Rappers wanaotoza mkwanja mrefu kwa collabo moja

Ila Eminem amekuzwa Sana kuliko uhalisia,ana flow ya kiwaki Sana kama analazimisha rap afu rap haimpendi.hit song zake za kuhesabika ila ndio hivyo ana kismat.sijawahi kumuelewa huyu mwamba
Sema hujawahi muelewa Ila kusema hitsong za kuhesabika nakataa, unamlinganisha na nani mwenye hitsong nyingi?
 
Majarida mbalimbali nchini Marekani yameorodhesha rapper 10 ambao wanachaji kiasi kikubwa sana cha pesa kwa ajili ya kumshirikisha kwenye wimbo wako wowote ule.

Katika orodha hiyo mkongwe Marshall Bruce Mathers III alimaarufu kama Eminem kwenye umri wa miaka 50 amewafunika vijana wengi sana kwenye suala la kuchaji kiasi cha pesa ili umshirikishe kwenye wimbo wako.

Eminem anachaji dola milioni 3 sawa na Tsh 7,020,000,000/= yaani bilioni saba huku akifuatiwa na Drake ambaye anachaji kiasi cha dola milioni 1 ambazo ni sawa Tsh 2340000000/= yaani bilioni 2.34.

Katika orodha hiyo rapper ambaye wengi hawakutarajia ni J Cole ambaye anachaji dola 2,000 kwa neno moja kwenye wimbo wako ambayo ni sawa na Tsh 4,680,000/= yaani milioni nne na laki sita za Kitanzania kila neno kwenye wimbo wako inategemeana na maneno mangapi.

Katika orodha hiyo wengi wame-comment wakishauri Future anatakiuwa kuongeza malipo yake huku wakisema kuwa dola laki mbili na nusu ambazo ni sawa nna T sh 585,000,000/= yaani zaidi ya milioni mia tano sio saizi yake.

Unahisi kwa Tanzania msanii gani anaongoza kutoza kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya collabo??

Credit: Bongo5View attachment 2550616
Future what
 
Ila Eminem amekuzwa Sana kuliko uhalisia,ana flow ya kiwaki Sana kama analazimisha rap afu rap haimpendi.hit song zake za kuhesabika ila ndio hivyo ana kismat.sijawahi kumuelewa huyu mwamba
Uzungu una mbebaa, hana lolote kwan sijawahi muelewa mie.
 
Back
Top Bottom