Eminem ndiye rapper bora kuwahi kutokea, kikwazo ni rangi

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264


Siwezi kuongea kwa niaba ya watu wenye asili ya africa wote wanaopenda hip hop, wawe wabongo, wamarekani weusi, waingereza , n.k, lakini wacha nitoe maoni yangu, Eminem is the goat (great of all time),

bigie na 2pac walikuwa hot lakini nadiriki kusema vifo vyao vilikuwa vikubwa mno kuliko muziki wao, ni kama Neymar na Mbappe wangetutoka mapema, hakika majina yao yangekuzwa mno kuliko walipo kwa sasa, Watu wangekua wanaamini Neymar na mbappe ndio wangekuwa wanastahili Ballon Dor kila mwaka. Kuijua stable longetivity ya msanii ni kitu muhimu sana,

Kwangu mimi hali ni tofauti, huwa sijali rangi, nachojali ni lyrics, delivery, word play, kucheza na speed, pumzi, nk, na hapa ndipo napojua hakuna msanii wa kumfikia eminem kukitendea miujiza kipaza sauti na kutumia kalamu vizuri kuandaa lyrics amazing.

Sote tunajua hip hop ilitengenezwa na kuchochewa na watu weusi, na hapa ndipo kuna baadhi ya watu wenye hii asili wanakuwa wagumu mno kukubali uhalisia kwamba Eminem ni mzungu na anafanya poa zaidi ya rappers weusi, hisia zinatumika kupinga badala ya kutumia akili kukubali ukweli.

Laiti Eminem angekuwa ni mweusi, basi ni wazi kabisa eminem angechukua ni Michael Jackson wa Hip hop

Pia ukija huku kwenye mitindo huru frreestyles na cyphers, eminem yuko vizuri.

Waliowahi kuingia 18 zake wengi walipotezwa, pengine cheo sahihi cha kumpa Eminem ni "Un-beefwithable"

Nimeweka videos za mnyama anakamua live hapa, karibu kuzicheki





 
Mkuu unajua Auto tune? Eminem ametoka kizazi feki na ile sio sauti yake ukimuweka live hawezi kurap vile anatumia sauti fake (Auto tune, distortion, overlap etc) ndio maana hawi regarded kama mwana Hiphop bora.

Kina rakim, 2pac, Nas, B.i.g Jay Z etc wanakuwa regarded kama bora zaidi.
 
Cheki mnyama anavyokamua live na hapa umri ushaenda

 
mtoe nas mweke nikki mbishi hapo
 
Kwa mara ya kwanza mkuu ntatofautiana na wewe.....
Live Em anarap vizuri tu, freestyle yupo vizuri tu.
Ntashare hata baadhi ya freestyle zake nilizonazo ikibidi....
Auto tune? Asilimia ngapi ya nyimbo zake ni auto tune?
When Am gone, Stan, Cleaning out my closet, ni auto tune......?
 
Binafsi eminem ndio best, lakini nikiwaza walichofanya big na pac kwenye umri mdogo nakosa majibu kabisa
 
Nitafutie not afraid live
Ule wimbo kuna vipengere anaimba na sio kurap

kumbuka eminem ni rapper na sio mwimbaji

kuna sehemu zenye high notes ilibidi ziwekwe auto tune ila kuna wengine husema anatumia mbinu ya zamani, unaimba chorus mara 4 then unazi overlap moja juu ya nyingine ili sauti iwe kama autotune,

hivyo sehemu za ku sing kuna msaada, ila kwenye ku rap vitu ni og.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…