Emmanuel Mbasha na Flora Mbasha wapatana

Emmanuel Mbasha na Flora Mbasha wapatana

chongchung

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2013
Posts
13,277
Reaction score
40,924
Stori: WAANDISHI WETU

HAKUNA neno zuri la kusema zaidi ya Mungu mkubwa! Ule mtafaruku ndani ya ndoa ya mwimba Injili mahiri Bongo, Flora na mumewe, Emmanuel Mbasha umedaiwa kumalizika kwa wawili hao kupatana, Risasi Jumamosi linakuwa nambari wani kukuhabarisha.
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, wawili hao walikalishwa kikao cha upatanishi mapema wiki hii kilichokuwa chini ya familia.
MANENO YA CHANZO
"Kikao cha familia kilikaa, Mbasha aliitwa akafika, Flora naye aliitwa akatokea, mazungumzo yalikuwa marefu lakini kimsingi waliamua kuweka kando mtafaruku wao na kuijenga upya ndoa yao," kilisema chanzo.

Chanzo kiliongeza kuwa katika kikao hicho cha mwanzoni mwa wiki hii, miongoni mwa adidu za rejea ilikuwa kutokumbushia vikao vilivyopita ambapo hakukupatikana muafaka.
VIKAO VILIVYOPITA
Katika vikao vilivyopita, wahusika wakuu walikuwa wazazi wa Mbasha (mzee Maneno Mbasha, Zulfa Maneno), ndugu wa Flora na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.


VIKAO VYA BAADAYE
Kwa mujibu wa chanzo, vikao vilivyofuata, wawili hao wakawa tayari kila mmoja ametema nyongo yake pembeni na kufikia makubaliano kwamba, ndoa yao isimame tena wakitumia maandiko kwenye Biblia kutoka kitabu cha Waebrania yanayosema: Ndoa na iheshimiwe na watu wote na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.

WAKORINTHO YAFUNGA KAZI
Kwa mujibu wa chanzo hicho, maneno mengine ya Biblia yaliyotumika kwenye kikao hicho mpaka wawili hao wakaamua kurudiana ni 1 Wakorintho 7:1-10 ambapo maandiko yanasema:
Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe. Mume na ampe mkewe haki yake vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake.


Flora Mbasha akiwa kwenye picha ya pamoja na mumewe, Emmanuel Mbasha.

Mke hana amri juu ya mwili wake bali mumewe vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake bali mkewe. Msinyimane, isipokuwa mmepatana kwa muda ili mpate faragha kwa kusali, mkajiane tena shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.
Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza, wala hapo si mimi, ila Bwana (Mungu), mke asiachane na mumewe, lakini ikiwa ameachana naye na akae asiolewe au apatane na mumewe, tena mume asimwache mkewe.
KIKAO CHA JUMAMOSI KUMALIZIA
Chanzo kilisema kuwa, kikao cha mwisho ambacho kitamalizia kuweka mambo sawa ili wawili hao waanze ngwe ya pili ya ndoa yao ambayo inaaminika itakuwa ya mwisho mpaka kifo kiwatenganishe, kinatarajiwa kufanyika leo jijini Dar es Salaam mahali ambapo hapakutajwa.


MWANASHERIA ATAJWA
Mwanasheria wa Flora aliyejulikana kwa jina moja la Ado ametajwa kusimamia kikao hicho ili wawili hao waanze maisha mapya baada ya safari fupi ya mvurugano uliowafanya kuwa mbalimbali.

AONGEA NA RISASI JUMAMOSI
Juzi, Risasi Jumamosi lilimsaka mwanasheria huyo kwa njia ya simu yake ya mkononi ili kumsikia anasemaje kuhusu kutajwa kwenye usuluhishi wa ndoa hiyo ambapo alipopatikana alisema:
"Niko Arusha, Ijumaa nitarudi Dar. Kuhusu kikao cha usuluhishi siwezi kukwambia lakini suala la kuwapatanisha nalifahamu, nawaomba na ninyi msaidie kufanikisha jambo hilo zuri."

VIPI KUHUSU KESI YA MADAI YA KUBAKA?
Hata hivyo, Wakili Ado hakutaka kugusia kuhusu kesi ya Mbasha iliyopo Mahakama ya Wilaya ya Ilala ambapo anadaiwa kumbaka shemejiye mara mbili (jina tunalo) ambayo kwa mujibu wa mahakama, upelelezi umekamilika na itasikilizwa Julai 17, mwaka huu.

KWA UPANDE WAKE FLORA
Risasi Jumamosi lilimwendea hewani, Flora ili kumsikia anasemaje kuhusu kuwepo kwa upatanishi kati yake na mumewe, Emmanuel.

Huyu hapa: "Ongea na wakili wangu atakwambia kila kitu." Ambapo majibu ya wakili yalikuwa: "Ninachojua mimi ni kwamba Flora ameshamsamehe mumewe na yuko tayari kuanza ukurasa mpya."
MBASHA SASA
Kwa upande wake, Mbasha alipozungumza na gazeti hili juzi alisema kurejea upya kwa ndoa yake ni jambo la kuupendeza moyo wake.

"Mimi sina neno nipo tayari, nimeshasamehe yaliyotokea, Flora ni mke wangu jamani, nampenda sana kutoka moyoni."
 
chongchung

Hii ni tamithiliya, au riwaya, sihitaji kutangaza mambo ya ndani kwenye media, au magazeti.
 
Last edited by a moderator:
Wenye ndoa hebu changieni hili......

