TANZIA Emmanuel Lukumai, Mwenyekiti wa CHADEMA Bagamoyo afariki dunia

TANZIA Emmanuel Lukumai, Mwenyekiti wa CHADEMA Bagamoyo afariki dunia

Corona sio Chadema Wala CCM!!

Tukiacha siasa ndio mapambano yataanza!!
Na nafikiri hatuko mbali kuacha siasa kwenye hili!
R.I.P
 
Badala ya kukaa na kucoments coments zenye vinasaba vya kisiasa huku watu wanaisha ni bora kupaza sauti zetu kwa jamii kuchukua tahadhari zaidi kwa faida ya jamii yenyewe.
Hata Rais atoke leo na kututangazia kuwa korona ipo, hilo tangazo halitapunguza vifo kama sisi wenyewe hatutochukua hatua.
 
View attachment 1708091

Taarifa kutoka Kanda ya Pwani ambayo imetolewa na Katibu wa Kanda hiyo Hemed Ally inaeleza kwamba Mh Lukumai amefariki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na Matatizo ya Upumuaji.

Mh Lukumai alikuwa Mgombea ubunge wa Chadema wa Jimbo la Bagamoyo kwenye kile kilichoitwa uchaguzi Mkuu wa October 2020.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi, Amina.
Magufuli is more dangerous than covid
 
..Pole kwa familia, ndugu, jamaa, na marafiki.

..MUNGU ailaze roho ya Emmanuel Lukumai mahala pema peponi.
 
Watu wanaisha kwa kweli.. Wiki.inayoisha Leo nimepoteza marafiki/work mates 2(mid 40s), graduates..bado walioko kwenye oxygen(2).. Boss wetu ana,anazo dalili zote,amejitenga home... Ni kama akuna kazi ofisini,simanzi
 
Back
Top Bottom