TANZIA Emmanuel Majura amefariki Dunia

Mungu ni mwema kila wakat ,na tunapaswa kushukuru Kwa kila jambo
 
Apumzike kwa amani
 

RIEP Emmanuel. Ulikuja bila kutaka na unaondoka bila kutaka. Sijui huyo Mama kama yuko hai anajisikiaje kumkimbia mtoto wa miezi sita.
Lazima alikuwa gaidi fulani anayestahili kukaa Guantamo bay
 
DUnia tunapita. Apumzike kwa amani ya bwana sote kwake tutarejea
 
Ni muhimu kuwa na utaratibu wa kujitathimini sana maisha yetu ili tusiwe tunakufuru na kujiona sisi ni victims wa ugumu wa maisha na matatizo yake na kumbe tuna bahati na fursa kibao za kuishi maisha ya furaha kama tukiridhika na maisha anayotupa muumba.
Huyu kijana kama sio kukataliwa sijui tuite kitu gani sasa hiki. Imagine baba yako mzazi anakukataa na haujazaliwa,mama yako mzazi anakuacha na watu wasio kujua ila wanachagua kujitolea kukulea kama damu yao. Ila bado hata baada ya watu hawa kukukubali na kukupenda shetani bado hajakubali akaamua akupe ugonjwa ambao anajua utakutesa na kukutenga na upendo wa watu hawa ambao wamejitolea kukupa familia na upendo ambao wazazi wako walishindwa.

Hii imekaaje wajameni? Mimi kwa upande wangu tukiitazama kiimani naona nguvu ya giza ilimuandama sana huyu mwanetu. Shetani huwa anajua wateule wa MUNGU hata kabla hawajazaliwa na ndio maana huanza vita yake hata kabla hata ya mteule mimba yake haijatungwa sababu mteule m'moja akifanikiwa kwake Shetani ni pigo kubwa sana kwa himaya yake ya kuzimu.

Hebu jiulize why baba akimbie mtoto ambaye alimtengeneza mwenyewe?

Sawa tufanye baba hana uchungu wa mwana kumshinda mama, ila MAMA MZAZI wa mtoto ambaye ndie kamleta,sio kaachiwa,kamleta yeye hapa duniani kwa uzao wake leo anamkimbia mtoto na kumuacha na watu baki ambao si damu yake.

Bado haijatosha baada ya kupata makazi mapya still shetani hajakubali akaona amfuate na kumtia maradhi ambayo yatamdhoofu na mkum'maliza.

Najua wengi hatujui namna shetani anafanya kazi zake. Kujua ni ngumu sana kwa akili ya kawaida unatakiwa kuwa na akili zaidi ya kawaida kumuelewa shetani na mitego/vikwazo vyake anavyokuwekea.

Usione watu wana maisha ya amani na utulivu na yasiyo na vikwazo ukadhani shetani hawaoni. Anawaona ila anapata shida kuwaingilia sababu ya ukaribu waliojiwekea na MUNGU.

Ndugu zangu,tujiweke karibu na MUNGU upo salama pengine kwasababu ya maombi ya bibi yako aliyomuomba MUNGU kumlindia kizazi chake kuanzia yeye hadi uzao wasaba. Baraka kidogo zisikufanye ubweteke ukaacha kuzungumza na MUNGU ukaendesha maisha kwa kanuni zako.

Usijiweke karibu na MUNGU kwasababu unahisi unakaribia kufa, kufa mapema sio mpango wa MUNGU hata siku moja. Jiweke na MUNGU kwasababu unataka ulinzi wakati ukiishi huu ulimwengu uliozungukwa na mipango ya shetani kila sehemu kuharibu baraka za watu.

Ukisimama na MUNGU sio tu wewe utakuwa salama ila hata wale wanaokuzunguka na hata utakao waleta kupitia uzao wako watakuwa chini ya ulinzi wake.

MUNGU aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi na ampe tena njia nyingine salama ya kurudi ulimwengu huu kuja kuifanya kazi yake aliyotumiwa kuja kuifanya awali katika mazingira salama na upendo bila mashambulizi ya shetani kumzunguka.
 
apumzike kwa aman
 
Mshana , nilikuwa out of contact kwa siku kama 5 hivi. Kikao cha kamati kuu ya chadema walitoa azimio gani kuhusu uchaguzi?
Your browser is not able to display this video.
 
Japo sometimes naweza kulaumu Ila huwa naiepuka kufuru kwa sababu dunia ni nzito sana kwa baadhi ya watu. Mungu ampumzishe maana sijui ilikuwa ngumu kwake kwa kiwango gani na matumaini gani alikuwa nayo.


Rest in peace 🙏🏽
 
RIEP Emmanuel. Ulikuja bila kutaka na unaondoka bila kutaka. Sijui huyo Mama kama yuko hai anajisikiaje kumkimbia mtoto wa miezi sita.
Lazima alikuwa gaidi fulani anayestahili kukaa Guantamo bay
 
 
Wakuu,
Tusitungishe mimba kama hatuna uhakika kwa kutoa sapoti ya malezi. Inahuzunisha mtoto anakuja duniani bila ridhaa yake na kula vumbi kali ila wazazi wapo tu.
 
Apumzike Kwa amani na Mungu awabariki wale wote mliojitolea kumsaidia naamini Mungu atawalipa
 
Apumzike kwa amani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…