End of the World: Nostradamus 2012, December 21 - Mayan Prophecy

End of the World: Nostradamus 2012, December 21 - Mayan Prophecy

Changia mjadala kwa imani yako wewe, tukianza kukosoa imani za watu hapa tutakuwa tunatoka nje ya mjadala. Labda mimi nikuulize, huyo yesu mnaemuita mungu alikuwepo miaka elfu mbili iliyopita. Kipindi hiko hakukuwa na teknolojia ta picha, je huyo tunaemuona kwenye maruninga ni yesu wawapi. Na biblia inasema ukristo ni dini ya wana Islael sasa wewe mmatumbi unayeamini katika kristo hiyo dini ni ya kwako? Na nani aliyekwambia yesu ni mungu!!!

Halikuwa lengo langu kukwambia haya, ila lengo langu ni kukukumbusha kuheshimu imani za watu km ambavyo mm naiheshimu yako.

Mkuu ubarikiwe, mimi binafsi siwezi kuchambua Uislam kwa sababu sina uelewa ni afadhali nikauliza kwa kujifunza, hali kadhalika Muislam hawezi kuelezea mambo ya imani ya kikristo. Ila anaruhusiwa kuuliza kwa maana ya kupata uelewa.
Kuheshimu imani za wengine ni jambo la muhimu sana mkuu.

Kwa imani yangu, siku ya mwisho ipo na inakuja, ila kuhusu lini, Biblia inatuambia hakuna mwanadamu ajuaye japo dalili zimetajwa.

"Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.
Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina,
wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu"

Mathayo 24:36-39
 
[h=3]MWISHO WA DUNIA WATAJWA[/h] WAKATI binadamu wakiendelea na mipango yao ya kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi kimazingira, kiulinzi na usalama, utabiri mpya wa kutisha unaonesha kuwa mwaka 2032 ndiyo mwisho wa sayari hii ya tatu katika mfumo wa jua.Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali katika mitandao ya internet, sayari iitwayo Nibiru, ambayo kisayansi inafahamika kama Planet X ipo njiani kuigonga dunia na hivyo kusababisha majanga mbalimbali kutokea.ITAONEKANA ANGANI KAMA MWEZIKwa mujibu wa mitandao hiyo ya kisayansi, sayari hiyo ambayo inaisogelea dunia kwa kasi kubwa, itaonekana kubwa na angavu wakati wa usiku angani na kuwa katika umbo la mwezi na hivyo kufanya miezi ionekane miwili...read more at HABARI,MATUKIO,PICHA MICHEZO,BURUDANI NA MATANGAZO KARIBU SANA KWENYE BLOG HII'INNOCENT MBWAGA'
Hiyo kali
 
Wanao tabiri mwisho wa Dunia wote ni wapinzani wa Mungu. ushauli wangu. ki Dunia: ishi kamakwamba Yesu atarudi baada ya miaka 1,000. ki Roho ishi kamakwamba Yesu anarudi na atafika baada ya saa moja ijayo
 
Ufufuo wa kwanza tayari umetoke, sasa ivi tunasubiri ufufuo wa pili, ambao mda wowote waweza kutumia. Na baada ya huu ufunuo wa pili ndipo mtangojea miaka alfu moja.
 
mambo ya udaku hayo bhana mwisho wa dunia pale utapokufa tuu.
 
Wewe naye hovyoooo. Sijui watu wengine mkoje kila siku join date ili? wewe changia alicholeta hutaki tambaa.
Usione mtu kajiunga karibuni ukamuona kuwa ndio mgeni. Mfano mimi baada ya kupoteza password imenibidi nikae kwanza nije nijiunge tena kwa jina lingine.

Mwanzo nilikuwepo toka 2011. Nikajiunga tena mwaka huu sasa muache hizo tabia na kujifanya JF ina wenyewe. Nyie wenye tabia hizo mnaboa.

Hahaaha! Lakini mara zote MBUZI MGENI ANAKUWA NA KAMBA MGUUNI, kila mtu humu ndani aliwahi kuwa mbuzi mgeni, si unajua unafananisha forum hii na mitandao mingine ya kijamii, baadaye ukishagundua mziki unavyochezwa humu ndani basi ushakuwa mwenyeji!
 
Mkuu ubarikiwe, mimi binafsi siwezi kuchambua Uislam kwa sababu sina uelewa ni afadhali nikauliza kwa kujifunza, hali kadhalika Muislam hawezi kuelezea mambo ya imani ya kikristo. Ila anaruhusiwa kuuliza kwa maana ya kupata uelewa.
Kuheshimu imani za wengine ni jambo la muhimu sana mkuu.

Kwa imani yangu, siku ya mwisho ipo na inakuja, ila kuhusu lini, Biblia inatuambia hakuna mwanadamu ajuaye japo dalili zimetajwa.

"Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.
Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina,
wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu"

Mathayo 24:36-39

Mwisho wa dunia unaozungumziwa hapa ni wa kisayansi zaidi, na si wa kiimani!
 
YESU ataoa? haahahaha, nyie kweli mmeishiwa!!!! yani mnawaza ngono tu...ndo mana mnaaminishwa kuwa kule peponi kutakuwa na vigoli (visichana vizuri) kibao!!!

Endelea na Imani yako achana na za wengine, mind your own business
 
Nimekupata mkuu, kama ni wa kisayansi haupo.

Kwa nini unasema HAUPO wakati kuna billions of moving bodies out there, na kuna evidence kwamba kuna unearthly bodies zilizowahi kuigonga dunia na kusababisha maafa makubwa, achilia mbali miripuko ya hatari which wiped out entire civilization! Anything can happen at any time, its just hard to predict exactly when!
 
Back
Top Bottom