TANZIA Emmanuel Majura amefariki Dunia

TANZIA Emmanuel Majura amefariki Dunia

R.I.P kijana.Jamani huyo mama yake ana roho ngumu mtoto uliembeba tumboni miezi tisa unamtelekeza.Inaumiza Sana ameishi Bila kujua ndugu zake WA damu.
Undugu wa damu wakati mwingine ni ujinga! Unaoishi nao karibu ndio ndugu zako hao!
 
Sihuzuniki na misiba Tena Kwa maana najua ni njia ya lazima Kila binadamu kupita
Hata sie tuliobaki tutapita huko.
Babu mmoja wa mika 90 alikuwa anasema hivi hivi kama wewe. Tena yeye alikuwa anaongezea na kibwagizo cha ''nimeona mengi ya dunia, niko tayari muda wowote, wala msilie''. Siku moja dume la ng'ombe likakata kamba na kuanza kufukuza watu..... alikuwa wa kwanza kutimua mbio utadhani ni Usain Bolt! Alipoulizwa vipi tena si ulisema uko tayari muda wowote? Alibaki kucheka tu...
 
Simjui ni nani ila apumzike kwa amani!

Inasikitisha sana mtoto analetwa duniani halafu anatelekezwa kabisa na wazazi wake.

Hakuna mtoto anayejileta mwenyewe hapa duniani.

Inatia simanzi sana.

Pole zake huyo dogo kwa yote aliyoyapitia.
Hauyajui ya wawili.Nyamaza.
 
Kwa masikitiko makubwa, nawajulisha kwamba ndugu yetu Emmanuel Majura amefariki dunia. Imma alikua mwanafunzi wa mwaka wa pili, akisomea uongozaji wa Filamu Taasisi ya sanaa Bagamoyo (TASUBA), akisomeshwa na GH Foundation.

Kwa wale mnaokumbuka Imma amekua na historia ngumu tangu utoto wake. Inadaiwa Mama yake alipewa mimba na mwanaume ambaye aliikataa. Kwahiyo akamzaa Imma na alipofikisha miezi 6 maisha yakawa magumu sana. Hivyo akaenda kuomba kazi za ndani kwa mzee Majura aliyekua mstaafu wa shirika la reli.

Lakini mama Imma alitoroka na kumuacha Imma kwa mzee huyo akiwa na miezi 6 tu. Mzee Majura alimlea Imma kama mjukuu wake na akamsomesha hadi alipomaliza kidato cha nne. Lakini alipata infection kwenye ngozi ya juu inayofunika ubongo (dura mater) na akaharibika sehemu ya fuvu lake upande wa mbele, akawa anatoka usaha masikioni na puani.

Alifanyiwa operation mbili KCMC bila mafanikio. Lakini watanzania kwa umoja wetu kupitia GH Foundation tulimsaidia akaletwa MOI ambapo alifanyiwa operation 3 ikiwemo ya kuondoa sehemu ya fuvu iliyoharibika na kuwekewa fuvu bandia (bone cement). Imma alipona na akaamua kurudi shule, ambapo alichagua kwenda kusoma Uongozaji wa filamu, Taasisi ya sanaa Bagamoyo (TASUBA).

Imma amefariki jana jumapili huko Bagamoyo na ibada ya mazishi itafanyika kesho jumanne chuoni TASUBA, kisha maziko yatafanyika katika makaburi ya Kikristo Bagamoyo mjini.

Mungu awabariki wote mliopata nafasi ya kugusa maisha ya Imma alipokua hai. Katika umri mdogo wa miaka 23 amepitia magumu mengi. Kwa bahati mbaya amekufa bila kuwajua ndugu zake wa damu, lakini angalau Mungu alituinua sisi kuwa ndugu zake. Kwaheri mdogo wangu Imma, tutaonana tena ng'ambo ya mto 😭😭
Credit: Malisa G.J
View attachment 3173474
Dah, Mungu amlaze mahala pema peponi
 
imenihuzunisha na kuniumiza sana historia yake fupi ya maisha.
 
R.I.P kijana.Jamani huyo mama yake ana roho ngumu mtoto uliembeba tumboni miezi tisa unamtelekeza.Inaumiza Sana ameishi Bila kujua ndugu zake WA damu.
RIP kijana mwendo umeumaliza. Mama yake anaroho ya Huruma na Hofu ya Mungu ndo mana katafuta mahali salama pa kumwacha(kwa Majura)kuliko wale wanao zaa na kumtupa mtoto jalalani au chooni.
 
Kwa masikitiko makubwa, nawajulisha kwamba ndugu yetu Emmanuel Majura amefariki dunia. Imma alikua mwanafunzi wa mwaka wa pili, akisomea uongozaji wa Filamu Taasisi ya sanaa Bagamoyo (TASUBA), akisomeshwa na GH Foundation.

Kwa wale mnaokumbuka Imma amekua na historia ngumu tangu utoto wake. Inadaiwa Mama yake alipewa mimba na mwanaume ambaye aliikataa. Kwahiyo akamzaa Imma na alipofikisha miezi 6 maisha yakawa magumu sana. Hivyo akaenda kuomba kazi za ndani kwa mzee Majura aliyekua mstaafu wa shirika la reli.

Lakini mama Imma alitoroka na kumuacha Imma kwa mzee huyo akiwa na miezi 6 tu. Mzee Majura alimlea Imma kama mjukuu wake na akamsomesha hadi alipomaliza kidato cha nne. Lakini alipata infection kwenye ngozi ya juu inayofunika ubongo (dura mater) na akaharibika sehemu ya fuvu lake upande wa mbele, akawa anatoka usaha masikioni na puani.

Alifanyiwa operation mbili KCMC bila mafanikio. Lakini watanzania kwa umoja wetu kupitia GH Foundation tulimsaidia akaletwa MOI ambapo alifanyiwa operation 3 ikiwemo ya kuondoa sehemu ya fuvu iliyoharibika na kuwekewa fuvu bandia (bone cement). Imma alipona na akaamua kurudi shule, ambapo alichagua kwenda kusoma Uongozaji wa filamu, Taasisi ya sanaa Bagamoyo (TASUBA).

Imma amefariki jana jumapili huko Bagamoyo na ibada ya mazishi itafanyika kesho jumanne chuoni TASUBA, kisha maziko yatafanyika katika makaburi ya Kikristo Bagamoyo mjini.

Mungu awabariki wote mliopata nafasi ya kugusa maisha ya Imma alipokua hai. Katika umri mdogo wa miaka 23 amepitia magumu mengi. Kwa bahati mbaya amekufa bila kuwajua ndugu zake wa damu, lakini angalau Mungu alituinua sisi kuwa ndugu zake. Kwaheri mdogo wangu Imma, tutaonana tena ng'ambo ya mto 😭😭
Credit: Malisa G.J
View attachment 3173474
Nini kime muua huyu kijana elimu ya nyota inahusu hasa ukisoma history yake.
 
Back
Top Bottom