TANZIA Emmanuel Lukumai, Mwenyekiti wa CHADEMA Bagamoyo afariki dunia

TANZIA Emmanuel Lukumai, Mwenyekiti wa CHADEMA Bagamoyo afariki dunia

View attachment 1708091

Taarifa kutoka Kanda ya Pwani ambayo imetolewa na Katibu wa Kanda hiyo Hemed Ally inaeleza kwamba Mh Lukumai amefariki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na Matatizo ya Upumuaji.

Mh Lukumai alikuwa Mgombea ubunge wa Chadema wa Jimbo la Bagamoyo kwenye kile kilichoitwa uchaguzi Mkuu wa October 2020.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi , Amina .
Nini gonjwa mama? Covid 19?
 
Mungu ampe pumziko kamanda.....huu ugonjwa hauchagui mpinzan wala chama tawala......kila kifo kimebeba machungu kwa wapendwa na watu wa Karibu.......kushangilia kifo cha mwanadamu mwenzako ni ushetani......Pumzika Kamanda wana bagamoyo watakukumbuka kwa harakati zako za kupigania demokrasia.........
Amina
 
Kwa hiyo
Tanzania na corona sasa imekuwa siasa na watanzania wanaendelea kupotea kila saa kila siku. Ndugai yeye kajificha.

Kwa hiyo tanzani sio sehemu ya dunia sio?
kwa wale wanaokufa huko nchi za watu wao wanapenda kufa au sio watu?
Ukiona ndugai kajificha na wewe jifiche sasa unatafuta nini wakati ni haki yako kujificha?
 
Wa CCM wakifa kwa Corona chama mfu cha CCM kinatangaza kuwa wamekufa kwa ugonjwa wa moyo au wamekufa kwa ajali.Yaani serekali ya CCM inapambana na Corona kwa kujidanganya kuwa Corona haipo!Shame on you!
 
Usiku wa kuamkia leo nilikuwa hospital fulani.. Kuna mtumishi wa serikali alilazwa hapo,aliwekewa oxygen..wiki nzima anayo..bahati nzuri anaendelea kupata nafuu.. Usiku akaletwa mzee mwenye hela zake (75+) pumzi imembana..,hamna mashine ya oxygen,zote zipo kwa wagonjwa.. Kimbembe kikaanza,vijana wa mzee wakalazimsha itolewe ya mtumishi(50),ambaye ameanza kupata ahueni.. Dr na nurses wakakomaa hakuna kutoa..wakampa mzee rufaa hosp ya mkoa na mtungi wa oxy,ulikuwa nusu.. Kwa kuwa yule mzee ni maarufu,ikapigwa simu kwa DC...wamekataa kuondoka...... Waliokuwa zamu wameitwa kwa DC ...
 
Covid19 imekuja kutufundisha kitu flani Kama Watanzania.
Wachumia siasa wachache, mwanzo walifkri kuwa Corona ikiingia Tanzania Basi itadhuru CCM au watu wa serikali tu, wakasahau kuwa Corona Ni janga la yeyote na halibagui chama Wala dini Wala kabila..

Acha Tuendelee kupata fundisho mpaka pale unafik utakapotupungua.
 
RIP Kamanda Lukumay.

Tatizo la kupumua linamaliza wazee na vijana Tanzania.

Tuchukue hatua sahihi za kujikinga dhidi ya janga la korona.
 
Back
Top Bottom