TANZIA Emmanuel Lukumai, Mwenyekiti wa CHADEMA Bagamoyo afariki dunia

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426


Taarifa kutoka Kanda ya Pwani ambayo imetolewa na Katibu wa Kanda hiyo Hemed Ally inaeleza kwamba Mh Lukumai amefariki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na Matatizo ya Upumuaji.

Mh Lukumai alikuwa Mgombea ubunge wa Chadema wa Jimbo la Bagamoyo kwenye kile kilichoitwa uchaguzi Mkuu wa October 2020.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi, Amina.
 
Mungu amrehemu, pole nyingi kwa makamanda wote.
 
Tanzania na corona sasa imekuwa siasa na watanzania wanaendelea kupotea kila saa kila siku. Ndugai yeye kajificha.
 
Poleni
 
Mungu ampe pumziko kamanda.....huu ugonjwa hauchagui mpinzan wala chama tawala......kila kifo kimebeba machungu kwa wapendwa na watu wa Karibu.......kushangilia kifo cha mwanadamu mwenzako ni ushetani......Pumzika Kamanda wana bagamoyo watakukumbuka kwa harakati zako za kupigania demokrasia.........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…