The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 20,242
- 45,930
Tatizo haufanyi utafiti mkuuu hata nikikuuliza ni lini wanasayansi walisema hicho unachokisema hauwezi kuniambia, na hii hapa wala si mpya kama anavosema kanjanja wa shigongo! Hiyo Mathayo 16:27-28 nimeisoma, huo mstari wa 28 umeuelewa vizuri:"Truly I tell you, some who are standing here will not taste death before they see the Son of Man coming in his kingdom", generation ngapi zimepita hata sasa unangoja?
Na vile vile nikukumbushe mkuu, Biblia inapoongelea mauti ni ile mtu kufa kimwili akiwa dhambini. Ndio maana Yesu anasema mtu akimwamini yeye hatakufa bali atakua na uzima wa milele. Ndio maana licha ya kwamba unamwamini au haumwamini Yesu, miili yetu inafikia ukomo wake hapa duniani lakini kwa wale wanaomwamini, wanatumaini la kuishi Milele baada ya maisha ya hapa duniani.
Kwa hao wanafunzi ambao Yesu alikua nao, kama wangedumu katika imani hadi mwisho, wangekua na tumaini la uzima wa milele (Wasingekufa)
Yohana 3:36
Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.
Sitaki kutoka sana kwenye maada, sorry kwa kukuzonga na mambo mengi