Swali huko kwenye vikao Frola alikubali Kuwa ile Kesi ya Kubaka ilikuwa Feki? na hiyo kesi itafutwa au? Maana hapo ndipo penye kizungumkuti ! Hivi huyo mwanaume anajisikiaje baada ya kumegewa kisha watu wakasafisha nyumba yote sasa wanajidai kupatana
 
chongchung

Hii ni tamithiliya, au riwaya, sihitaji kutangaza mambo ya ndani kwenye media, au magazeti.

Kwa kweli hili jambo la kwenda kuleta kiringi cha mapaparazi na kuja kuwaonesha namna mnavyoishi ndani me halinibariki kabisa yan.
 
Sasa Mbasha Na Flora Wamerudiana, Mlotaka Waachane Sasa Mnaaibika. Bibi Na Bwana Wakigombana,waache Wenyewe Wataelewana, Ukileta Ujuaji Unaaibika Pakubwa,poleni Na Muache Majungu Na Uzush
 
Sasa Mbasha Na Flora Wamerudiana, Mlotaka Waachane Sasa Mnaaibika. Bibi Na Bwana Wakigombana,waache Wenyewe Wataelewana, Ukileta Ujuaji Unaaibika Pakubwa,poleni Na Muache Majungu Na Uzush

We si miongoni mwa wanaoshabikia mbasha afungwe? Si ulikuwa unashabikia kuwa mbasha ajibu tuhuma kama kabaka au hajabaka?? Wewe si ndo kibaraka wa gwajima wewe!!!.sasa huoni kuwa hii thread yako inakuhusu mwenyewe moja kwa moja....mana wewe na mungu mtu wako gwajima, mnapenda mbasha afungwe.
 
huu unaitwa uhayawani, hapa jf kuna member aliyempeleka mbasha jela?
 
Sasa Mbasha Na Flora Wamerudiana, Mlotaka Waachane Sasa Mnaaibika. Bibi Na Bwana Wakigombana,waache Wenyewe Wataelewana, Ukileta Ujuaji Unaaibika Pakubwa,poleni Na Muache Majungu Na Uzush

Waaibike thrice
 
we si miongoni mwa wanaoshabikia mbasha afungwe? Si ulikuwa unashabikia kuwa mbasha ajibu tuhuma kama kabaka au hajabaka?? Wewe si ndo kibaraka wa gwajima wewe!!!.sasa huoni kuwa hii thread yako inakuhusu mwenyewe moja kwa moja....mana wewe na mungu mtu wako gwajima, mnapenda mbasha afungwe.

hukuwa na ufahamu wa kumweleewa

ya rohoni waachie wa rohoni

ndoa imerudi kingine
 
hukuwa na ufahamu wa kumweleewa

ya rohoni waachie wa rohoni

ndoa imerudi kingine

Alicho kiandika kikowaz kabisaa.....fuatilia coments zake kwenye the bold utajua kuwa nae ni miongoni mwa mashabiki walikuwa wanapenda ndoa ivunjike
 
Hakuna kitu hapo

Gwajima kaamua kuyanyamazisha na dogo kabinywa ndude tu, mikandamizo inaendelea kama kawa
 
Sasa Mbasha Na Flora Wamerudiana, Mlotaka Waachane Sasa Mnaaibika. Bibi Na Bwana Wakigombana,waache Wenyewe Wataelewana, Ukileta Ujuaji Unaaibika Pakubwa,poleni Na Muache Majungu Na Uzush

Majungu na umbea hatuachi ndo kazi yetu na kuaibika kwenye umbea ni kama ajali tu
 
Sasa Mbasha Na Flora Wamerudiana, Mlotaka Waachane Sasa Mnaaibika. Bibi Na Bwana Wakigombana,waache Wenyewe Wataelewana, Ukileta Ujuaji Unaaibika Pakubwa,poleni Na Muache Majungu Na Uzush

Acha hizo : Majungu yapi? na Uzushi upi? Kuna Mtu aliwatuma wautangazie Umma migogoro yao ? Frola alichepuka kwa Raha zake kamaliza kiu sasa analudi kwake baada ya kumsweka Mbasha Jela kwa kutengenezea Kesi Feki , vipi sasa Kesi itafutwa Kimagumashi? au kesi watazuga unaendelea kisha baadae wadai Hakuna ushahidi?maana Bongo kila kitu kinawezekana ! Hata staili ya kuchepuka Pia Frola kabadili toka analogia sasa atakuwa Digtal ,mchungaji yupo kumbuka na kiu bado kipo, Tunawaomba hao Frola na Mme wake Wakigombana wasiwatangazie watu Michepuko Yao kisha waje na Maneno eti kuna Majungu na Uzushi ! Watambue Kuwa kila Mtu ana shida zake huku majumbani lakini wengi wanakomaa wenyewe mpaka wanamaliza . Ukumbike Pia jukwaa la JF limefanya kazi kubwa Kumrekebisha Frola hadi akajiludi wewe Mbasha huna budi kuwashukulu wana JF kwa kukurejeshea Tunda lako.
 
huu unaitwa uhayawani, hapa jf kuna member aliyempeleka mbasha jela?

Huyo SAM LOVE kachemsha kweli ! Kasahau Kuwa wana JF ndio wamemrejesha Frola kwake baada ya kumkosoa saana kadhalika kufichua Uovu wake sanjari na Historia yake ndipo Frola akazinduka toka Michepukoni na Kurejea kwao , Vipi Mbasha na Frola wamepima Ukimwi? Najua watu watasema hayo ni Yao Binafsi , lakini kumbuka walitutangazia shida zao na sisi tunawajibu.
 
Back
Top Bottom