Undugu wa damu wakati mwingine ni ujinga! Unaoishi nao karibu ndio ndugu zako hao!R.I.P kijana.Jamani huyo mama yake ana roho ngumu mtoto uliembeba tumboni miezi tisa unamtelekeza.Inaumiza Sana ameishi Bila kujua ndugu zake WA damu.
Babu mmoja wa mika 90 alikuwa anasema hivi hivi kama wewe. Tena yeye alikuwa anaongezea na kibwagizo cha ''nimeona mengi ya dunia, niko tayari muda wowote, wala msilie''. Siku moja dume la ng'ombe likakata kamba na kuanza kufukuza watu..... alikuwa wa kwanza kutimua mbio utadhani ni Usain Bolt! Alipoulizwa vipi tena si ulisema uko tayari muda wowote? Alibaki kucheka tu...Sihuzuniki na misiba Tena Kwa maana najua ni njia ya lazima Kila binadamu kupita
Hata sie tuliobaki tutapita huko.
Hii ni lini? Mbona tunaambiwa Lissu na Mbowe hawasemeshani jamani? Na waandishi wa habari wanaripoti upumbavu!
Hauyajui ya wawili.Nyamaza.Simjui ni nani ila apumzike kwa amani!
Inasikitisha sana mtoto analetwa duniani halafu anatelekezwa kabisa na wazazi wake.
Hakuna mtoto anayejileta mwenyewe hapa duniani.
Inatia simanzi sana.
Pole zake huyo dogo kwa yote aliyoyapitia.
Dah, Mungu amlaze mahala pema peponiKwa masikitiko makubwa, nawajulisha kwamba ndugu yetu Emmanuel Majura amefariki dunia. Imma alikua mwanafunzi wa mwaka wa pili, akisomea uongozaji wa Filamu Taasisi ya sanaa Bagamoyo (TASUBA), akisomeshwa na GH Foundation.
Kwa wale mnaokumbuka Imma amekua na historia ngumu tangu utoto wake. Inadaiwa Mama yake alipewa mimba na mwanaume ambaye aliikataa. Kwahiyo akamzaa Imma na alipofikisha miezi 6 maisha yakawa magumu sana. Hivyo akaenda kuomba kazi za ndani kwa mzee Majura aliyekua mstaafu wa shirika la reli.
Lakini mama Imma alitoroka na kumuacha Imma kwa mzee huyo akiwa na miezi 6 tu. Mzee Majura alimlea Imma kama mjukuu wake na akamsomesha hadi alipomaliza kidato cha nne. Lakini alipata infection kwenye ngozi ya juu inayofunika ubongo (dura mater) na akaharibika sehemu ya fuvu lake upande wa mbele, akawa anatoka usaha masikioni na puani.
Alifanyiwa operation mbili KCMC bila mafanikio. Lakini watanzania kwa umoja wetu kupitia GH Foundation tulimsaidia akaletwa MOI ambapo alifanyiwa operation 3 ikiwemo ya kuondoa sehemu ya fuvu iliyoharibika na kuwekewa fuvu bandia (bone cement). Imma alipona na akaamua kurudi shule, ambapo alichagua kwenda kusoma Uongozaji wa filamu, Taasisi ya sanaa Bagamoyo (TASUBA).
Imma amefariki jana jumapili huko Bagamoyo na ibada ya mazishi itafanyika kesho jumanne chuoni TASUBA, kisha maziko yatafanyika katika makaburi ya Kikristo Bagamoyo mjini.
Mungu awabariki wote mliopata nafasi ya kugusa maisha ya Imma alipokua hai. Katika umri mdogo wa miaka 23 amepitia magumu mengi. Kwa bahati mbaya amekufa bila kuwajua ndugu zake wa damu, lakini angalau Mungu alituinua sisi kuwa ndugu zake. Kwaheri mdogo wangu Imma, tutaonana tena ng'ambo ya mto 😭😭
Credit: Malisa G.J
View attachment 3173474
Daaaah noma sanaaaaSihuzuniki na misiba Tena Kwa maana najua ni njia ya lazima Kila binadamu kupita
Hata sie tuliobaki tutapita huko.
Mke wangu ni weweMSIBA AMEKUFA MKE WAKO? PUMBAVU, SUBIRI MKE WAKO AFE THEN TUTAKUPA POLE NA KUACHA SIASA
RIP kijana mwendo umeumaliza. Mama yake anaroho ya Huruma na Hofu ya Mungu ndo mana katafuta mahali salama pa kumwacha(kwa Majura)kuliko wale wanao zaa na kumtupa mtoto jalalani au chooni.R.I.P kijana.Jamani huyo mama yake ana roho ngumu mtoto uliembeba tumboni miezi tisa unamtelekeza.Inaumiza Sana ameishi Bila kujua ndugu zake WA damu.
Nini kime muua huyu kijana elimu ya nyota inahusu hasa ukisoma history yake.Kwa masikitiko makubwa, nawajulisha kwamba ndugu yetu Emmanuel Majura amefariki dunia. Imma alikua mwanafunzi wa mwaka wa pili, akisomea uongozaji wa Filamu Taasisi ya sanaa Bagamoyo (TASUBA), akisomeshwa na GH Foundation.